Tangazo la Wizara la Mkutano na Watanzania wanaosoma Ukraine

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

TANGAZO KWA UMMA


MKUTANO KATI YA WIZARA NA WANAFUNZI WANAOSOMA MASHARIKI MWA UKRAINE HUSUSANI ENEO LA LUGANSK


Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inawatangazia wanafunzi wote wa Tanzania wanaosoma katika vyuo vya Lugansk, Ukraine na maeneo mengine Chini ya Ufadhili wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambao hivi sasa wako likizo hapa nchini kuwa kutakuwepo na mkutano kujadili, pamoja na mambo mengine, hali ya usalama na hatua za kuchukua kabla ya kurudi Lugansk kuendelea na masomo, mwezi Septembea, 2014.

Mkutano huo utafanyika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, siku ya Jumatano, tarehe 3 Septemba, 2014 saa nane mchana. Aidha, wanafunzi wengine wanaosoma Lugansk kwa udhamini binafsi wanaombwa kuhudhuria ili kushiriki katika mkutano huo.

Imetolewa na:

Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
7 Mtaa wa Magogoni,
Post Code 11479,
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM.