Hatimaye familia za Kleruu na Mwamwindi zakutana ana kwa ana

Eva Kleruu na Amani Mwamwindi baada ya kukutana
Eva Kleruu (kushoto) na Amani Mwamwindi walipokutana.

Rejea simulizi la Rashidi Mkwinda: “Eva, mwanaye Dk Kleruu mwenye nia ya kukutana na familia ya Mwamwindi, amsimulia...” leo, mwanahabari Frank Leonard anaripoti kwenye blogu yake kuwa: SIMANZI na machozi yalibubujika wakati familia mbili za Dk Wilbert Kleruu na Said Mwamwindi zilipokutana juzi mjini Iringa kwa ajili ya maridhiano yaliyoondoa tofauti zao.

Dk Kleruu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa Desemba 25, 1971 na Mamwindi aliyekuwa mkulimaa maarufu wa mahindi katika kijiji cha Isimani, wilayani Iringa.

Tangu kifo cha Mkuu wa Mkoa huo kitokee miaka 43 iliyopita, kabla ya kukutana juzi, familia hizo mbili hazikuwahi kukutana.

Watoto wa kwanza wa familia hizo, Eva Kleruu (56) na Amani Mwamwindi (63) ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa kwa niaba ya familia zao walikutana na kufanya maridhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, mjini Iringa juzi.

“Hotuba ya Rais siyo rasimu iliyoko bungeni, ule ni msimamo wa CCM”

Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wamesema watajibu hotuba ya Rais Kikwete kwenye Bunge Maalum la Katiba na nje ya Bunge kwa kutumia taarifa mbalimbali za tume ya marekebisho ya katiba ambazo zimefanyiwa utafiti wa kina.

Katika mazungumzo yao na waandishi wa habari jana, viongozi wa umoja huo ambao ni kutoka vyama vya upinzani pia walishukuru wabunge wao kwa kutotoka nje ya Bunge wakati Rais Kikwete anahutubia licha ya kuwa hotuba hiyo haikuwafurahisha kabisa.

Mwenyekiti mwenza wa UKAWA, Profesa Ibrahimu Lipumba alisema watakachojadili bungeni ni rasimu ambayo imetokana na maoni ya wananchi ambayo imewasilishwa bungeni na mwenyekiti wa tume ya

Mrejesho wa Wajumbe Bunge la Katiba wa “Tanzania Kwanza” kuhusu hotuba ya Rais Kikwete kwenye Bunge Maalumu

Maelezo kwa njia ya sauti yamepachikwa mwishoni mwa taarifa ifuatayo ya maandishi:

Sisi Wajumbe Wa Bunge Maalum la Katiba tunaotoka makundi mbalimbali na pia tunaoamini katika kauli mbiu isemayo “TANZANIA KWANZA”, tunapenda kutoa tamko rasmi la kuunga mkono hotuba aliyoitoa Mheshimiwa Rais alipokuwa akihutubia Bunge Maalum la Katiba Tarehe 21/03/2014 kama ifuatavyo: 

Kwanza, tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kwa hotuba yake aliyoitoa wakati akizundua Bunge Maalum la Katiba tarehe 21 Machi 2014. Tunaamini Rais, kama Mkuu wa Nchi, alikuwa na haki na wajibu wa kutoa mwelekeo na maono yake kuhusu Rasimu ya Katiba na hatua hii tuliyonayo sasa ya kuipitia Rasimu kwenye Bunge la Katiba. Tunafarijika kwamba hotuba hiyo imepokelewa vizuri na Watanzania wengi kwenye kila kona ya nchi yetu na wengi wao wamekuwa wakitutumia ujumbe wakituhimiza kuizingatia hotuba hiyo katika kutimiza wajibu wetu.

Pili, tunamshukuru Rais kwa uchambuzi wake wa kina wa Rasimu na ushauri wake kwetu kuhusu haja ya

Mbunge wa Nzega anurusika huku mmoja akipigwa risasi usoni


Mbunge wa jimbo la Nzega, Dkt Hamis Kigwangalla facebook status


Kadama Malunde, Nzega — Jeshi la polisi wilayani Nzega mkoani Tabora limetumia nguvu kusambaratisha maandamano ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu yaliyolenga kupinga kufungwa kwa machimbo yao ya Mwashina yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania Limited wilayani Nzega.

Mara baada ya kukaribia katika eneo la machimbo ambako maandamano yalikuwa yanaelekea, kabla hata hawajafika eneo la machimbo, ghafla polisi waliibuka na kuanza kurusha mabomu hovyo na baadaye

Kiongozi wa Wizara amtetea Shikuba, ‘bilionea wa dawa za kulevya’

Baadhi ya viongozi wakubwa katika Serikali ya Rais Kikwete wametajwa kuwa ndiyo chanzo cha kudhoofisha juhudi za kupambana na vita dhidi ya mihadarati kwa kuwakumbatia watuhumiwa waliokamatwa.

