[video] Siku Mhe. Lipumba aliposimama na kutamka sababu ya kukataa alipoteuliwa kuwa mjumbe, Kamati ya Uongozi, Bunge Maalumu la Katiba

Kura ya SIRI vs WAZI: Michango ya Wajumbe ndani ya Bunge la Katiba

Video iliyorekodiwa na "Kamati ya Maridhiano" ikiwaonesha wajumbe mbalimbali wa Bunge Maalumu la Katiba hapo jana, Alhamisi, Machi 27, 2014 wakitoa maoni na michango yao kuhusiana na mvutano kuhusu aina ya upigaji kura, ama iwe ya wazi au ya siri.

Video imepachikwa hapo chini...


Job opportunity at BBC Tanzania for Senior Mentor/Trainer

Location: Tanzania

Reports to: Niambie Project Manager

Contract duration: 12 months (with possible extension)


Application instructions: Candidates should send their CV and a covering letter (PDF or Microsoft Word format) which outlines their experience and suitability for the role in English to [email protected]. The name of the position applied for should be included in the subject line of the email.

Please do not send certificates or other attachments. Applicants with no separate covering letter will not be

Mvua yaongeza kero ya usafiri na makazi Dar es Salaam


Dar es Salaam, asubuhi ya Ijumaa, Machi 28, 2014
Mvua zilizoanza kunyesha juzi usiku na kuenelea jana na leo asubuhi jijini Dar es Salaam zimesababisha adha katika makazi ya watu hasa wanaoishi katika maeneo ya mabondeni na watumiaji wa barabara kutokana na miti kuanguka na kuziba njia huku maji yakijaa barabarani na kusababisha ugumu kwa vyombo vya moto kupita, kama inavyoonekana kwenye video na picha zifuatazo kutoka kwa wadau...

Ofisa JWTZ afungwa kwa kujipatia faida kwa njia ya ulaghai

Hakimu Mkazi Waliarwande Lema wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana alitoa hukumu ya kumfunga Meja Muhsin Kombo, Mwanajeshi wa JWTZ  kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hatia ya kughushi.

Kombo na mkewe Devotha Soko walikuwa wanakabiliwa na mashitaka sita ya kupanga njama, kughushi, kutoa taarifa za uongo na kujipatia Sh milioni 100 kwa njia ya udanganyifu.

Jaji Lema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 19 na vielelezo vya upande wa Jamhuri pamoja na

[video] Bunge la Katiba: Mchango wa Mwigulu Nchemba kuhusu mfumo wa kupiga kura

Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalumu, Pandu Ameir Kificho, jana aliwasilisha mapendekezo ya Azimio la Bunge Maalumu la kufanya marekebisho ya Kanuni ya 37 na 38, ili Bunge liazimie kura zote, za wazi na za siri, zitumike kufanya uamuzi mmoja.

“Kanuni zetu za Bunge Maalumu zimeweka fursa hiyo ya kufanya marekebisho au mabadiliko ya kanuni hizo. Dhamira ya kufanya marekebisho haya ya kanuni inatokana na sababu ifuatayo.
“Jambo la msingi lililosababisha kufanya mabadiliko ya kura zetu, ni msingi wa kanuni ya 38 (2) ya Kanuni za Bunge Maalumu ambayo ilieleza kuwa, utaratibu wa kupiga kura utakubaliwa na Bunge hili baadaye.
“Kwa msingi huo, mabadiliko ya kanuni hizo, yanapendekeza kuziba pengo lililokuwepo katika utaratibu wa kupiga kura kwa kupendekeza kuziba pengo lililokuwepo katika utaratibu wa njia zote mbili za kura, yaani utaratibu wa kura ya siri au kura ya wazi kadri kila mjumbe atakavyochagua utaratibu wa kutumia katika upigaji kura,” 
alisema Kificho.

Pamoja na mapendekezo hayo, mgawanyiko uliozoeleka ndani ya Bunge, kati ya

Fainali za muziki wa dansi, taarabu, kizazi kipya na utenzi kwa ajili ya Miaka 50 ya Uhuru

Kama tunavyofahamu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unatimiza miaka 50 tarehe 26 Aprili, 2014. Kutokana na ukweli kwamba huu ndio muungano pekee wa nchi mbili uliodumu kwa muda mrefu kuliko yote barani Afrika. Ndio maana Serikali imeona vemakuadhimisha sherehe hizo zikiwahusisha wananchi kwa nderemo na vifijo vingi.

