Taarifa ya usaili wa Jeshi la Polisi Tanzania kwa wakazi wa Mbeya

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, BARAKAEL .N. MASAKI – ACP anawatangazia Wananchi wote ya kuwa orodha ya majina ya vijana waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2013 na cha Sita mwaka 2014 na kuchaguliwa kufanya usalii wa kujiunga na Jeshi la Polisi inapatikana kwenye tovuti ya Polisi: www.policeforce.go.tz au wafike ofisi ya kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya iliyopo Forest jirani na Mahakama kuangalia majina yao.

Muhimu:
  • Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha kwenye jedwali hapo juu ili mradi tu awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi halitahusika na lawama yoyote ile kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili hali ambapo jina lake si miongoni mwa walioitwa kufanya usaili.
  • Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s) ], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
  • Mwombaji awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa.
  • Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.

Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia muda wa kuanza usaili.

TAREHE YA USAILI KWA MKOA WA MBEYA NI 28.09.2014 HADI 01.10.2014. SAA 08:00 ASUBUHI HADI 10:00 JIONI.