Kamati ya Nishati na Madini haina mamlaka na $122m za IPTL, BoT

Suala la IPTL na fedha $122m zilizochotwa BoT linachunguzwa na CAG (ukaguzi maalumu) na PCCB (forensic investigation).

Kamati ya PAC iliagiza ukaguzi na uchunguzi huo na itapokea taarifa, kuhoji wahusika na kuwasilisha Taarifa Bungeni kwa maamuzi.

Kamati ya Nishati na Madini haina mamlaka yoyote, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, kushughulika na suala hili mpaka hapo taarifa ya uchunguzi itakapotoka. 

Ni busara ya kawaida kabisa kwamba mkutano kati ya Jukwaa la Wahariri na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini kuhusu suala hili ungesubiri matokeo ya uchunguzi. Inawezekana wizara inalo la kueleza, ikaeleze kwa CAG na PCCB.

--- mwisho wa nukuu ya 'status update' ya Mhe. Zitto Kabwe (via Facebook) ---

Pia jisomee The Citizen: Who is fooling the public on IPTL?

Huduma za dharura kwa wazazi zaokoa maisha Kibiti

Baadhi ya wakina mama wakipatiwa huduma katika kituo cha afya Kibiti leo.

MGANGA Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kibiti, Chagi Jonas Lymo amesema uwepo wa huduma za dharura kwa wajawazito katika kituo hicho cha afya umesaidia kiasi kikubwa katika uokoaji wa maisha ya mama mjamzito pamoja na vifo vya watoto eneo hilo.

Lymo ametoa kauli hiyo leo mjini Kibiti alipokuwa akizungumza na Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe

Waziri Membe azungumza na Gavana wa MarylandTaarifa ya IKULU -- Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Gavana wa Jimbo la Maryland la nchini Marekani, Mhe. Martin O'Malley walipokutana jijini Washington D.C kwa mazungumzo kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Jimbo hilo na Tanzania katika masuala ya uchumi, jamii na siasa.

Mhe. Membe alipata fursa ya kukutana na Gavana huyo alipokuwa mjini humo kwa ajili ya kumwakilisha

Mvua kubwa: Abiria wakwama, Dereva nusura apoteze uhai

Dereva alilazimika kupanda juu ya mti ili kujiokoa asisombwe na mafuriko
Dereva alilazimika kupanda juu ya mti ili kujiokoa asisombwe na mafuriko

Mamia ya wasafiri waliokuwa wakitokea Karatu kuelekea Arusha, Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, wameshindwa kuendelea na safari baada ya kushindwa kuvuka mto Kirurumo uliopo mpakani mwa Wilaya za Karatu na Monduli, baada ya mto huo kufurika na kufunika barabara kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha.

Mwandishi wa habari wa TBC aliyeko Manyara ameripoti kuwa miongoni mwa watu waliokwama ni

[video] Bunge la Katiba: Kamati zawasiisha taarifa; Muungano tata

Na Magreth Kinabo - Dodoma (via Tanzania Government blog)

Baadhi ya Kamati za Bunge Maalum la Katiba leo zimeanza kuwasilisha taarifa zao kuhusu sura ya kwanza na ya sita ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge hilo, mjini Dodoma, huku maoni ya walio wengi wapendekeza Serikali Mbili.

Uwasilishaji wa taarifa hizo ulianza mapema leo asubuhi mara baada ya Mwenyekiti wa Bunge hilo,Samuel Sitta kuanza kikao, ambapo Kamati mbili ndizo zilizopata fursa ya kuwasilisha, kwa mujibu wa muda uliopangwa .Kamati nyingine zitaendelea sasa 10: 00 jioni.

Kamati iliyokuwa ya kwanza kuwasilisha taarifa hiyo ni Kamati Namba Mbili, ambayo Mwenyekiti wake ni Shamsi Vuai Nahodha, ambaye ndiye aliyeiwasilisha katika Bunge hilo.

