Vivazi vilipevyondezesha uzinduzi wa Zanzibalicious Women Group


Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bi. Mwanaidi Salehe (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Uwezeshaji, Bi. Fatma Gharib Bilal wakati wa sherehe za uzinduzi wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious uliofanyika mwishoni mwa juma ndani ya Zanzibar Ocean View.

Picha zote, maelezo: Zainul Mzige

Pongezi Mama Kamm kwa kutwaa tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka

Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimvisha medali ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014, Dk. Maria Kamm.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimvisha medali ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014, Dk. Maria Kamm.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano Dk. Maria Kamm aliyetwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 ndani ya Ukumbi wa African Dreams uliopo Area D, Dodoma jana usiku.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano Dk. Maria Kamm aliyetwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 ndani ya Ukumbi wa African Dreams uliopo Area D, Dodoma jana usiku.

Taarifa, picha na maelezo kutoka kwa RICHARD BUKOS / GPL, DODOMA -- DK. Maria Kamm ametwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 baada ya kuwapiku wenzake watatu jana usiku.

Dk. Kamm ametwaa tuzo hiyo baada ya kupata asilimia 32.5 ya kura zote zilizopigwa kupitia tovuti ya www.globalpublishers.info pamoja na

Wengine 21 wapoteza uhai ajalini PwaniWatu 21 wamefariki dunia katika ajali mbaya iliyotokea jana saa mbili usiku katika Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani ikihusisha magari 3 na wengine 11 kujeruhiwa.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei, alisema ajali hiyo imetokea katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam-Lindi, eneo la Ikwiriri, wilayani humo.

Awali ajali hiyo ilihusisha magari mawili, Toyota Hiace (T 948 CUX), iliyokuwa ikitokea Ikwiriri kuelekea

PAC yaanza kuchunguza ukwepaji kodi unaofanywa na makampuni ya Kimataifa

Leo tarehe 30 Machi 2014, kamati ya BUNGE ya PAC imeanza rasmi uchunguzi kuhusu ukubwa wa tatizo la ukwepaji kodi na utoroshwaji wa fedha unaofanywa na makampuni ya kimataifa ( multinational corporations). Uchunguzi huu unatokana azimio la umoja wa kamati za PAC za nchi za SADCOPAC lilioamuliwa Arusha, Tanzania mwezi Septemba mwaka 2013 ( Azimio lilisomeka – PACs should initiate investigations on the extent of tax avoidance/evasion and illicit money transfer in their jurisdiction).

Leo PAC imekutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Kitengo cha Fedha Haramu ( FIU) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ajili ya majadiliano ya awali kuhusu

Taarifa ya Tume kuhusu mwenendo wa kampeni Chalinze

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MWENENDO WA KAMPENI KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA CHALINZE


1.0 UTANGULIZI

Ndugu zangu wanahabari, awali ya yote nawashukuru sana kwa kuitikia wito wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Natambua mna majukumu mengi ya kuhabarisha umma, hasa katika kipindi hiki ambacho nchi yetu ipo katika mchakato wa mabadiliko ya katiba na uchaguzi huu mdogo wa Chalinze.

Kwanza nianze kwa kuvipongeza vyama vyote vya siasa ambavyo vimeweka wagombea katika uchaguzi huu. Hivi sasa hapa nchini kuna vyama vya siasa ishirini na moja (21) vyenye usajili wa kudumu na ambavyo kisheria