Viongozi wapya wa CHADEMA Kigoma

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Kigoma kimepata viongozi wapya wa muda katika ngazi ya Mkoa na Wilaya katika uchaguzi uliyofanyika jana kama ifuatayo:-
  1. Ally Kisala ambaye ni Diwani wa Mwandiga, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Mkoa wa Kigoma
  2. Katibu Mkuu ni Shabaan Madede 
  3. Mratibu wa Baraza la Wanawake Mkoa (BAWACHA) ni Vestina James Luhihi 
  4. Omary Gindi ni Mratibu wa Baraza la Vijana (BAVICHA)
  5. Jeremia Misigaro ni Mratibu wa Baraza la Wazee.
Viongozi wa Jimbo 
  1. Mwenyekiti ni Khalfani Bona
  2. Katibu ni Frank Luhasha
  3. Katibu Mwenezi ni Idd Ngesha
  4. Mratibu wa Baraza la Wazee ni Yassin Mapigosaba 
  5. Mratibu BAVICHA ni Amfua Athumani
Mkurugenzi Mkuu wa Oganaizesheni na Usimamizi CHADEMA Taifa, Benson Kigaila, ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu katika uchaguzi huo, alisema chama kimefanya uchaguzi huo kutokana na mapengo yaliyoachwa wazi na viongozi waliyohama hivi karibuni, na watashika madaraka hayo hadi uchaguzi utakapofanyika tena kwa mujibu wa katiba Agosti 30 mwaka huu.