[video] Tundu Lissu akizungumza kabla ya matangazo kukata ghafla TBC

Official video song "Nasimama" by Lady JayDee


Mkurugenzi Tanzania Women's Bank azungumza na wakina Mama DMV

Ms Margareth Chacha Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Women's Bank akiongea na akina mama DMV siku ya Ijumaa April 11, 2014 na kuwapa faida ya kufungua akaunti na Benki hiyo.
Bi. Margareth Chacha, Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Women's Bank

Bi. Margareth Chacha, Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Women's Bank alizungumza na akina mama DMV siku ya Ijumaa, Aprili 11, 2014 na kuwapa faida ya kufungua akaunti na Benki hiyo.

Mojawapo ya faida hizo ni masharti nafuu ya mikopo. Alieleza kuwa kwenye Mabenki mengine inakuwa vigumu kwa wanawake kupata mikopo akitolea mfano wa sharti mojawapo ambalo ni kuwa na nyumba. Kwa uzoefu

[video, text] Bunge la Katiba: Ripoti iliyowasilishwa na Dk Kigwangala ya Wajumbe walio wengi wa Kamati Namba Nne

TAARIFA YA KAMATI NA. 4 YA BUNGE MAALUM KUHUSU SURA YA KWANZA NA SURA YA SITA YA RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


________________________


UTANGULIZI

Mheshimiwa Mwenyekiti, 
kwa mujibu wa Kanuni ya 32 ya Kanuni za Bunge Maalum za Mwaka 2014, Kamati Namba 4 ilipokea kutoka kwako Sura ya Kwanza na Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuzijadili na kutoa mapendekezo. Kamati yangu ilipokea Sura hizo mnamo tarehe 31 Mwezi wa Machi, 2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti,

kwa muda wa siku mbili, yaani tarehe 1 na 2 Aprili, 2014, katika ukumbi Na. 135 uliopo katika jengo la Hazina, Dodoma, kamati yangu ilizijadili na kuzipigia kura Ibara zote 19 zilizopo kwenye Sura zilizotajwa, kati ya tarehe 3 na tarehe 4 Aprili, 2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuzijadili Sura mbili ulizozileta kwetu, Kamati ilizijadili kwa kuchambua Ibara moja hadi nyingine. Hatimaye, Kamati imeandaa taarifa ambayo inazingatia maoni ya Wajumbe walio wengi na maoni ya Wajumbe walio wachache. Hivyo basi, naomba kuwasilisha taarifa hii kwa mujibu wa kanuni ya 62 (1) ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, 2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha 26 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, sura ya 83 kikisomwa pamoja na Kanuni ya 64 (1) ya Kanuni za Bunge Maalum za mwaka 2014, zimeainisha utaratibu wa kufikia maamuzi katika mijadala ya Kamati. Hivyo basi, Kamati imezingatia matakwa haya ya sheria na Kanuni katika maamuzi yake kama itakavyoonyeshwa katiba kila ibara.

2.0 YALIYOJITOKEZA KWENYE MAJADILIANO

Maoni ya Wajumbe Walio Wengi

Maoni kwa Ujumla na Sababu za Kupendekeza Marekebesho
Video za mwendelezo zimepachikwa hapo chini...

CRDB yachangia Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa sherehe za Muungano


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB Bwn. Martin Mmari akimkabidhi Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula kitita cha dola 5,000 katika kikao cha makabidhiano kilichofanyika Ubalozi wa Tanzania siku ya ijumaa April 11, 2014.

Lissu kuendelea Jumatatu alikokomea leo baada ya TBC kukata ghafla

Wananchi katika moja ya mskani ya Kikwajuni Weles (Zanzibar).  wakifuatilia mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba Tanzania kupitia Kituo cha Television ya Taifa TBC, kikiripoti moja kwa moja kutoka Dodoma wakati Mhe Tundu Lissu alipokuwa akizungumza. (picha: ZanziNews.com)  

Kupitia blogu yake,  Mjumbe wa Bunge la Katiba, Salma Said ametoa ufafanuzi wa kilichotokea leo Bungeni na mustakabali wake kama ifuatavyo:

Ni kweli hali ya hewa leo katika Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea Dodoma ilichafuka ghafla na kusababisha kelele na manunguniko kutoka kwa wajumbe wakilalamikia kukatika kwa matangazo ambapo matangazo yanayorushwa moja kwa moja (Live) na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kutoka Bungeni Dodoma yalikatika kulikotokana na sababu za kiufundi.

Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta amelazimika kuakhirisha kikao hadi Jumatatu ambapo kabla ya kusikilizwa taarifa za kamati nyengine mbili zilizobaki itabidi Mjumbe wa Bunge hilo Tundu Lissu aendelee kutoa

Bunge la Katiba: Maoni yaliyowasilishwa na Tundu Lissu kabla ya matangazo TBC kukatika ya Wajumbe walio wachache wa Kamati na. 4

MAONI YA WAJUMBE WALIO WA WACHACHE KATIKA KAMATI NAMBA NNE KUHUSU SURA YA KWANZA NA SURA YA SITA YA RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA [Kanuni ya 32(4) ya Kanuni za Bunge Maalum, 2014]


UTANGULIZI
Mheshimiwa Mwenyekiti,


Sura ya Kwanza na Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (‘Rasimu’) ndizo msingi ambao Rasimu yote imejengwa juu yao. Wakati Sura ya Kwanza inagusa suala la muundo wa Muungano katika ibara moja tu kati ya ibara tisa, Sura yote ya Sita inahusu ‘Muundo wa Jamhuri ya Muungano.’ Suala la Muungano na hasa Muundo wake limetawala mjadala wa kisiasa na kikatiba wa Tanzania kwa zaidi ya miaka thelathini. Ndio maana katika waraka wake wa siri kwa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (‘CCM’), Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya chama hicho imetamka kwamba “muundo wa Muungano ndiyo moyo wa Rasimu na ndiyo unaoamua ibara nyingine zikae vipi.”


Suala hili pia limetawala mchakato wa Katiba Mpya tangu ulipoanza miaka mitatu iliyopita. Kama alivyosema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Joseph Sinde Warioba wakati wa kuwasilisha

[photo, video update] Dar es Salaam lilivyojaa maji!

Kwa maelezo na maelekezo ya namna ya kutoa msaada kwa waathirika wa marufiko ya mvua Dar es Salaam, tafadhali fuatilia/wasiliana na Tanganyikan (via Twitter)
Video ya wakazi wa Jangwani walivyohamia kwenye vituo vya mabasi yaendayo haraka kwa ajili ya kujihifadhi na picha zaidi za maeneo mbalimbali yalivyojaa maji, zimepachikwa hapo chini...