Safu ya uongozi mpya CHADEMA Geita

Katika uchaguzi uliyofanyika mwishoni mwa wiki, kwenye ukumbi wa Alpha Hotel ukijumuisha majimbo yote ya mkoani Geita ambayo ni Geita, Busanda, Nyang’hwale, Bukombe, Chato na Mbogwe, CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Geita kimewachagua viongozi wake kama ifuatavyo:-
  • Alphonce Mawazo - Mwenyekiti (alipata kura 34 dhidi ya 14 za mpinzani wake wa karibu, Daudi Ntinonu)
  • Sudi Kanyagara - Katibu (alipata kura 35 za ndiyo na 13 hapana.)

BAVICHA
  1. Mwenyekiti - Neema Chozaire, 
  2. Katibu - Frederek Baya

BAWACHA
  1. Mwenyekiti - Husna Said 
  2. Katibu - Eva Shadrac
Baraza la wazee
  • Katibu ni Amosi Nyanda 
  • Mweka Hazina ni Kayaga Kayaga

Matokeo hayo yalitangazwa na Mwenyekiti wa uchaguzi ambaye pia ni Ofisa kutoka Kanda ya Ziwa Magharibi, Tungaraza Njugu.

Naye Mawazo ambaye alishawahi kuwa diwani wa Kata ya Sombetini jijini Arusha na Naibu Meya kwa chama cha CCM kabla ya kujitoa na kurudi CHADEMA 2012, alisema atashirikiana na kila mtu ndani ya chama na kumuomba Ntinonu ambaye alimwita ‘kaka’, ushauri na maelekezo kwa ajili ya ujenzi wa chama.