Marekani yathibitisha kuwa imemuua kiongozi wa al-Shabab

Mashabulizi yaliyofanywa na majeshi ya Marekani wiki hii nchini Somalia, yamemwuua kiongozi wa kundi la al-Shabab, Ahmed Abdi Godane.

Msemaji wa Pentagon, Rear Admiral wa kikosi cha Maji, John Kirby alisema katika taarifa yake fupi kwa maandishi baada ya kuthibitisha kwa siku nne pasina shaka kuwa Godane ameaga dunia:
"We have confirmed that Ahmed Godane, the co-founder of al-Shabaab, has been killed. The U.S. military undertook operations against Godane on Sept. 1, which led to his death. Removing Godane from the battlefield is a major symbolic and operational loss to al-Shabaab. The United States works in coordination with its friends, allies and partners to counter the regional and global threats posed by violent extremist organizations."
Hata hivyo, kundi la al-Shabab halijatamka hadharani kuwa Godane amefariki.

Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud amekaririwa akisema kuwa mashambulizi hayo yalifanyika akiwa na taarifa na kukubaliana na uamuzi huo na kuunga mkono jitihada za washirika wake wanaosaidia kupambana na al-Shaban.

Rais wa Marekani, Barack Obama akizungumza katika hitimisho la mkutano na NATO huko Newport, Wales aliwaambia wanahabari kuwa wanachofanya dhidi ya al-Shabab bila shaka yoyote inaonesha walivyodhamiria kupambana situ na kundi hilo, bali pia na lile la ISIS/ISIL.