Ujumbe wa Mch. Peter Msigwa (Mb) kwa magazeti 'yanayowandama'

Kuna magazeti ambayo kwa mda wa zaidi ya miezi mitatu ,yamekuwa yakiniandama, kuwa natumiwa na WAMAREKANI,PAMOJA NA Nyarandu ,na wakati mwingine Lembeli amejumishwa na KUITA utatu mtakakatifu. Kimsingi magazeti haya jina langu limeonekana zaidi kwenye kurasa za mbele baada ya Mimi kuionyesha DVD ya green miles .nomba watanzania tujiulize maswali haya .1.hotuba yangu ya kwanza Kama waziri kivuli ,nilikosoa kamati ya ushauri kuhusu VITALU vya uwindaji ,sambamba na kumkosoa Msekwa kuwa amekuwa mwenyekiti wa bodi ya ngorongoro ,mtendaji kinyume cha sheria... Nini nani alinitumia wakati huo?2.hutuba iliyofuata nilimtaja katibu mkuu wa Chama kikubwa kuwa meli zake zilisafirisha meno ya tembo ,sambamba na kumtaja mfanyabiashara mkubwa kuwa EIA umemtaja kuwa anahusika na ujangili.....nani alikuwa anitumia wakati huo?3.hutuba iliyofuata nilikosoa utendaji wa Nyarandu, kumleta mwandishi, kutoka uk ,ugomvi wao na katibu mkuu , na mwisho nikatoa DVD ,kutaka serikali ichukue hatua......Leo naambiwa natumiwa ,hii NAAMINI ni kwa sababu nimegusa masilahi ya WATU fulani ,
Hapo Nyuma siku wahi kuambiwa , sijasoma, nilifeli, degree yangu haieleweki,Tuchulie Mimi, sijasoma, nilifeli, natumiwa ,kuna utatu mtakatifu , JE hii inaondoa UHALISIA kwamba GREEN MILES wamevunja SHERIA ZA UWINDAJI?
Kwa kuwa Mimi sikusoma,kwa hiyo kukiuka sheria za uwindaji ni HALALI,Kutokusoma kwangu , utatu matakatifu , kutumiwa ,kunafutaje makosa, kumi na moja ambayo, green miles wanashindwa kujibu Toka nimeongea na vyombo vya habari. Kama Mimi nimehongwa Kama gazeti la Fahamu na Jamhuri linavyodai, kunaondoaje makosa ya green miles. Kama wanaamini kuwa nimehongwa ni Vema wakatoa ushahidi wa makosa yangu ili vyombo husika vikachukua hatua, dhidi yangu,Kama Mimi nilivyoweka makosa ya green miles hadharani . na hiyo itakuwa kesi nyingine amabayo hata hivyo haiondoi makosa ya Green miles. Nawasihi wananchi masikose kuona DVD Leo ITV SAA 3:30 ili mjue kwa nini green miles na wapambe wao magazeti ya Fahamu na jamhuri wanavyoshindwa kujibu hoja,
 — with Waziri Martine Kindole.