Maadhimisho ya mwaka huu ni maalum na yalizinduliwa na Mhe. Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi tarehe 01/03/2014 huko Zanzibar. Sherehe zitafanyika kwa mbwembwe za matukio mbalimbali tayari yamefanyika na mengine yanaendelea kufanyika. Kauli mbiu ya Maadhimisho haya ni UTANZANIA NI MUUNGANO WETU, TUULINDE TUUIMARISHE NA KUUDUMISHA.

Tarehe 29/03/2014 kutakuwa na Fainali za Muziki wa Dansi,Taarabu, Kizazi kipya na

This Saturday is Back to College Bash @ New Landmark Resort


Maoni ya wadau: Wanawake hawapendi kuwapigia kura wanawake wenzao?

Ni swali ambalo watu hujiuliza hasa ukizingatia kuwa takwimu zinaonesha kwamba wanawake ni wengi zaidi ya wanaume katika jamii.

Kama ni hivyo, ni kwa nini wagombea wengi wa nafasi mbali mbali za uongozi ambao ni wanawake hushindwa katika chaguzi?

Je, ni kwamba wanawake hawapendi kuwapigia kura wanawake wenzao? Na kwa nini wanawake hawachaguani?

Sikiliza maoni ya wadau wengi hapa kwa kutazama video hii:-

The fast emerging oil and gas frontier region: 5th Eastern Africa Oil, Gas-LNG & Energy Conference


PRESS RELEASE


5th Eastern Africa Oil, Gas-LNG & Energy Conference - 28 – 30 April 2014, Intercontinental Hotel, Nairobi, Kenya

Eastern Africa: The fast emerging oil and gas frontier region


NAIROBI, Kenya, March 27, 2014/ -- With a 35+year track record in and on Africa, Global Pacific & Partners (www.glopac-partners.com) hosts this landmark meeting on Eastern Africa. Now in its 5th year, Global Pacific & Partners invites you to this annual event held in Nairobi, Kenya, providing unrivalled new

Bomba la gesi Mtwara-Dar es Salaam kukamilika Julai 2014

Mhandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela (Kulia) akiwaonesha mabomba ya kusafirishia gesi Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea baadhi ya maeneo yanakopita mabomba hayo. Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita 492 zimeshatandazwa.
Na Saidi Mkabakuli -- Maendeleo ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu kufuatia kuendelea vyema kasi ya kundaza bomba hilo.

Wakizungumza na wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Wahandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela na Mhandisi Omary Kitiku wamesema kuwa kasi ya sasa ya

Tamko la Serikali kuhusu wachimbaji wadogo na mgodi wa Resolute

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU UVAMIZI WA WACHIMBAJI WADOGO KATIKA ENEO LA MGODI WA KAMPUNI YA RESOLUTE (T) LIMITED.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

(SML NA. 19/97) WILAYANI NZEGA


1.UTANGULIZI

Kampuni yaResolute (T) Ltd (RTL) inamiliki Mgodi wa Golden Pride ulioko katika eneo la Lusu, wilayani Nzega. Mgodi huo unaendeshwa chini ya leseni ya uchimbaji mkubwa yenye namba SML 19/97 iliyotolewa tarehe 15/05/2000 ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 38.74, na itafikia ukomo tarehe 14/05/2015.

Kampuni ilianza uchimbaji mwaka 1998, na Mgodi huo ulifunguliwa rasmi tarehe 6 Februari, 1999. Uwekezaji katika mgodi huo uligharimu dola za marekani milioni 77, na uzalishaji ulifikia wakia za dhahabu 180 kwa mwaka. Kampuni kwa sasa iko katika hatua za ufungaji mgodi baada ya kukamilisha shughuli za uchimbaji na uchakataji wa mawe ya dhahabu.

Mgodi wa Golden Pride ni wa shimo la wazi (Open Pit Mine). Shughuli za uchimbaji katika mgodi huo zilifikia ukomo Januari 2013. Aidha, Uchakataji wa mawe ya

Timu ya soka ya “andunje” wa Brazil

Video inawaonesha wacheza soka wa timu ya watu wafupi (mbilikimo, "andunje") wa nchini Brazil wakisakata kabumbu.

Moja ya sheria inayoruhusiwa katika mchezo huo ni ya kumbeba mchezaji mwingine ili “kujenga ukuta” katika jitihada za kuzuia mpira wa adhabu ndogo kuelekea golini.