Mmoja wa vigogo hao anayefanya kazi katika wizara nyeti, ametajwa 'kumpigania' bilionea aliyekamatwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam akituhumiwa kuhusika na shehena ya kilo 210 za dawa za kulevya aina ya heroin zinazokisiwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 10 ambazo zilikamatwa nchini mwaka 2012 mkoani Lindi.
Tayari bilionea huyo, Ali Khatib Haji 'Shikuba' ameshafunguliwa mashitaka, kesi yake ikiunguruma katika

Ridhiwani Kikwete azuru shule inayotumia darasa moja

Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji cha Kikwazu, Mussa Yahaya kuhusu shule ya msingi Kikwazu iliezuliwa paa na kimbunga mwanzoni mwa mwaka huu na kubakisha darasa moja tu linalotumika.

Kimbiji walaumu kuvamiwa na kuharibiwa makazi, mshamba

Kikosi kimoja kinachodaiwa kuwa ni cha askari wa Jeshi la Wananchi kinatuhumiwa kuvamia maeneo ya wananchi na kuvunja makazi na kufanya uharibifu mkubwa katika huko eneo la Kimbiji, Temeke, Dar-es-Salaam.

Hali hiyo imewaacha wananchi wakiishi kwa mashaka. Wenyeji wa Kimbiji ambao wanamiliki maeneo yao na ni wakazi wa asili maeneo hayo wamesema wamekuwa wakipewa vitisho vya wanajeshi wenye nia ya kuwanyang'anya ardhi kwa kutumia kofia za jeshi.

---
Ujumbe via eMail.
Bofya hapa kusikiliza mahojiano baina ya Vijimambo blog na Mwenyekiti wa Kijiji husika.

Picha za misa ya maombolezo kwa kifo cha Caroline Mwaiselage

maerehemu Caroline Mwaiselage

Na Luke Joe -- Picha za misa ya kumbukumbu iliyofanyika siku ya Jumamosi March 22, 2014 College Parka Maryland kwa ajili ya maerehemu Caroline Mwaiselage aliyekuwa mfanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani aliyekutwa na mauti alipokua amekwenda Tanzania, Machi 7, 2014 mwaka huu.

Katabazi: Hivi ndivyo tunavyopambana kweli na dawa za kulevya?

SERIKALI pamoja na wananchi miongoni mwetu tumekuwa tukijinasibu kuwa tunapiga vita matumizi ya dawa za kulevya ‘unga’ yenye mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi.

Hoja ya kupiga vita biashara hii haramu inatokana na bidhaa yenyewe kusababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji pamoja na kuichafulia sifa nzuri nchi ya Tanzania inayoonekana ni kitovu cha usafarishaji wa dawa hizo.

Serikali na taasisi mbalimbali za umma zimekuwa zikiibuka pale wanapokamatwa watuhumiwa wa dawa hizo wakiwa na uzito mkubwa au kuwahusisha watu wenye majina makubwa.

Wakati huo ndiyo huonekana mwanasiasa fulani akijinasibu kuwa kinara wa kupinga usafirishaji, uuzaji na

[video] Tanzania msiige Katiba za wenzenu - Amos Wako

Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Kenya, Amos Wako ameliasa Bunge Maalum la Katiba lisinakili michakato ya Kikatiba toka nje, kwani yale yaliyofanywa na nchi nyingine hayaakisi wala kukidhi matakwa ya Watanzania.

Wako, ambaye hivi sasa ni Seneta wa Kaunti ya Busia, aliweka hayo bayana katika semina mahsusi ilofanyika Dodoma, wakati akielezea yale Kenya iliyokumbana nayo wakati ikiandika Katiba yake mpya -- MCL inaripoti zaidi kwenye video iliyopachikwa hapo chini.

Tuhuma za Polisi kuua: Familia ya Massawe kushitaki Mahakamani

FAMILIA ya marehemu Elineema Massawe imesema wanajipanga kwenda mahakamani wiki ijayo wakidai kupata uhakika kuwa kifo cha ndugu yao chanzo chake kimetokana na kipigo alichopatiwa na polisi wa kituo cha Mbezi kwa Yusufu.

Akizungumzia kifo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Godfrey Shoo, alisema wanawashukuru Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuweka ukweli hadharani kuhusu kifo cha Massawe.

Alidai kuwa kwenda kwao mahakamani kunatokana na viashiria mbalimbali vilivyoelezwa na Daktari (jina tunalo), aliyefanya upasuaji kwamba marehemu alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa tetenasi uliyotokana