Msafara wa Makamu I wa Rais wa Zanzibar wapata ajali Mwanza

UPDATE/TAARIFA MPYA imeongezwa

.
Inaripotiwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Kambaya akizungumza kwa njia ya simu kutoka Mkoani Mwanza amesema Maalim Seif hajadhurika katika ajali hiyo ambayo ilitokea wakati wakielekea katika eneo ilikotokea ajali ya mabasi mawili na gari dogo jana huko Musoma na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30:
“Ni kweli msafara wa Makamu wa Rais na Katibu Mkuu Taifa umepata ajali ila yeye yuko salama, lakini viongozi wetu wa chama akiwemo katibu wa Chama cha Wananchi CUF Wilaya ya Nyamagana Bi Rehema Mwenda Pamoja na Mkuu wa Kitengo cha cha Habari wa chama Chetu wilaya ya Nyamagana, Hassan Shido ndiyo wamepata majeraha kutokana na ajali hiyo.”
Kambaya ameongeza kusema kuwa ajali imetokana na dereva wa gari aina Scania kwenda
kuligonga gari la nne lilokuwa limewabeba viongozi hao kutoka gari lililombeba Maalim Seif kwenye msafara huo.


Moja ya gari ambalo lilikuwa kwenye msafara wa baada ya kupata ajali, Misungiwi, Mwanza.


Hili ni gari jingine ambalo lenye usajili namba T397ANU nalo lilihusika katika ajali hiyo.
.
Kupitia blogu ya Pamoja Pure, habari zinasema msafara wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad umepata ajali ukihusisha magari mawili kati ya yalipogongana na lori lenye tela.

Mkuu wa kitengo cha habari Wilaya, Shido ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Utemini Kata ya
Mirongo amejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando.Katibu wa CUF Wilaya ya Nyamagana, Rehema Mwenda amejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando (kulia) na muonekano wa gari (kushoto) baada ya ajali katika wilaya ya Misungwi, jijini Mwanza.