Tuna maiti ya Muungano bila kujua - Ndi

Na Ndimara “Ndi” Tegambwage — WAJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba, juzi Jumamosi jijini Dodoma, walishuhudia Chama Cha Mapinduzi kikishinikiza matakwa yake katika utungaji wa Katiba Mpya.
Walimwona Rais Jakaya Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa CCM, kwanza akiuma na kupuliza na baadaye akimwaga nyongo na hapa na pale, akitetea na kushinikiza matakwa ya chama chake.
Hakika Rais Kikwete hakwenda Dodoma kufanya ufunguzi wa shughuli za kujadili Rasimu ya Katiba Mpya; bali alikwenda kuweka vijembe, vitisho na msimamo wa chama chake juu ya mambo kadhaa; lakini zaidi juu ya mfumo wa Muungano wa serikali tatu.
Kinachosumbua wengi ni kwamba rais kwanza, ameonyesha kutoona mambo muhimu; na pili, ameonyesha kuwa mwoga.
Rais amekataa kuona kuwa leo hii hakuna Tanzania moja kama ilivyokuwa tangu mwaka 1964. Bali

Ujerumani kutumia euro milioni 10 kukarabati reli ya kati

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Dkt. Frank Steinmeier akizungumza waandishi wa habari kwenye mkutano huo jijini Dar es Salaam na kuelezea mafanikio ya ushirikiano wa nchi hizo mbili.

Habari na Damas Makangale, MOblog Tanzania -- SERIKALI ya Ujerumani kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania imeahidi kutumia zaidi ya Euro milioni 10 kukarabati reli ya kati (Central Line Railway).

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani nchini, Dkt Frank-Walter Steinmeier, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard Membe amesema serikali ya Ujerumani imekubali kwa dhati kabisa kukarabati reli ya kati kwa manufaa ya Tanzania na nchi jirani.

“kwa sasa siwezi kusema ukarabati utaanza lini na jina la mwekezaji kwa sababu

[video] Mkutano wa CUF Kibanda Maiti, Machi 26, 2014

Video za mkutano wa CUF uliofanyika katika viwanja vya Kibanda Maiti, huko Zanzibar jana Jumatano, Machi 26, 2014 ukizungumzia masuala ya Serikali, Muungano na yatokanayo na Rasimu ya Katiba Mpya, Randama ya Katiba Mpya na Hotuba ya Rais Kikwete kwenye Bunge la Katiba.

Baadhi ya Wazungumzaji ni Eddy Riyami, Mansour Yusuf Himid na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.

Video (kwa hisani ya "Kamati ya Maridhiano" zimepachikwa katika "playlist" iliyopachikwa hapo chini.

Rais wa SMZ kuwatunuku nishani waliofanikisha Mapinduzi 1964

Taariaf iliyotolewa jana na Idara ya Habari-Maelezo, Zanzibar imesema kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein atakabidhi nishani ya Mapinduzi kwa watu na makundi mbalimbali yaliyoshiriki kwa njia tofauti katika kufanikisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar tarehe 12 January, 1964.

Sherehe hizo zitafanyika siku ya Ijumaa tarehe 28/3/2014 saa 10:00 alasiri na Jumamosi tarehe 29/3/2014 saa 9:30 alasiri, katika uwanja wa polisi Ziwani Zanzibar.

Wanachuo mbaroni kwa kuwaweka kinyumba wanafunzi wa Sekondari

Afande Kasusura akimpeleka mtuhumiwa kuonesha mwenzake alipo.
 Jana jioni katika Chuo cha Mwenge mkoani Kilimanjaro, walikamatwa wanachuo wawili kwa tuhuma za kubaka.

Mzazi wa watoto wanaotuhumiwa kubakwa aitwaye "R.B.T." alieleza kuwa siku ya Ijumaa majira ya jioni, binti yake aitwaye "M.B.T" mwenye umri wa miaka 15, mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Maki Sekondari iliyoko Olele huko Marangu Kitowo alitoweka nyumbani kwao huko Huko Marangu Kitowo akiwa na mwenzake aliyetambulika kwa jina la "K.A.M." mwenye umri wa miaka 16 na

Ufafanuzi wa iliyokuwa Tume ya Katiba kwa aliyokosoa Rais Kikwete

Iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, chini ya Jaji Joseph Warioba, imetoa ufafanuzi katika baadhi ya maeneo ya Rasimu ya Katiba yaliyokosolewa na Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge Maalumu la Katiba wiki iliyopita.
 
Taarifa ya Tume hiyo kwa umma wa Watanzania, iliyosambazwa jana kwenye vyombo vya habari, ilisema hatua hiyo ya kutoa ufafanuzi katika baadhi ya maeneo imetokana na kile kinachoelezwa na Tume hiyo kuwa shauku kubwa ya wananchi kutaka ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu Rasimu ya Katiba baada ya hotuba ya Rais Kikwete.
 
Ufafanuzi huo ni huu ufuatao:-