Tangazo kwa wote waliochaguliwa kujiunga JKT

Tangazo lililotolewa na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, JKT, linasema kuwa, jeshi la Kujenga Taifa linawatangazia vijana wote waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa Sheria kuwa wanatakiwa kuripoti kwenye makambi waliyopangiwa kuanzia tarehe 04 Septemba 2014 kwa mafunzo yatakayoanza rasmi tarehe 11 Septemba 2014.

Aidha, tangazo hilo linasema kuwa JKT inakanusha uvumi unaosambazwa kwa kutumia ujumbe mfupi wa njia ya simu "SMS" na kwenye mitandao ya kijamii kuwa mafunz hayo hayatakuwepo. Taarifa hii si ya kweli bali ni uzushi na upotoshaji.

Inasisitizwa kuwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria ni lazima. Atakayeshindwa kuripoti atakuwa
amevunja sheria na atachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na JKT kwenye tovuti yake, wanaotakiwa kuripoti ni kama ifuatavyo:-

  1. Walimu wote wa ngazi ya cheti (GATCE) 2014 (waliohitimu mwaka 2014)
  2. Wallimu elfu tatu wa ngazi ya Diploma (DSEE) (waliohitimu mwaka 2014)
  3. Vijana wa Kidato cha Sita ambao hawajaandika barua za kuomba kuahirisha kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa hapo awali.

Majina ya vijana na vikosi valivyopangiwa yanapatikana katika tovuti ya JKT: www.jkt.go.tz

N.B Vijana wenye ulemavu unaoonekana waripoti katika kambi ya Ruvu. Mara watakaporipiti Ruvu watafanyiwa uchunguzi na jopo la Madaktari ili kubaini ulemavu wao ili waweze kupewa mafunzo kulingana na ulemavu walionao.


TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA.