Wakulima almanusra wamtandike Naibu Waziri

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi amenusurika kupata kipigo kutoka kwa wakulima wa zao la pamba katika kijiji cha Marekano wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu kwa madai ya kutoridhishwa na majibu aliyoyatoa juu ya mbegu za pamba zisizo na manyoya (za Quton) kutoota katika musimu uliopita wa kilimo.

Tukio hilo limetokea kijijini hapo wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kushitukiza ya kutembelea vituo vinavyonunua zao hilo katika wilaya hiyo ili kukagua mizani zinayotumika kupimia zao hilo kutoka kwa wakulima.

Wakati akitoa majibu kwa wakulima ambao walikusanyika ghafla wakati akikagua mizani hiyo katika moja ya kituo kilichopo kijijini hapo ambao walihoji ni kwa nini serikali iliwalazimisha kununua mbegu hizo ambazo hazikuota pamoja bei ya kununulia zao hilo.

Taarifa ya Samweli Mwanga-Simiyu via Malunde1 blog