Picha, Magazeti kuhusu ?Kutekwa ?Kukamatwa Mbunge wa CHADEMA

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara CHADEMA, Mhe. Rose Kamili (nyuma ya askari wa kike) akiwa chini ya ulinzi jioni ya Jumamoasi ya Machi 15, 2013 kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota, Iringa Vijijini baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kuigawa fedha kwa wanakijiji, siku moja kabla ya uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara CHADEMA, Mhe. Rose Kamili (nyuma ya askari wa kike) akiwa chini ya ulinzi jioni ya Jumamoasi ya Machi 15, 2013 kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota, Iringa Vijijini baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kuigawa fedha kwa wanakijiji, siku moja kabla ya uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini.

Taarifa kwa wahitimu Kidato cha Sita 2014 ya kujiunga na Jeshi la Polisi

KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI KWA WAHITIMU WATARAJIWA WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014


Katika mwaka wa fedha 2014/2015 Jeshi la Polisi linatarajia kuajiri wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014 na kidato cha nne mwaka 2013.

Ili kutekeleza azma hii tumeweka fomu kwenye tovuti ambayo wahitimu watarajiwa wa kidato cha sita wa mwaka 2014 watajaza kabla ya kufanya mitihani yao ya kumaliza kidato cha sita.

Baada ya kujazwa kikamilifu wakabidhi fomu kwa wakuu wa shule ambao watazirejeshe kwa

Taarifa ya matokeo ya awali ya uchaguzi mdogo wa Ubunge Kalenga

UPDATES/TAARIFA MPYA:

  1. CCM kura 22,908 (asilimia asilimia 79.4)
  2. CHADEMA kura 5,800 (asilimia 20.1)
  3. CHAUSTA kura 143 (asilimia 0.5)

Washabiki wa CCM wakimbeba aliyekuwa mgombea wa CCM jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini Godfrey Mgimwa, baada ya kupata matokeo ya awali ya CCM kuongoza kata 11 kati ya 13 katika matokeo ya uchaguzi uliofanyika leo. Shamrashamra hizo zilifanyika Ofisi ya CCM mkoa wa Iringa.

Taarifa kutoka kwa Bashir Nkoromo — Takwimu za matokeo ya awali yasiyo rasmi yanaonesha ifuatavyo:-

Taarifa ya Kamati ya PAC baada ya kukutana na BoT leo

Kamati ya PAC Leo imekutana na Benki Kuu ya Tanzania kupokea Maelezo kuhusu fedha Tshs 201 bilioni za akaunti ya Tegeta Escrow. Fedha hizi zinahusiana na mkataba IPTL. PAC ina wasiwasi kwamba TANESCO, kwa mujibu wa nyaraka, itatakiwa kulipa fedha nyingi zaidi zinazofikia zaidi ya Tshs 200 bilioni kwa kampuni iliyonunua IPTL.

Kamati imeamua kwamba:-
  1. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanya ukaguzi maalumu wa suala zima IPTL na uhalali wa utoaji wa fedha kutoka akaunti maalumu ya tegeta escrow.
  2. TAKUKURU waanze uchunguzi wa mchakato mzima wa mkataba wa IPTL, umiliki wa kampuni hiyo na uhamishaji wa umiliki kwenda kampuni ya PAP.
Kamati imeshangazwa na kitendo cha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kuanzisha

[audio] Fr. Evod Shao azungumzia mwaka mmoja wa Papa Francis


Na Mubelwa Bandio, JamiiProduction  — Wiki hii, kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, alitimiza mwaka mmoja tangu achaguliwe kutwaa nafasi hiyo.

Kwa miezi yote 12 iliyopita, Papa Francis amekuwa mmoja wa watu waliofuatiliwa zaidi duniani na kuaminika kuwa mmoja wa watu waliokuwa na ushawishi mkubwa kwa mwaka wa 2013.

