Ujumbe wa LadyJayDee kuhusiana na habari za magazeti ya udaku

Zamani ilikuwa haipo sehemu ya kujitetea, gazeti likishaandika ndio limeandika.
Lakini sasa ulimwengu umebadilika, sio muda wa watu wote kulishwa chakula kisichofaa.Kwanza hicho kichwa cha habari kimenivunjia heshma sana

Nafikiri lengo ni kuilazimisha jamii inayomuelewa JayDee tofauti imuone kuwa ni mtu asiefaa, sawa.

Dogo anaswa na mkoko? Huo mkoko mmemnasa nao wapi wakati hizo picha ni mimi nilizi post mwezi February Instagram?????

Picha ambazo zilipigwa Nyumbani lounge tena kutumia simu ya Gardner.

Jide, dogodogo gumzo mjini

Gumzo ni kitu kinachoongelewa sana na kilichoenea kila kona ,,,,,sasa hii habari ni gumzo wapi ambapo haisikiki, ......

Mngeandika tumeamua kumuanzishia Jide gumzo hili, ndio ningewaelewa.

Vitu vya kuzua.Ni watu wengi tu wakija band wakipata nafasi wanaomba kupiga picha na mimi na wengine pia wanaomba kupiga picha na gari sababu wanaipenda.

Kama mtu yoyote anavyoweza kupiga picha na sanamu la kitu chochote anachokipenda.

Hivi je! Wimbo wa JayDee mgumba, JayDee tasa umechuja? Umeisha chati?? Nashangaa na
najiuliza tu

Inawezekana wimbo huo umechuja ndio maana mnatafuta wimbo mwingine utakao hit zaidi ya ule

Ndio kinachopelekea kuandika story za namna hii

Sio nyinyi mliokuja kuomba radhi kwa yote mliowahi kuniandika na kudai kuwa mmejirekebisha, miezi kadhaa tu iliopita?

Sio boss wenu aliemfuata Gardner na kumwambia tumalize tofauti zetu?

Kama hizo tofauti zilikuwepo ๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž

Inawezekana nyie ndio mna tofauti na mimi, sijawahi kuwa na tofauti na mtu hata nisiemfahamu. ..

Nashukuru Mungu nilikataa msamaha wenu ni kama nilihisi hamkumaanisha

Au sababu sijawahi kukubali show mlizotaka kufanya na mimi?

Je! Hiki ni kisasi? Sielewi

Mungu alienisimamia ataendelea


Hii sio vita ya kwanza wala ya mwisho

Dunia ni mapambano.

Kama nia ni kufanya niishi maisha ya uoga, kudhoofika na msongo wa mawazo mmefeli ,,,,, wengine mkijidai ni wacha Mungu huku mkiumiza nafsi za watoto wa binadamu wenzenu.

No wonder mnaishi bila amani mbali na utajiri mlionao kwa kuogopa visasi.

Sikuzaliwa kukata tamaa

Pia wapo wanaopenda kuandikwa kwenye hayo magazeti yenu

Wafanyieni favor ya kuwapa hiyo nafasi mi sifanyi muziki wa magazeti ya udaku

Mkiachana na mimi nitashukuru sana

Hata ndoa yangu ikivunjika haimaanishi mnitafutie story za kunichafua

Ndoa ya Madiba ilivunjika sembuse yangu nina utofauti ipi na binadamu wengine?

Nyie ndoa zenu ziko perfect si ndio?

Hewala watakatifu nyie, mnaoficha yenu na kutangaza ya wenzenu.

Mwisho nawaomba watu mnaonielewa kutoamini tu habari yoyote ambayo haijatoka kwangu wala kwa muwakilishi wangu ambae ni "Webiro Wakazi Wasira".

Kama kuna chochote cha watu kujua nitakiongea mimi kwa mdomo wangu sio kuwekewa maneno mdomoni.

Kila siku ooooh tulimpigia simu hapatikani, namba yangu yenyewe kwanza hata mnaijua???

Mngekuwa mnaijua msingekuwa mnahangaika mnawapigia watu wangu wa karibu kunitafuta , na hao watu hawawezi kunisaliti ndio sababu mpaka miaka 70 mtaishia kusema tulimpigia simu JayDee hapatikani.

Nyie muongee chochote mnachojiskia

Ila sie hatuna haki kujitetea ??

Hili nalo litapita kama mengine

Na inshallah nitakuwa hapa hapa nimesimama nawaangalia


Picha moja wapo ni hiyo ambapo mtoto wa vitoto alikuja siku hiyo hiyo na akapiga picha na Gardner, mbele ya gari hiyo hiyo mnayodanganya watu kuwa mmemkuta nayo na mahala ni hapo hapo Nyumbani Lounge, ,,,,, na picha nyingine ni hizo nilizowahi kuzi post mimi mwenyewe mwezi february leo zinanihukumu endeleeni kudanganya jamii

Na hizo ni chat alizoniandikia huyo mtoto wa vitoto ambae ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona na sijawahi kumuona tena. . Zaidi ya kuongea nae twitter ,,, sisemi kama mimi malaika lakini

Ukweli huwa hauchanganywi na uongo

Kwa hili mmenidhalilisha sana

Kama nia yenu jamii inione mwanamke nisiefaa na ninaependa dogodogo

Basi Mungu atawaonyesha ukuu wake

---
via ukurasa wake wa facebook.com