Ujasiriamali: Ajenga barabara shambani mwake na kutoza ushuru
Familia moja huko Bath nchini Uingereza inanufaika na mapato ya ushuru wa barabarani wanaoutoza kwa ajili ya kufidia gharama za barabara waliyoitengeneza katika shamba lao kwa ajili ya magari kupita baada ya ile iliyokuwa ikitumika kwa usafiri, kufungwa kwa ajili ya matengenezo.
Mike Watts anasema anataraji atarejesha gharama zote alizoingia kwa kutoza £2 kwa gari kwa kila safari.
Watts anasema wazo hilo lilitokana na kuona watu wakitumia shamba la mkulima mmoja kama njia baada ya kuwaruhusu wachache kupita bila malipo, lakini ghafla aliona ongezeko la magari yapatayo mia baada ya watu kuambizana kwenye mtandao wa Twitter.
Watts alipokutana na mkulima huyo katika mgahawa mmoja walikokuwa wakipata 'moja baridi na moja moto', ndipo wazo la ujenzi wa barabara hiyo lilipozaliwa, 'akamsomesha' mkulima wanachoweza kufanya. Wakapeana mikono na ndani ya siku 10 barabara ikawa imetengenezwa na kukamilika.
Watts anasema gharama za ujenzi wa njia hiyo ni paundi 150,000 na kwa kuwa hakuwa na fedha hizo kibindoni, 'alimsomesha' mkewe kuwa wanaweza kuzipata kwa mkopo kupitia thamani ya nyumba yao: "I said to her, 'Right, now, we haven't got 150,000 pounds, but we have got that in equity in our house, so if you want to make the gamble, you just tell me and I'll build this road just to keep you happy,' "
Watts amekaririwa akisema kuwa karibu gharama za matengenezo ya njia hizo zinarudi na huenda wakapata faida kidogo ambayo anasema wanaistahili.
Watts anafurahia mafanikio zaidi kwa kusema: "We are now on Google maps. It's wonderful."