Papa alitawala habari kwa kuonyesha nia ya kulifanya kanisa kuondokana na dhana ya utajiri na hata

Barua ya wazi kwa Watanzania wote: Yuko Tembo Sebuleni

© 2014 na Mlenge Fanuel.

Yuko tembo sebuleni, na kaya inaendelea na gumzo, gumzo ambalo tembo siyomada inayozungumzwa. Madhali kaya inaendelea na gumzo, na katu haimtaji tembo, kaya ile inaamini uwepo wa tembo haubadili lolote kwa vile tu kaya haimjadili. Hivi ndivyo namna Tanzania ilivyojikita kuhangaikia katiba mpya ilhali mchakato wa EAC unashika kasi. Angalia Kielelezo 1.

Kielelezo 1: Yuko tembo sebuleni, na kaya inaendelea na gumzo, ambalo tembo siyo mada inayozungumzwa.
Kielelezo 1: Yuko tembo sebuleni, na kaya inaendelea na gumzo, ambalo tembo siyo mada inayozungumzwa.

Kielelezo 1: Yuko tembo sebuleni, na kaya inaendelea na gumzo, ambalo tembo siyo mada inayozungumzwa.

“Si kweli!”

“Haiwezekani!”

“Hatutakubali!”

Ni miongoni mwa vile raia wengi wa Tanzania husema wanapoeleweshwa maana ya EAC: kwamba, EAC ya sasa ni ya kuunda taifa lingine ambamo Tanzania haitakuwa tena ni taifa dola huru.

Nami pia nilisema vivyo hivyo nilipobaini nini hasa maana ya EAC ya sasa hivi. Ni kawaida kwa akili ya

Taarifa ya TAMISEMI: Maagizo ya ajira mpya na Majina ya Walimu wapya kwa shule za Msingi, Sekondari, Vyuo

OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (OWM - TAMISEMI)

AJIRA MPYA YA WALIMU WAPYA KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2013/14.


A: OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI INATANGAZA ORODHA YA WANACHUO WAHITIMU WA MAFUNZO YA UALIMU KAMA IFUATAVYO:-

i. Walimuwa Cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 17,928
ii. Walimu wa Stashahada kwa ajili ya shule za sekondari 5,416
iii. Walimu wa Shahada kwa ajili ya shule za sekondari 12,677

Walimu hawa wamepangwa katika Halmashauri na shule za mazoezi za vyuo vya ualimu Tanzania Bara.

B: Kila Mwalimu (ajira mpya) atatakiwa kuzingatia yafuatayo:-

Bunge la Katiba lapongezwa kwa kuonesha usawa katika jinsia

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Lilian Liundi wa TGNP Mtandao akizungumza.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Lilian Liundi wa TGNP Mtandao akizungumza.

Na Thehabari.com — MTANDAO wa Wanawake na Katiba wenye mashirika zaidi ya 50 yanayotetea haki za wanawake katika Katiba mpya, umelipongeza mchakato na matokeo ya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa Bunge Maalum la Katiba (Mwenyekiti na Makamu wake) ambao umezingatia usawa wa jinsia.

Kauli hiyo imetolewa leo kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Lilian Liundi wa TGNP Mtandao kwa niaba ya Mtandao wa Wanawake na Katiba jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa licha

Ndoto ya bandari mpya Mbegani yakamilika

Meneja Miradi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Alexander Ndibalema (kulia, aliyesimama) akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, wawakilishi wa wanavijiji vya Mradi wa Bandari Mpya ya Mbegani na Timu ya Uthamini wa Ardhi wa eneo la mradi. Waliokaa viti vya mbele ni viongozi wa Timu ya ukaguzi, Bibi Florence Mwanri (wa pili kulia) na Prof. Longinus Rutasitara (wa tatu kulia). Kushoto ni Mratibu wa ziara hiyo, Bibi Salome Kingdom.
Meneja Miradi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Alexander Ndibalema (kulia, aliyesimama) akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, wawakilishi wa wanavijiji vya Mradi wa Bandari Mpya ya Mbegani na Timu ya Uthamini wa Ardhi wa eneo la mradi. Waliokaa viti vya mbele ni viongozi wa Timu ya ukaguzi, Bibi Florence Mwanri (wa pili kulia) na Prof. Longinus Rutasitara (wa tatu kulia). Kushoto ni Mratibu wa ziara hiyo, Bi. Salome Kingdom.

