Watu wa Ontario, Canada watembelea Jumuiya ya Wagonjwa wa Hemophilia

Dave Neal akiwafundisha vijana jinsi ya kujidunda wenyewe

Mtaalamu kutoka Hemophilia Ontario, Canada Bw. Dave Neal akiwafundisha vijana wenye tatizo la kutoganda damu au Hemophilia jinsi ya kujidunda sindano bila ya msaada wa daktari au muuguzi.

Mafunzo hayo yalifanyika katika washa iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Hemophilia Tanzania kikishirikiana na Chama cha Hemophilia Ontario cha Canada tarehe 15/11/2014 na kufanyika katika ukumbi wa Salender Bridge Club, Dar es salaam.

Hemophilia ni ugonjwa unaowapata watoto wa kiume zaidi na mgonjwa hulazimika kuishi nao maisha yote. Ugonjwa husababisha uvimbe katika maungio ya mwili, ulemavu, maumivu makali, damu kuvuja bila ukomo pale mshipa unapokatika/ pasuka na mara nyingine upotevu wa maisha.

Kwa upande wa wanawake ugonjwa huu hujulikana kama Von Willebrand Disease (VWD). Vilevile unaondoa uwezo wa damu kuganda na hivyo damu kuvuja kwa muda mrefu au bila ukomo.

Maelezo zaidi tembelea; World Federation of Hemophilia - Home (www.wfh.org)

Picha ya mkutano wa wadau


  • Shukurani mdau R. M. kwa kutushirikisha taarifa hii.