Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa akisalimiana na mdogo wa marehemu Betty Ndejembi, Aisha Ndejembi aliyeuawa wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mzee Pancras Ndejembi na Mama Ndejembi ambao marehemu alikuwa mjukuu wao.
Mheshimiwa Lowassa alikwenda nyumbani kwa mwanasiasa huyo mkongwe eneo la Uzunguni mjini Dodoma kumpa pole ya kufiwa na mjukuu wake huyo.
Mzee Ndejembi akimuelezea Mhe. Lowassa mkasa mzima wa kifo cha mjukuu wake, Betty Ndejembi aliyeteswa na kuuawa na watu wasiyojulikana jijini Dar es Salaam.