Akiwasilisha taarifa hiyo, Nahodha aliliarifu Bunge hilo kuwa zipo baadhi ya ibara

TMA WARNING: Heavy rains, strong winds and large ocean waves

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF TRANSPORT
TANZANIA METEOROLOGICAL AGENCY
Telegrams:"METEO"DAR ES SALAAM.

Telephone: 255
(0) 22 2460706-8

Telefax: 255
(0) 22 2460735
P.O. BOX 3056
DAR ES SALAAM.
http//www.meteo.go.tz

Our ref: TMA/1622
10th April, 2014
Information to the Public: Periods of heavy rains at times, strong winds and large ocean waves are expected.
Information No.
201404-01
Time of issue(Hour)
03:30pm
EAT


Category:
Warning
Valid from:
11th

Date
April, 2014

Valid to:
14th
April, 2014
Date


Phenomena/Hazard/Disaster
Periods of heavy rainfall exceeding 50mm in 24hours, strong winds
exceeding 40 km/hr and large ocean waves reaching 2m.Level of Confidence:
Medium: (70%)
Expected Area :
Unguja and Pemba isles, Dar es Salaam, Pwani and Tanga regions, with
possibility of spreading towards Lindi, Mtwara and Morogoro regions.
This is due to the enhancement of the Inter-tropical convergence zone
Text:
(ITCZ) associated with atmospheric easterly waves propagating from east

towards and over the areas mentioned above.


Advisory:
Residents of high risk areas, Ocean users and Disaster Management

Authorities are advised to take necessary precautions.
Remarks:
TMA will continue to monitor the situation and issue updates when

necessary.
Issued by
Tanzania Meteorological Agency.

Picha za Waziri Membe akipokea tuzo kwa niaba ya Rais Kikwete

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, akimsikiliza mwendesha shughuli Lady Kate Atabalong Ndi, Kamishna Masuala ya Afrika wa Gavana wa jimbo la Maryland nchini marekani kabla ya kupokea Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa Jumatano, Aprili 9, 2014. Kushoto ni Naibu Spika Mhe Job Ndugai ambaye yuko katika ziara ya kikazi nchini Marekani, ambapo alialikwa kuhudhuria hafla hiyo. Nyuma yake ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula. 

Picha ya juu na zinazofuata hapa chini pamoja na maelezo, zinaka IKULU.

Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii

Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii (CISNA) wakiendelea na Mkutano huo uliofunguliwa rasmi jana April 10, 2014 na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Peter Ilomo (katikati mwenye tai nyekundu).

Na Mwandishi wetu — MKURUGENZI wa Mfuko unaosimamia mifuko ya hifadhi za Jamii nchini (SSRA) , Irene Isaka ametoa wito kwa wanachama wapya kujiunga kwa wingi kwenye mifuko hiyo kwa sababu muda si mrefu serikali itaweka uwiano wa mafao sawa kwa mifuko yote.

Isaka alisema hayo jana katika mkutano wa 32 ambao unazikutanisha nchi wanachama wa SADC unaendelea jijini Dar es Salam.

“ Tukiwa katika mkutano huu tunaweza kujifunza mambo mengi kutoka kwa wenzetu wa SADC huku na

WHO recommends drugs costing up to $84,000 a course for Hepatitis C treatment

Authors of the first-ever global guidelines for treating hepatitis C went big Tuesday, advocating for worldwide use of two of the most expensive specialty drugs in the world.

The new guidelines from the World Health Organization give strong endorsement to the two newest drugs. Gilead Science's Sovaldi costs $1,000 per pill, or $84,000 for a 12-week course of treatment, and Olysio, Janssen Pharmaceutical's drug, gosts $66,360 for its three-month course.

The high prices have ignited a firestorm of objection. In the United States, doctors and insurers worry that the cost of the drugs will make their widespread use impossible. And critics say even if the prices are heavily discounted in other countries, the drugs will still be unaffordable in most of the world. ... click here to continue reading

Now this is odd enough! A 9-month-old boy charged with attempted murder in Pakistan?


via The NPR -- A 9-month-old Pakistani boy has been charged along with the rest of his family with attempted murder, according to reports.

