Taarifa ya Dk Cyril Chami (Mb) kuhusu akaunti inayotumia jina lake Facebook

Dk Cyril A. Chami
Dk Cyril A. Chami

Naitwa Dr Cyril August Chami, Mbunge wa Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.

 Kwa miezi kadhaa sasa kuna mtu au kikundi cha watu ambaye/ambacho kimeunda akaunti feki kwenye Facebook kwa jina langu na kuitumia akaunti hiyo kunichonganisha na Chama cha Mapinduzi (CCM) na viongozi mbali mbali nchini Tanzania kwa lengo kuu moja: kunipaka matope na kuichafua taswira yangu mbele ya umma na ndani ya CCM.

Wanachokilenga (na hapa natumia wingi kwa sababu ndivyo nimeelezwa na Cyber Crime Unit of the Police Force Tanzania) ni kupambana nami kupitia mitandao ili tu 2015 nisiteuliwe na CCM kuendelea kugombea ubunge Jimbo la

Mbunge wa Kilwa, Murtaza Mangungu auchambua uraia pacha

Murtaza Mangungu
Murtaza Mangungu (picha: Maktaba)

Na Luke Joe -- Mhe. Mutaza Mangungu, Mbunge wa Kilwa (CCM) alizungumza na blogu ya Vijimambo mchana wa Jumatatu March 17, 2014 kutoka Dodoma na kuelezea suala la Uraia pacha.

Tafadhali bofya kitufe cha pleya liyopachikwa hapa chini kumsikiliza.


Bunge la Katiba kupewa semina na mshauri wa Rais wa Kenya, na Seneta Wako

Kamati ya Maridhiano ya Bunge Maalum la Katiba wameridhia Jaji Joseph Warioba kuwasilisha bungeni Rasimu ya Katiba Jumanne, Machi 18, 2014

Wabunge aw Bunge Maalum la Katiba wametakiwa kuhudhuria kikao cha bunge Jumanne, Machi 18, 2014 saa tatu asubuhi kwa shughuli za kuapishwa kwa wabunge 30 na kumsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba akiwasilisha Rasimu ya Katiba kwa saa nne.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha maridhiano kilichohudhuriwa na

Chaguzi ndogo Ubunge: Yatokanayo Kalenga; Matarajio Chalinze

Godfrey Mgimwa na mkewe Robby Mgimwa wakionesha hati ya ubunge baada ya kukabidhiwa (picha: Bongo Leaks blog)

AKIWA ameambatana na mkewe, Robby Mgimwa, Jumatatu ya Machi 17, 2014 Godfrey Mgimwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alitangazwa mshindi wa ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga baada ya kuvibwaga kwa kura za kishindo vyama vingine viwili vilivyoshiriki uchaguzi huo.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Jumapili ya Machi 16, mwaka huu, Mgimwa alizoa kura 22, 962 ambazo ni sawa na

Taarifa juu ya kikao cha Bunge la Katiba Jumanne Machi 18, 2014

Baada ya kutokea vurugugu zilizosababishwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum kupelekea Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji Joseph Warioba kutokuwasilisha rasimu ya pili ya Katiba kwa wajumbe hao, Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta aliitisha kikao cha maridhiano na baadhi ya wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali yaliyopo katika Bunge hilo ili kupata muafaka wa hoja zilizokuwa zimejitokeza.

Baada ya kikao hicho kilichodumu kwa takribani masaa manne na kumalizika saa nne za usiku, Mhe. Samuel Sitta amewaeleza waandishi wa Habari matokeo ya kikao hicho, ambapo wajumbe wa kamati hiyo

Kusini mwa Tanzania mbioni kupata hospitali ya rufaaMthamini Mkuu wa Ardhi wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Abdallah Komba (aliyeinama) akiwaelekeza namna ya hospitali ya rufaa ya mkoa huo itakavyokuwa wakati Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea mradi huo.


Na Saidi Mkabakuli — Wakazi wa mikoa ya kusini ikiwemo Mtwara, Lindi, na Ruvuma inatarajiwa kupata hospitali ya kisasa ya rufaa itakayojengwa katika eneo la Mikindani, nje kidogo ya mkoa wa Mtwara katika lengo la kuhakikisha kuwa ukuaji wa uchumi unakuwa shirikishi na kuendelea kuboresha huduma za jamii hususan na afya katika mikoa hiyo.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, Dkt. Shaibu Maarifa wakati akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya

Makamu wa Rais, Dk Bilal afungua kongamano la wawekezaji wa Israel na Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu, Machi 17, 2014

Na Frank Shija/MAELEZO -- Imeelezwa kuwa Tanzania ni nchi ambayo ina ardhi kubwa na yenye rutuba amaboya haijatumiwa kwa shughuli za kilimo na uzalishaji.

Hayo yamebainishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Gharib Bilal wakati akifungua kongamano la Kibiashara Baina ya Tanzania na Israel lililoanza leo jijini Dar es Salaam.

