Ajali katika milima ya Sekenke


Dereva wa lori lililokuwa limebeba saruji kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Mwanza leo amefariki dunia baada ya lori hilo kupinduka eneo la Sekenke mkoani Singida. Watu wengine wanne waliokuwa kwenye lori hilo wamejeruhiwa.

Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kufeli breki kwa lori hilo lililokuwa likishuka milima ya Sekenke na mpaka anaondoka eneo la ajali hiyo bado dereva (marehemu) na mmoja wa watu waliokuwemo aliyekuwa hai walikuwa bado wamenasa kwenye lori hilo.