Mmoja wa wanaohisiwa kuvamia na kuua polisi Geita akamatwa juu ya mti na bomu

Silaha ziliroporwa kituo cha olisi Ushirombo, wilaya ya Bukombe na kukamatwa leo

Habari kutoka Geita zinasema kuwa, msako uliofanywa jana na jeshi la polisi mkoani Geita huko Ushirombo umefanikisha kumkamata mtu mmoja (waliyekuwa wakimhisi kuwa ni jambazi) akiwa ameketi mtini huku ameshikilia bomu.

Msako huo pia umepata mabomu 3 na bunduki 7 aina ya SMG vikiwa vimewekwa kwenye tanuru la kuchomea matofali.

Jeshi hilo pia imemkamata pia mwalimu mmoja katika shule ya sekondari Ushirombo na watu wengine watatu wanaohitsiwa kushiriki katika tukio la jana.