Musa Khan was photographed last week crying as his grandfather held him for fingerprinting. He was with his family during a protest in a Lahore slum that turned violent in February. Police say the boy, who was

Efatha yapinga kunyang‘anywa shamba na kuhoji, wamekoma lini kuwa Watanzania?

Bodi ya wadhamini ya huduma ya Efatha, ambao ni wamiliki wa shamba la Efatha, imemjibu katibu mkuu wa CCM, Abdulrahamn Kinana kutokana na kauli yake kuwa atahakikisha Serikali inanyang’anya shamba hilo na kulirejesha kwa wananchi.

Katika taarifa yake kwa umma, bodi hiyo imesema mbali na kuwa hawakubaliani na uamuzi huo, wanahoji kama mpango ni kuwapa wananchi shamba hilo, ni lini wao (Efatha) wamekoma kuwa wananchi wa Tanzania.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa baadhi ya waumini wa Efatha ni wanachama wa CCM na wengine ni

Tanzania at risk of losing embassy property in Kenya

Tanzania is embroiled in a case in which it risks losing one of its properties in Nairobi over a Ksh42 million ($484,533) debt.

The case is traceable to January 31, 2000 when the High Court of Zanzibar ordered that Kenyan businessman J. S. Kinyanjui and Lamshore Ltd be paid $484,533 for supplying rice to the Isles government.

The businessman moved to the Kenyan High Court and sought the execution of the judgment delivered 14 years ago after he was unable to get the money in Zanzibar.

Mr Kinyanjui filed an application for orders to attach and sell a piece of land belonging to the United Republic of Tanzania in a prime area of Nairobi as a way of recovering the money he was awarded.

Alarmed by the move and the possibility of the plot located in Upper Hill area being auctioned off, the Tanzanian government has asked to be joined in the case, arguing that, as owner of the property targeted for the requested auction, it is directly affected and should be part of the case. click here to continue reading.

Kitchen Party Gala @Kilimani Hall, Dodoma

Taarifa ya CCM juu ya kauli ya Lembeli “CCM SIYO MAMA YANGU”

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAREHE 07.04.2014

CCM MKOA WA SHINYANGA YA LAANI KAULI YA MBUNGE WA JIMBO LA KAHAMA JAMES LEMBELI KUWA “CCM SIYO MAMA YANGU”

Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga KIMELAANI vikali kauli ya Mbunge James Lembeli Mbunge wa Jimbo la Kahama aliyoitoa kwenye vyombo ya habari hivi karibuni iliyosema “CCM SIYO MAMA YANGU”.
Kwa hiyo Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga na wana CCM wote kwa ujumla wamestushwa na kauli ya Mbunge Lembeli anayetokana na CCM kwani kauli hii hatukutegemea sote kama ingeweza kutolewa na Mwanachama ambaye tena ni Kiongozi ndani ya Chama.

Tunaomba ieleweke na tunautaarifu Umma na wana CCM wote kuwa CCM haina tatizo kabisa na msimamo wa Mbunge James Lembeli kuhusu msimamo wake wa serikali moja, mbili, tatu au nne na hata serikali ya Tanganyika kwani huo ni uhuru wake binafsi. Tatizo letu kubwa kwake ni kauli aliyoitoa kuwa “CCM SIYO MAMA YANGU” kwani kauli hiyo ameitoa sio mahali pake na haihusiki na utashi wake binafsi katika msimamo alionao katika BUNGE LA KATIBA. Kauli hii inaukakasi na ni sawa na kukinajisi Chama.Lakini jambo la ajabu na la kushangaza ni kuhusu kulitumia jina la Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere vibaya, amekuwa akijifananisha na kauli ya Baba wa Taifa tungependa atambue kuwa Lembeli hana hadhi na sifa ya kujifananisha na Baba wa Taifa; kwani kujifafanisha kwake na Baba wa Taifa huko ni matumizi mabaya ya kujitwisha sifa asizostahiki kwani Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere alikuwa na karama, hekima na busara kubwa za pekee na aliheshimika Dunia kote pia alikuwa anatoa kauli zake kutokana na mazingira yaliyokuwepo wakati huo.