Dkt. Bilal amesema kuwa Tanzania ina jumla ya hekta milioni 44 ambazo ni nzuri na zenye rutuba na

Askari 4 wafukuzwa kazi, kushitakiwa kwa kujihusisha na ujambazi

Taarifa ya Jeshi la polisi (imepatikana via Habari24 blog) inasomeka ifuatavyo:

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewafukuza kazi kwa fedheha askari wanne wa Jeshi la Polisi kutokana na makosa ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

Askari waliofukuzwa wanatoka katika vikosi mbalimbali kama ifuatavyo:-
  1. E.6396 CPL RAJABU MKWENDA @ UGORO wa Makao Makuu ya Polisi.
  2. F.9412 PC SIMON wa Kituo cha Polisi Kati.
  3. F.9414 PC ALBERNUS KOOSA wa Kikosi cha Bendi ya Polisi Dar es Salaam.
  4. F.9512 PC SELEMAN wa Kituo cha Polisi Kigamboni.
Uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba askari hao wamekuwa wakijihusisha na uhalifu ikiwa ni pamoja na tukio la tarehe 09/03/2014 eneo la Mbezi Beach “A” ambapo majambazi wapatao 15 walifika katika ofisi ya

Scam alert: "MH370 Malaysia Airlines is found"

(image via Hacker9)

They are at it again.

Scammers don't care. Put it plainly in simple English, they don't have a heart, or else why would they harm another being?

They will turn any tragic event into an opportunity for self gain. Such is the world we live in.

Now beware.

There is a new fake video link circulating on some Facebook pages with this title: “Malaysia Plane Crash into Vietnam Sea MH370 Malaysia Airlines is FOUND” or something similar to it, all with a purpose of tricking people into

Zanzibar: Afa akiongea kupitia simu iliyopata hitilafu wakati ikichajiwa

Ali Bakari Ali (20) mkazi wa Kisima Majongoo mjini Unguja amekufa baada ya simu yake aliyokuwa akitumia ambayo ilikuwa imeunganishwa na chaja ya umeme kupata hitilafu.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema Ali alikufa baada ya kupata mshtuko wa umeme unaotokana na simu yake iliyokuwa imewekwa katika

Chimbuko la kikao cha Bunge la Katiba kuahirishwa leo Machi 17, 2014


Jumatatu ya leo, Machi 17, 2014 Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mhe. Sammuel Sitta amelazimika kukiahirisha kikao kilichokuwa kinaendelea jioni baada ya kutokea kutoelewana bainaa ya wajumbe na wabunge wa bunge la katiba.

Vurugu zilitokea pale Mhe. Sitta alipomruhusu Jaji Joseph Sinde Warioba (Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba), awasilishe Rasimu ya Katiba hiyo Bungeni.

Baadhi ya wajumbe hawakukubaliana na hatua hiyo na ndipo wakaanza kujibizana huku wengine

Dampo lalazimisha familia kula chakula ndani ya neti kuepuka kipindupindu

Moja ya familia zilipata chakula ndani ya neti kuepuka nzi wanaoambukiza kipindupindu.

via HabariLeo -- Katika harakati za kujikinga na maradhi na usumbufu wanaoupata wa nzi majumbani, wakazi wanaoishi karibu na eneo la Dampo la Pugu Kinyamwezi, Ilala jijini Dar es Salaam wamebuni mbinu mpya za kukabiliana na tatizo hilo na sasa familia zinalazimika kula chakula zikiwa ndani ya vyandarua.

Na imefahamika kuwa, ili kutochosha vyandarua vyao, familia nyingi katika eneo hilo zinakuwa na vyandarua vya ziada, vingine vikitumika wakati

First African Retail Development Index: Rwanda tops, Tanzania comes 4th

- Ground breaking Report Sheds Light on Retail in Africa

- Rwanda, Nigeria, Namibia, Tanzania and Gabon occupy the top five places of the inaugural A.T. Kearney African Retail Development Index (ARDI)

- A.T. Kearney Study provides global retailers with direction on entering specific African countriesJOHANNESBURG, South-Africa, March 17, 2014/ -- A new study designed to help large, organized retailers determine where and how to best enter Sub-Saharan Africa’s rapidly growing retail sector is published by A.T. Kearney (atkearney.com), a leading global strategy consultancy firm, today.


Rwanda, Nigeria, Namibia, Tanzania and Gabon occupy the top five places of the inaugural A.T. Kearney African

Nyumba inapangishwa


Nyumba yenye vyumba vitatu kikiwemo Master Bedroom inapangishwa maeneo ya Mbezi Beach, barabara ya Muafaka nyuma ya Art Gallery almaaruf, Jogoo, jijini Dar es Salaam.

Nyumba hii inauzio pamoja na geti.

Kama utapenda kupangisha unaweza kupiga namba 0754-367995 , 0777-967995 na

SUA trainings on Kiox - search tool powered by LibHub

Please register for more skills on searching using Kiox as search tool powered by LibHub on your convenient day and place.

Click here to check the timetable and mail to register and book a place to [email protected] or [email protected] 

See also Poster1 and Poster2 for details.

Filamu ya Kitendawili ipo sokoni

Serikali yaungwa mkono katika kutenga bajeti kukabiliana na vifo vya uzazi

Washiriki anuai kutoka Mkoa wa Rukwa wakiwa katika picha za matukio.

ZAIDI ya wananchi 16,828 wa Mkoa wa Rukwa wamesaini ombi la haki (petition), wakiiomba Serikali kutenga bajeti mahususi ili kuviinua vituo vya afya nchini viweze kutoa huduma za dharura kwa za uzazi ikiwemo upasuaji, damu salama, vifaa vya kutosha na wafanyakazi wenye ujuzi.

Taarifa hiyo imetolewa na Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama, Bi. Rose Mlay jana mjini