Utafiti wa UNICEF unaopingana na maandiko ya Mungu
Nimesoma utafiti wa UNICEF (United Nations Children's Fund) au Mfuko wa Kimataifa wa Watoto ambalo ni shirika la Umoja wa Mataifa kwa shabaha ya kuwasaidia watoto duniani, limekuja na utafiti ulioniacha nitafakari mengi kuhusu wanangu Fariss na Fridausi. Na wewe pia kama u-mzazi tafakari kuhusu utafiti huo kisha vuta subra na hekima, durusu maandiko kwenye vitabu vitukufu.
Nianze na sehemu ya utafiti huo kabla sijagusa mafundisho ya dini na muono wa mitume kwenye dini ambazo wengi wetu tu waumini, hapa naangazia Uislamu na Ukristo ambazo ni dini kuu mbili zenye waumini
wengi hapa nchini.
Sehemu ya utafiti huo inasema “…six (6) in ten (10) children ages two to 14 are regularly beaten by parents and caregivers..” yaani watoto sita kati ya kumi wenye umri kati ya miaka 2 hadi 14 hupigwa mara kwa
mara na walezi wao na wazazi wao. Yaani watoto wa umri huo (miaka 2 hadi 14) wamekuwa wanakula mkong’oto kutoka kwa walezi (Walimu/wadada/wakaka wa kazi nk) wazazi wanapokuwa hawapo nao
lakini wakati huo wazazi nao wamekuwa wanatoa mkong’oto kwa watoto wao wanapo pindi wanapo pituka mipaka.
Utafiti huo ukaendelea “…Most violence against children occurs at the hands of the people charged with their care or with whom they interact daily - caregivers, peers and intimate partners," yaani, mkong’oto au
vipigo hivyo vinatokea mikononi mwa watu waliopewa jukumu la kuwalea, wanao kutana nao kila siku, walezi na marafiki wa karibu wa rika moja.
Wakati naendelea kuusoma utafiti huo nikakutana na maneno haya yaliyo niumiza “..the most severe forms of corporal punishment - hitting a child on the head, ears or face or hitting a child hard and repeatedly
…". Adhabu zilizo kubuhu ni kupiga kichwani, masikioni au usoni kwa nguvu na kurejelea.
Unaweza kujisomea zaidi utafiti huo hapa :
smh.com.au/world/one-in-10-girls-worldwide-are-sexually-abused-unicef-says-20140905-10cxn6.html
Baada ya kusoma utafiti huo nikajikuta narudi kuangalia muktadha wa maandiko ya imani za dini, na hapa naanza na Biblia.
Mithali 22:15, Agano la kale, nimekutana na maneno haya: "Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto, lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali." Maneno haya maana yake ni kwamba, asiyemchapa mwanae anamfanya awe mjianga, kwa vile hatma ya kutomchapa ni kubaki na ujinga wake.
Maandiko mengine ya Biblia pia katika kitabu cha Mithali 23:13 yanasema "Usimnyime mtoto wako mapigo,maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa…" Katika kitabu hicho hicho cha Mithali (23:14) pia nikasoma
maandiko haya "…utampiga mtoto kwa fimbo na kumuokoa nafsi yake na kuzimu." Baaada ya kusoma nikagundua kuwa, kumbe fimbo humponya mtoto na kumuokoa nafsi yake na kuzimu?! Maandiko kwenye biblia yanasisitiza umuhimu wa adhabu ya fimbo kwa mtoto.Yaani kwa mujibu wa maandiko hayo
fimbo kwa mtoto ni lazima, na ni dawa iponyayo. Hapa nikakumbuka tena ile methali, “..asiye funzwa na mamae hufunzwa na ulimwengu, na amleaye mwanaye kama yai hula hasara..”
Watoto wameelezwa katika Qur’ani kuwa ni bi-shara njema. Pia ni kiburudisho cha macho yetu. Amesema Mwenyezi Mungu:
وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا
وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ{74}
“Ewe Mola wetu, tupe katika wake zetu na watoto wetu watakaoyaburudisha macho yetu….”(25:74).
Na watoto ni pambo la maisha katika ulimwengu huu: “Mali na watoto ni pambo la maisha ya duniani….” (18:16). Aya hizi zinaonyesha namna mtoto anavyopewa thamani, na najua mnajuna kuwa kawaida ya kitu chenye thamani hutunzwa vizuri, na kulindwa, na hakibugudhiwi wala kufujwa
thamani yake.
Mtume (s.a.w.) anatudhihirishia ya kuwa ulimwengu wa utoto ni kama pepo, pale aliposema: “Watoto ni vipepeo vya Peponi.” Kuwatunza watoto ni jambo la lazima, na kuwapenda humleta mtu karibu na Mwenyezi Mungu. Maana yake ni nini, ukimpenda mwanao/mtoto unakuwa karibu na mwenyezi Mungu na ukimchukia unakuwa mbali na mwenyezi Mungu, na kimantiki awaye mbali na mwenyezi huwa yuko karibu na shetani au ibilisi.
Mtume (s.a.w.) amesema: “Lau kama si watoto wanyonyeshwao, na wazee wanaorukuu (kwa kuswali) na wanyama wal- ishwao mashambani, basi mngelipatwa na adhabu kali.”, Kumbe sisi wazazi tunaepushiwa adhabu kwa kuwajili watoto kwa kuwanyonyesha tu watoto! Kumbuka neno kunyonyesha lina maana pana, lina maanisha kushibisha, yaani kumpa mtoto vyakula vifaavyo ili ashibe
Inaonyesha wazi kwamba huruma na uangalifu wa Mwenyezi Mungu kwa watoto ndiyo uliofanya Mwenyezi Mungu kuzuia adhabu juu ya watu wake. Lakini mtume huyo akatufundisha kuwa “…Ukiona baya linatendeka unalikemea na likirejea, au kukinai unaliondosha kwa mkono wako. Hapa kwenye kuliondosha baya kwa mkono inaweza kuwa kwa kipigo kama si kuadhibu kwa mkono.
Sheria ya Kiislamu imewaamuru wazazi kuwa na dhamana kwa maisha ya mtoto na makuzi yake. Kwa msingi wa kwamba, mtoto huchukuliwa kuwa ni dhamana waliyopewa, ambayo inapaswa kutunzwa nao kwani watakujaeleza mbele ya Mwenyezi Mungu (jinsi walivyoitunza amana waliyopewa). Moja ya hadithi za mtume SAW inasema “….Kila mmoja wenu ni mchungaji na kila mmoja ataulizwa juu ya kile akichungacho…”
Kwa maana hiyo, Ukimuacha mwanao bila kumchunga anaweza kudondokea kwenye maangamivu, akidondokea kwenye mzazi ana angamia naye maana “..Mchunga janga hula na wakwao, kwenye Quran tukufu inasema “…Wala msijitie wenyewe katika maangamivu ….” (2:195). Maana yake ni kwamba
kuiacha jamii yako ipotee ni kujiingiza kwenye maangamivu.
Mtoto akipotoka, onya, kemea, finya kidogo, au chapa! Rudisha yeye kwenye mstari mnyofu asilete upumbavu. Tena asikushinde!
#Pichani nimekachapa Firdaus kalikuwa kanalilia kutia mkono kwenye soketi ya umeme. Pumbavuuu..
"..Wala msijitie wenyewe katika maangamivu ….” (2:195)
---
Imeandikwa na Mohamedi.Mtoi