[video] UKAWA wazungumzia mgomo dhidi ya Kamati ya Kanuni ya Bunge la Katiba

Viongozi wa UKAWA (kutoka kushoto: James Mbatia, Freeman Mbowe, Ibrahim Lipumba na Tundu Lissu), wakionyesha mshikamano huku baadhi ya wabunge wakizomea.

Kwenye video iliyopachikwa hapo chini, viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao ni wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, waheshimiwa. James Mbatia, Freeman Mbowe na Prof. Ibrahim Lipumba wanazungumzia sababu za kuigomea Kamati ya Kanuni ya Bunge la Katiba siku ya Jumatano, Machi 26, 2014.

Notice: Changes to the UK Visa application centre in Tanzania

British High Commissioner-Dianna Melrose (left) Kashif Chaudry-Regional Director Africa-UK Visas and Immigration (center) and Rebecca Hadlow (Right)

NEXT GENERATION OUTSOURCED VISA (NGOV) PROJECT

PRESS RELEASE

Tanzania
25 March 2014

On 31 March, our new commercial partner for UK visa services, Teleperformance Ltd., will take over the running of our Visa Application Centre in Tanzania. The Visa Application Centre will be moving from its current location at the British High Commission to different premises in Dar es Salaam as follows:

New Teleperformance Application Centre Address
Viva Towers,
294-295 Ali Hassan Mwinyi Road,
Upanga,
Dar es Salaam,
Tanzania.

Date of Relocation
31 March 2014.

UK visa customers will continue to complete their applications and pay their visa fee online at Visa4UK before selecting an appointment at the Teleperformance application centre. Hours of operation at the new centre will be

Tamko la Mtandao wa Watu wa Pemba kuhusu hotuba ya Rais Kikwete kwenye Bunge la Katiba

NEPPELTA

NETWORK FOR PEOPLE OF PEMBA LIVING IN TANZANIA MAINLAND
MTANDAO WA WATU WA PEMBA WAISHIO TANZANIA BARA

MAKUNGANYA STREET/ KARIAKOO
P.O. BOX 21243
DAR ES SALAAM
23/03/2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

TAMKO RASMI LA KUUNGA MKONO HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE LIYOITOA KWA BUNGE MAALUMU LA KATIBA, DODOMA TAREHE 21/03/2014.


Ndugu,
Waandishi wa habari,

Tunamtanguliza Mwenyezi Mungu mwingi wa rehemu, heri na Baraka.

Mpango wa kuunganisha nchi za Zanzibar na Tanganyika ambao mchakato wake ulianza mwaka 1963 ulikuwa ni utashi wa Viongozi wetu wawili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Marehemu Mzee Abeid Aman Karume.

Wote wawili kupitia vikao vyao mbalimbali walikubaliana kuziunganisha nchi hizi kwa maslahi mema ya

Mkutano wa CUF Kibanda Maiti: “Sikutarajia hata siku moja Rais Kikwete atafitinisha watu” Maalim Seif

  • video za mkutano mzima unaweza kuzitizama kwa kubofya hapa

Katibu Mkuu wa CUF Mhe.  Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Kibanda Maiti, Zanzibar


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema hakufurahishwa na baadhi ya kauli zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete alipokuwa akizindua Bunge Maalum la Katiba na ameamua kumwandikia barua kumueleza masikitiko yake.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama cha CUF katika viwanja vya Kibandamaiti, Mhe. Maalim Seif alisema, Rais Kikwete kama mkuu wa nchi, hakupaswa kuingiza

M/Kiti Bunge la Katiba aahirisha kikao: Kanuni hizi hazijadiliki, hazipiti!

*Video fupi ya hali ilivyokuwa ndani ya ukumbi wa Bunge imepachikwa hapo chini baada ya taarifa ya Bi. Salma Said (Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba) aliyoandika kwenye blogu yake, wavuti.com inainukuuu ifuatavyo:-

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu akizungumza juu ya ukiukwaji wa kanuni za bunge, pembeni ni mjumbe wa bunge hilo kutoka Taasisi za Kidini, Sheikh Thuwein Issa Thuwein na mbele ni Mhe. Anna Kilango.
Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu akizungumza juu ya ukiukwaji wa Kanuni za Bunge, pembeni ni mjumbe wa bunge hilo kutoka Taasisi za Kidini, Sheikh Thuwein Issa Thuwein na mbele ni Mhe. Anna Kilango.

Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba hawajaridhishwa na mwenendo wa Mwenyekiti wa Bunge hilo Samweli Sitta namna anavyoendesha vikao na kukiukwa baadhi ya kanuni za bunge hilo, Mjumbe wa Bunge hilo Tundu Lissu leo alionesha kutoridhishwa kwake na kusema kanuni zilizobadilishwa hazijadiliki wala hazipiti.

Naye Abubakar Khamis Bakar alisema haiwezekani bunge likakiuka kanuni na wajumbe wakaendelea kunyamaza kimya. 

Ismail Jussa alihoji kwa Mwenyekiti wa Bunge hilo kwamba kanuni zilizotungwa na kuridhiwa na wajumbe wote vipi

Two men in Tanzania riding a bike, " ? in style"

THE young men above ride a bicycle on the streets of the capital, Dodoma, Tanzania in a peculiar manner, with the one given a lift sitting on the handle bar while facing the rider. (Photo by Hilary Bujiku of PMO/DAILY NEWS)

Two more photos below...

Muhtasari wa ratiba ya mazishi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, John TupaTaarifa kutoka Musoma zinaeleza kuwa mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa (aliyezaliwa Januari Mosi, 1950 na kuaga dunia asubuhi ya jana) unatarajiwa kuagwa kesho nyumbai kwake kuanzia 1 mpaka saa 3 asubuhi na baadaye kupelekwa katika Kanisa Kuu la Katoliki, Parokia ya Musoma kwa ajili ya ibada itakayoanza saa 5 adhuhuri hadi saa 9 alasiri.

Katibu Tawala wa Mkoa bwana Benedictor Ole-Kuyan amesema baada ya ibada, mwili wa marehemu utasafirishwa hadi uwanja wa ndege wa Mwanza ambapo

Bongo Movie, Mabibo Beer Co. watoa misaada hospitalini Mwananyamala

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer ambao ni wauzaji wa vinywaji vya Windhoek na Climax, Mama Benadetha Rugemalila akikabidhi baadhi ya misaada kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Bw Kariamel Wandi wakati Kampuni ya Mabibo Beer wakishirikiana na Wasanii wa Bongo movie walipotembelea Hospitali ya Mwanyamala ikiwa wanaadhimisha miaka mitatu ya Kuanzishwa kwa Klabu ya Bongo Movie.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila akikabidhi baadhi ya misaada kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Bw Kariamel Wandi wakati Kampuni ya Mabibo Beer wakishirikiana na Wasanii wa Bongo movie walipotembelea Hospitali ya Mwanyamala ikiwa wanaadhimisha miaka mitatu ya Kuanzishwa kwa Klabu ya Bongo Movie.

Kampuni ya Mabibo Beer ambao ni wauzaji wa vinywaji vya Windhoek na Climax kwa kushirikiana na Wasanii wa Bongo Movie leo wametembelea hospitali ya Mwananyamala kwenye maadhimisho ya miaka mitatu ya kuzaliwa kwa Klabu ya Bongo Movie.

Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bw Steve Nyerere walitoa misaada kwa wagonjwa katika hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na mabeseni ya kuogeshea watoto, pampers, sabuni na mafuta ya kujipaka.

Sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Bongo Movie zitafanyika katika ukumbi wa Arcade East 24 uliopo Mikocheni kwa burudani kutoka FM Academia, Banana Zoro Band na msanii Shilole.


Wasanii wa bongo movie wakielekea kwenye wodi za wagonjwa katika hospitali ya Mwananyamala.


Mmoja wa akina maama akipokea misaada kutoka kwa mmoja wa wasanii wa Bongo Movie.


Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Bw Steve Nyerere (kushoto) akisisitiza jambo kwa wenzie.

Mkuu wa Chuo GTI afungua mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Katiba

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya

Na TheHabari Team -- MKUU wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo leo jijini Dar es Salaam amefungua mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yaliyowashirikishwa washiriki kutoka katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Pwani na Morogoro.

Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Jinsia kilichopo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, Bi. Zuki Mihyo alisema kutokuwepo na misingi imara ya kutetea, kulinda na

Kipindi kipya cha Tv cha wafanyakazi majumbani "Dada Jijue"

Joyce Kiria/Wanawake Live

Usikose kipindi kipya cha 'DADA JIJUE' kutoka kampuni ya Wanawake Live TV kitakachofundisha wafanyakazi wa kazi za majumbani. 

Kipindi hicho kitawafunza mbinu mbalimbali za kufanya kazi zao kwa ufanisi na

M-pesa yapendezesha maadhimisho wiki ya Ustawi wa Jamii

Dk Steven Kebwe (kulia) akipewa maelezo na Mwezeshaji wa kikundi cha wajasiriamali kutoka Karatu Jane Mwelye.

Dar es Salaam, 26 Machi 2014 . . . . Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zinazoshehereka wiki ya Ustawi wa jamii duniani, Imeelezwa kuwa teknoloji ya simu imekuza ajira na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kuchangia ustawi bora wa jamii.

Maadhimisho hayo yaliyozinduliwa na Naibu Waziri wa afya na Ustawi wa Jamii Dk. Steven Kebwe, kwa kutoa wito kwa jamii ya Watanzania kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha huduma za Afya na Ustawi wa jamii, na kutoa

“Nilipingana na Mwl. Nyerere... nikafukuzwa ukuu wa mkoa” Kingunge

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Kingunge Ngombale Mwiru, alisema kuwa aliwahi kuvuliwa wadhifa wa ukuu wa mkoa kwa sababu ya kutofautiana kimtazamo na hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere.

Kingunge alikumbushia tukio hilo juzi katika semina ya waandishi wa habari iliyofanyika mjini Dodoma katika Ukumbi wa Msekwa, naye akiwa mmoja wa watoa mada.

Akijibu swali la mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima la kwa nini amegeuka mlalamishi wa kukosoa viongozi wenzake wa sasa wakati amekuwa sehemu ya serikali kwa awamu zote nne bila kutimiza wajibu wake, Kingunge alisema kuwa amekuwa akikosoa na wakati fulani iliwahi kumgharimu:
“Wakati fulani nikiwa mkuu wa mkoa, nilipingana na Mwalimu Nyerere nikikataa katiba isibadilishwe kwa manufaa ya watu fulani, basi nikafukuzwa ukuu wa mkoa. Hivyo si kweli kwamba sikukosoa, hata sasa naendelea.”


TBC Jambo Tanzania: TanzaniaKwanza, UKAWA katika Bunge la Katiba

Mazungumzo na Dkt Emmanuel Nchimbi na Charles Mwijage katika kipindi cha Jambo Tanzania kuhusu suala la makundi ya wajumbe wa Tanzania Kwanza na UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi) katika Bunge Maalumu la Katiba.

[video] Watanzania waliokamatwa China na mihadarati huenda wasinyongwe

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule amesema kutokana na uhusiano wa karibu wa kidiplomasia na nchi ya China, watu 15 waliokamatwa na dawa za kulevya nchini humo huenda wasinyongwe na badala yake watakabiliwa na kifungo cha  maisha gerezani nchini humo.

Tizama video ya KURASA za EATv iliyopachikwa hapo chini kwa taarifa zaidi...

Maalim Seif plans public rally to protest Pres. Kikwete’s speech

via The Citizen — Zanzibar’s First Vice President, Mr Seif Shariff Hamad, is today scheduled to address a public rally in Zanzibar to express the views of the Civic United Front (CUF) on the progress of the Katiba review process, it was announced yesterday.

Confidants of Mr Hamad said he will use the rally at Democracy Grounds in Unguja to express the party’s disappointment with last Friday’s speech by President Jakaya Kikwete to members of the Constituent Assembly. Both Dr Shein and Mr Hamad attended Kikwete’s official address to the CA as state officials.

A member of the Zanzibar House of Representatives for Stone town Mr Ismail Jussa Ladhu confirmed the rally to The Citizen on Monday: “He will tell the people of Zanzibar what their next step should be after President Kikwete appeared to play down their views in the proposed new Constitution,” he said.