Mapokezi ya binti Mwanaafa Mwinzago kwao MtwaraMara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara, mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago akitoa maneno ya shukrani kwa wakazi wa Mtwara waliojitokeza kuja kumpokea uwanja wa Ndege wa Mtwara mapema leo. Vilevile alitoa shukrani zake zote kwa Watanzania wote kwa kuweza umpigia kura na kumfanya aibuke mshindi wa milioni 50/= za Tanzania katika fainali ya Shindano la Kusaka vipaji vya Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT).Wapenzi, Mashabiki na wana Mtwara wakiwa Nje ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara wakisubiri kumpokea mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago kwaajili ya kumpongeza kwa kuibuka mshindi wa shilingi milioni 50 za Kitanzania katika fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) lililofanyika mwisho wa Mwezi wa Nane katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.Wakazi wa mkoa wa Mtwara wakimpongeza Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago ambaye amewasili mkoani Mtwara ambapo ndio nyumbani kwao akitokea Dar es Salaam mara baada ya kuibuka mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 50 za Kitanzania.

Ndugu, jamaa na marafiki wa mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara akitokea Dar es Salaam.Shangwe na nderemo zilitawala katika viunga vya Uwanja wa Ndege wa Mtwara kabla na baada ya mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014, Mwanaafa Mwinzago kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara akitokea Dar es Salaam ambapo fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) lilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City.Msafara wa kuelekea nyumbani Kwa MShindi wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago ukitoka katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara.Msafara ukielekea myumbani kwa mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago,Wazee kwa Vijana wakimpongeza Mwanaafa Mwinzago wakati alipokuwa akipelekwa nyumbani kwao kwa msafara wakati akitokea Uwanja wa NdegeVijana nao wakimpongeza Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago

Wakazi wa Mtwara wakimpongeza Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakati alipokuwa akipita na masafara uliompokea uwanja wa Ndege wa Mtwara na kumsindikiza hadi nyumbani kwao Magomeni Mkoani Mtwara mapema leo asubuhi

Wanafunzi wa Shule ya Msingi wakimpongeza Mwanaafa Mwinzago wakati alipokuwa akipita na msafara kutoka Uwanja wa Ndege wa Mtwara akielekea nyumbani kwa ajili ya kujiandaa kwenda Shule leo asubuhi wakati alipowasili kutokea Mkoani Dar es Salaam.

Majirani, ndugu, marafiki na wakazi wa Mtwara wakimshangilia mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakati alipowasili nyumbani kwao eneo la Magomeni, Manispaa ya Mtwara Mikindani akitokea Uwanja wa Ndege wa Mtwara.

Picha zote: Josephat Lukaza/Lukaza Blog