Taarifa ya uteuzi wa Dkt Msonde kuwa Katibu Mtendaji NECTA


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Charles Msonde kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA).

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam jioni ya jana, Alhamisi, Agosti 14, 2014, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa uteuzi huo ulianza juzi, Jumatano, Agosti 13, 2014.

Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Msonde alikuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo la mitihani.

Dkt. Msonde anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Joyce Ndalichako, ambaye amerudi kuendelea na kazi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kumaliza likizo yake ya kujinoa (Sabbatical Leave).

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

15 Agosti, 2014