Idara ya uhamiaji Jijini Dar es Salaam imewakamata raia 12 wa kigeni waliokuja nchi kinyume na sheria wakiwemo wanajeshi wanne wa Jeshi la Nepal na 8 kutoka nchini India walioletwa nchini kinyume na sheria kwa kile walichosema ni maisha magumu nchini kwao.
Raia hao wamekamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya ESCOT iliyoko huko Kijitonyama jijini Dar es Salaam katika operesheni maalum iliyoendeshwa na Idara ya Uhamiaji Jijini baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo juu ya uwepo wa watu hao ambao waliwatilia mashaka.
Afisa uhamiaji wa jiji la Dar es salaam Grace Hokororo akizungumza kuhusu suala hilo |
Miongoni mwa wanajeshi hao wa Nepal, yumo komando mmoja wa jeshi hilo ambyeo amedai kuletwa nchini kwa ajili ya kutafutiwa ajira ya masuala ya ulinzi katika nchi za Afrika na hivyo walishukia Tanzania kama kituo kwa ajili ya kufanikisha malengo yao.
Afisa wa Uhamiaji wa jiji la Dar es Salaam, Grace Hokororo amesema kuwa wahamiaji hao wamekuwa wakipita katika nchi ya Tanzania na kupelekea nchi nyingine kama Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyishwa kazi zisizo halali.
. |
. |
Aidha Bi Gace amewataka Watanzania kuwafuchia watu wanaowaficha watu kama hao kwani ni kinyume na sheria na baadaye huleta madhara makubwa kama vile ya uhalifu na uuzwaji wa dawa za kulevya.