Tarehe kamili ya mwisho wa BMK ni kizungumkuti!

Wakati tamko la Serikali linaonesha kuwa Bunge Maalumu la Katiba linatakiwa kumalizika Oktoba 4, 2014, kalenda ya Bunge hilo ambayo wamegawiwa wajumbe inaonesha kuwa Bunge hilo litamalizika mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Kutokana na kutofautiana huko, Kamati ya Uongozi imelazimika kuiagiza Sekretarieti ya Bunge hilo kufuatilia serikalini kujua sababu ya kuwepo kwa tofauti hizo.