Mbunge Selasini atoa fedha na vifaa kwa michezo JimboniMbunge wa Jimbo la Rombo (CHADEMA) Joseph Selasini ametoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi 500,000 na fedha ya kusaidia kambi ya Mabingwa wa Ligi ya Wilaya hiyo Border Shooting FC 2013/2014 wanaoshiriki ligi ya mkoa wa Kilimanjaro.Akikabidhi msaada huo Mbunge Selasini alisema mchezo wa soka katika wilaya yake umekuwa ukizorota na kuona kwamba vipaji vinapotea na kutengeneza taifa la vijana wasio na mwelekeo.

“Soka ni mchezo unaopendwa, lakini tusipotia juhudi za makusudi kuuendeleza tutabakia kuangalia ya wenzetu wanaofanya vizuri kitu ambacho ni kibaya wakati vipaji tunavyo,” alisema Selasini.Selasini amesema itakuwa ni heshima kwake na kwa Watanzania kuona Rombo ikifanya vyema katika medani ya soka katika siku za usoni hali ambayo itaibua vipaji vya soka.

Holili/Rombo, Kilimanjaro