Taarifa ya Mbunge ya kuomba radhi kwa kufika maeneo ya Bunge

TAREHE: 09/08/2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: KUOMBA RADHI KWA KUFIKA MAENEO YA BUNGE


Jana kunabaadhi ya vyombo vya habari viliandika kuhusu mimi kufika maeneo ya bunge la katiba Dodoma mnamo Jumanne tarehe 05/08/2014.

Ni kweli nilifika kwa na kujisajili bungeni Dodoma kwenye bunge la katiba.Kuhudhuria kwangu kulitokana na kutokuwa na taarifa za kutosha kutoka kwa viongozi wangu wa chama. Binafsi lilikwenda Dodoma ili kusubiri maelekezo ya viongozi wangu wakuu.

Baada ya kuwasiliana na viongozi wangu wa Bunge wa Chama ndipo waliponitaarifu kuwa wabunge wa CUF hawatahudhuria kama jinsi ilivyokubaliwa kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.Hivyo siku hiyohiyo nilindoka Dodoma na kurejea Dar es Saam na hivi sasa niko jimboni Masasi .Naomba radhi kwa wananchi wote ikiwa kujisajili kwangu bungeni bila kuwa na taarifa za kutosha kumeleta usumbufu kwa chama, familia yangu, UKAWA na wananchi.

Clara Mwatuka
0719568101
Mbunge wa Viti Maalum CUF-Mjumbe wa Bunge la Katiba