Inaelekea kumebakia suitafahamu au tafsiri fulani kuhusu matokeo ya uchaguzi wa DMV 2014 kufuatia takwimu za kura tulizotoa na kuwasilisha kwa bodi ya DMV.
Tamko hili linaweka wazi mshindi katika kila nafasi iliyogombaniwa. Hivyo kwa mujibu wa matokeo ya kura na wa katiba, wafuatao ndiyo viongozi wapya wa jumuia yetu kwa miaka miwili ijayo:-
RAIS- Iddy Sandaly |
MAKAMU WA RAIS - Harriette Shangarai |
KATIBU- Saidi Mwamende |
MAKAMU WA KATIBU- Bernadetta Kaiza |
MWEKA HAZINA- Jasmine Rubama |
Tamko hili pia limefikisha Kamati ya Uchaguzi wa 2014 kwenye tamati yake.
Mungu ibariki DMV, na adumishe mshikamano imara wa Watanzania.”
Safari Ohumay
Mwenyekiti