IGP Ernest Mangu amekaririwa akisema kuwa Jeshi la Polisi limetangaza zawadi ya shilingi millioni kumi kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wahalifu na silaha zilizoibwa.
Dkt Rutatinsibwa amekaririwa akisema kuwa hali za majeruhi ni mbaya na wamehamishiwa katika hospitali ya rufaa Bugando.
--------
Ripoti kupitia Malunde1 blog zinasema kuwa kituo cha polisi kilichopo Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita kimevamiwa na majambazi usiku wa saa tisa kuamkia leo.
Katika tukio hilo, askari wawili kati ya wanne waliokuwa zamu, wameuawa huku waliobakia wakiachwa wamejeruhiwa.
Wahalifu walilipua chumba cha kuwekea silaha na kuondoka na bunduki zaidi ya tano aina ya SMG na mabomu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Geita, Joseph Konyo yupo katika eneo la tukio.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Dkt Honorata Rutatinisibwa amekiri kupokea miili ya askari wawili (wa kike na kiume).