Kuhusu kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu wa SMZ

Mkutano kati ya waandishi wa habari wa Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Othman Masoud Othman, uliokuwa ufanyike leo Mjini Unguja ili kupata kweli kuhusu kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu huyo katika Kamati a Uandishi wa Katiba ya Bunge Maalum la Katiba umeshindwa kufanyika.

Habari kutoka Mjini Unguja, zinasema waandishi wa habari ambao walikusanyika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu huyo, walielezwa kwamba Othman hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa kuwa alikuwa na kikao kingine cha ndani na kuruhusu vyombo vya habari vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pekee kuzungumza naye.

Hivi karibuni, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa Mwanasheria Mkuu huyo alijiuzulu katika Kamati ya Bunge.