UKAWA watiliana saini makubaliano ya Uchaguzi Serikali za Mitaa

Kutoka kushoto: Katibu Mkuu CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, wakisaini makubaliano hayo ya UKAWA.

Sehemu yamakubaliano ya UKAWA yaliyotiwa saini

Viongozi wa UKAWA wakionesha hati ya makubaliano aada ya kutia saini Jumanne, Novemba 4, 2014 kwenye ofisi za Makao Makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam.
Makubaliano ya UKAWA yamevihusisha vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, yataanza kutekelezwa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu ambapo UKAWA utasimamisha mgombea anayekubalika katika eneo husika bila ya kujali chama.