Na Saidi Mkabakuli — Tathmini iliyokuwa ikifanyika katika kutimiza ndoto ya kuwa na Bandari mpya ya Mbegani kufikia mwaka 2017 na kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16) imekamilika kwa takribani asilimia 90 ya eneo zima la mradi huo.

Hayo yamedhihirishwa na Mthamini Mkuu wa Ardhi ya Mradi huo, Mhandisi Emmanuel Mrema wakati akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya

Ukweli mchungu: Wapinzani hawana sifa za kuongoza nchi

UKWELI MCHUNGU: WAPINZANI HAWANA SIFA ZA KUONGOZA NCHI.

(A COMPARATIVE ANALYSIS)


Siasa ama chama chochote cha siasa ni zao la falsafa. Kuwa Mwanasiasa bila kuwa na falsafa ama kuwa na Chama cha Siasa ambacho hakina msingi wa falsafa ni kasoro kubwa ambayo hufanya mwanasiasa ama Chama Cha Siasa kutofanikiwa katika lengo lake kuu. Kukosa falsafa kunasababisha Mwanasiasa ama Chama Cha Siasa kutokuwa na dira ya kuifuata na matokeo yake ni kufanya siasa inayoegemea katika matukio na kukosoa mawazo na mipango ya wengine ama vyama vingine bila kuwa na WAZO kuu ambalo unalisimamia kama mwanasiasa ama Chama Cha Siasa. Kila mwanadamu kwa asili ya Uanadamu wake hujengwa na imani juu ya kitu fulani, uamini katika mlengwa fulani unaofahamika kwa jina la ITIKADI, Hivyo Chama Cha Siasa ni mkusanyiko wa kundi la watu ambao wanaamini katika ITIKADI moja, hivyo tukiitaja CCM directly tunataja UJAMAA kama ITIKADI kuu ambayo wanachama na Viongozi wa CCM wanaiamini na kuitetea kwa hoja na nguvu zote.

Utangulizi huo unamaana moja kuu katika makala hii niliyoipa jina "UKWELI MCHUNGU" kuwa CCM imejipambanua kwa itikadi yake na kuisimamia popote pale, wapinzani hawana msingi unaotokana na

Jihadhari na mtego huu wa kuiba password ya Facebook

via Evarist Chahali @ blogu ya KULIKONI

Jana nilifahamishwa na rafiki yangu mmoja kwamba ametumiwa barua pepe inayoonyesha kutoka kwa mwanasiasa mmoja wa huko Tanzania. Katika e-mail hiyo, mwanasiasa huyo anaonekana kulalamika kuhusu chapisho (post) lililowekwa na rafiki yangu huyo (japo hakuna chapisho aliloweka).

Ni kwa namna gani matapeli (hackers) hao hujaribu kukutega (trick) wapate password yako? 

Matapeli hao wanakupa link wanayodai ndiyo yenye chapisho (post) lako huko Facebook. Ukiibonyeza

Basi la Yanga lapata ajali

Taarifa katika ukurasa wa Facebook wa Young Africans Sports Club inasema kuwa basi la timu ya soka ya Yanga (Young Africans) lililokuwa limebeba wachezaji pamoja na viongozi wa benchi la ufundi, limepata ajali katika eneo na Mikese Mizani.

Ajali hiyo imesababishwwa na mabasi yaliyokuwa “yakitanua” kuelekea mikoani kuziba njia na kulilazimisha basi hilo kutumbukia kwenye mtaro.

Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa tatu na nusu asubuhi na hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa.

Timu inaondoka na usafiri wa basi jingine kuelekea jijini Dar es Salaam.

Umoja wa Wanawake Shirika la Masista Tanzania kukarabati shule ya Saranga

UMOJA wa Wanawake unaosimamiwa na Shirika la Masista Tanzania (DMI), umechukua jukumu la kukarabati chumba cha darasa kwenye Shule ya Msingi Saranga iliyoko Kimara wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, baada ya shule hiyo kujikuta miongoni mwa zile zinazokabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo ya uchakavu wa madarasa.

Akizungumza na waandhishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa umoja huo, Angela Mkemwa, alisema umoja huo unaoundwa na vikundi vidogo vidogo katika Kata ya Saranga umekusudia kuisaidia shule hiyo baada ya kusahauliwa na seriakali. Alisema zoezi hilo ni endelevu na

Rais Kikwete aonana na Maite Nkoana-Mishambane

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam, Machi 16, 2014.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Machi 16, 2014, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

Ujumbe huo wa Rais Zuma umewasilishwa kwa Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Maite Nkoana-Mashabane wakati mama huyo alipokutana na kufanya mazungumzo na

Vodacom Tanzania yatoa miavuli 20 kwa Jeshi la Usalama Barabarani

Mkaguzi Msaidizi wa usalama barabarani kanda ya Kinondoni, Byego Marwa akipokea msaada wa miamvuli (20)kutoka kwa Menaja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, msaada huo utawawezesha askari wa usalama barabarani kujikinga na mvua wakiwa katika maeneo ya kazi,wanaoshuhudia wa pili kutoka kulia ni Tumaini Kimaro, Simoni Lugangila na Emmanuel David. Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Viongozi wa Uamsho wafutiwa mashitaka

Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) wamefutiwa mashitaka na mahakama ya wilaya ya Mwanakwerekwe dhidi ya kesi ya kufanya mkusanyiko bila ya kibali iliofunguliwa Mei mwaka jana visiwani Zanzibar.

Uamuzi huo umetolewa na Hakim Ame Msaraka Pinja baada ya kukamilika kusikilizwa kesi hiyo na washitakiwa kuonekana hawana hatia katika mashitaka yaliokuwa yamefunguliwa na Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar, mwezi Mei mwaka jana.

Hakimu Pinja amesema kwa kuzingatia mashahidi wanne upande wa mashitaka pamoja na

[audio] Nje-Ndani: Kadari Singo (Mwakilishi wa Diaspora katika Bunge la Katiba) na Idd Sandaly

Katika kipindi cha NJE-NDANI kilichorushwa moja kwa moja na Jamii Production na Border Radio, tulimsikia Mwakilishi wa Diaspora katika Bunge maalumu la Katiba nchini Tanzania, Kadari Singo na Rais wa Jumuiya ya waTanzania Washington DC, Idd Sandaly wakizungumzia maendeleo na changamoto zinaizoikabili diaspora katika ajenda zake kwenye bunge hilo.

Karibu usikilize, ushirikishe na utoe maoni. (Tunaomba radhi kwa mawasiliano hafifu katika baadhi ya sehemu.)

Ridhiwani Kikwete katika harakati za kusaka kura Chalinze

Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze, ndugu Ridhiwani Jakaya Kikwete ameendelea na mikutano yake ya kusaka kura ili ashinde katika uchaguzi mdogo wa kiti cha Ubunge wa Jimbo la Chalinze unaotarajiwa kufanyika Aprili 6, 2014.

Zifuatazo ni picha na maelezo kutoka kwa Othman Michuzi kuhusu matukio hayo.

Ridhiwani pamoja na Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze, Steven Kazidi wakiwa na Mama wa Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Chalinze (aliefariki Dunia), Marehemu Said Bwanamdogo walipofika kumjulia hali nyumbani kwake Kijijini Miono, Bagamoyo, Machi 15, 2014.