Kwani Baba wa Taifa kila jambo lililokuwa linahusu swala la Chama na Mstakabali wa Taifa alitumia vikao kulizungumza sio anavyofanya Lembeli kuropoka ovyo, kutumia ubabe na kukosa staha kwa Chama.
Tabia ya Mbunge Lembeli ya kukidhihaki Chama imekuwa ikijitokeza mara kwa mara, lakini tunapenda atambue na kumkumbusha kuwa Lembeli hapo alipofika na jeuri yote na umaarufu alionao unatokana na CCM, kabla ya mwaka 2005 hakuna Mtanzania aliyemfahamu popote nchini.

Lakini baada ya kupewa ridhaa na CCM na hatimaye kuchaguliwa Ubunge ndipo akajenga umaarufu uliotokana na CCM. Lakini jingine tunapenda kumkumbusha kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Lembeli alikuwa na wakati mgumu sana ndani ya Chama na nje ya Chama lakini Chama na Wanachama wakampigania kwa hali ya juu sana na kwa mazingira magumu na hatimaye ushindi ukapatikana.

Leo shukrani anazotoa kwa Chama ni kukiambia CCM SIO MAMA YAKE.

Basi na kama Lembeli anaona CCM SIO MAMA YAKE ni vyema akatueleza MAMA YAKE NI NANI – KISIASA na kama ana MAMA MWINGINE KISIASA ni VYEMA AKAMFUATA HUYO MAMA HUKO ALIKO anayeona atamfaa kumpa umaarufu zaidi ya CCM.

Mwisho CCM Mkoa wa Shinyanga hakitakuwa tayari na hakitawavumilia wanachama na viongozi wake wenye tabia kama ya Lembeli ya kuendelea kukidhalilisha Chama hadharani.

Lakini pia Chama kitaendelea kuheshimu Demokrasia ndani ya Chama na Uhuru wa mawazo unaofuata maadili, miiko na taratibu za Chama ndani ya vikao.

Asanteni kwa kunisikiliza.

Taarifa hii imeandaliwa na Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga na imesomwa na:-

Ndugu Emmanuel S. Mlimandago
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM
Mkoa wa Shinyanga

From South Africa to Niger, The Innovation Prize for Africa 2014 Finalists are


From the World’s First Injectable Skeleton Regeneration Protein to a Domestic Waste Biogas System, Ten Africans Are Innovating the Future of the Continent

JOHANNESBURG, South-Africa, April 10, 2014/ -- The African Innovation Foundation (AIF) (http://www.africaninnovation.org) announced the finalists of the prestigious Innovation Prize for Africa (IPA) 2014 (http://www.innovationprizeforafrica.org). Ten African innovators have created practical solutions to some of the continent’s most intractable problems, from a domestic waste biogas system to a

Jhikoman & Afrikabisa Band kuanza Europe Tour


  • Kufunika katika maonyesho Makubwa barani ulaya yakiwemo ya Ujerumani, Finaland, Norway
Mwanamuziki mwashuhuri wa Reggae Afrika mashariki Jhikoman kutoka Bagamoyo Tanzania, anatarajiwa kuondoka nchini katikati ya mwezi huu April 2014 kuanza ziara ya miezi mitatu barani Ulaya, ambapo atatumbuiza katika maonyesho makubwa ya Kimataifa huko ughaibuni.

Baadhi ya festivals zitakazofunikwa na mwanamuziki huyo ni Helsink Film Festival nchini Finland na

Mjengwa na Katiba Mpya: Nimeitafak​ari sana njia ya Kikwete

Rais Kikwete

Ndugu zangu,

Naziona ishara za kuendelea kwa mvumo mbaya wa upepo wa kisiasa na hususan inapohusu hoja ya Muungano na muundo wa Serikali.

Mjadala unaoendelea sasa ni kama vile umefunikwa kwa chandarua kisicho na kinga ya wadudu wenye madhara kama mbu.

Tunakoelekea si kuzuri. Msimamo wangu uko wazi, kuwa tunahitaji muundo wa Serikali Tatu ili tuimarishe