Uaumuzi wa Kamati ya TCRA dhidi ya Clouds Television


Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Margaret Munyagi (wa pili kulia), akiwa na wajumbe wenzake wakati wa mkutano huo. Kutoka kushoto ni Abdul Ngarawa, Joseph Mapunda, Walter Bgoya na Mkurugenzi wa Utangazaji (TCRA), Habby Gunze. (picha: jamii.com | simu namba 0712-727062)

SHAURI LA UKIUKAJI WA KANUNI ZA UTANGAZAJI NAMBA 5/2014 DHIDI YA CLOUDS TELEVISION


Tarehe 16/05/2014 na 06/06/2014 kati ya sa 3.00 na 4.00 usiku, kituo cha Clouds Television cha Dar es Salaam kilirusha kipindi cha Bibi Bomba ambacho kilikiuka Kanuni za Utangazaji (Maudhui) za mwaka 2005, Kipindi hicho katika tarehe tofauti kilitangaza shindano la kumtafuta mshindi wa bibi bora nchini ambaye angezawadiwa shilingi Milioni kumi. Maudhui ya kipindi hiki yalidhalilisha mabibi hao washiriki kutokana na maswali ya aibu waliyokuwa wakiulizwa na Waamuzi wa shindano hilo ambayo ni kinyume na Kanuni za Huduma ya Utangazaji(Maudhui),2005.

Bofya hapa kupakua na kusoma shauri hilo.