Taarifa ya Ikulu kuhusu Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue akionesha Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mbele ya Waandishiwa habari na Wapiga picha, Aprili 14, 2014, hati ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge Maalum la Katiba siku chache zijazo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Ombeni Sefue akionesha Hati halisi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mbele ya Waandishiwa habari na Wapiga picha huko Ikulu leo Aprili 14, 2014, hati ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge Maalum la Katiba siku chache zijazo.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              [email protected]             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO LA KATIBU MKUU KIONGOZI KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU HATI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR
IKULU, DAR ES SALAAM, TAREHE 14 APRILI, 2014
__________________________________________________

            Siku 12 zijazo tutasherehekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wamezaliwa watu ndani ya Muungano huu na wengine wana wajukuu.

            Inasikitisha sana kuwa leo, miaka 50 baadaye ipo dhana potofu inayojengwa kuwa Muungano huu si halali kwa vile hakuna Hati ya Muungano (Articles of the Union).

            Waasisi wa Taifa letu ambao tarehe 22 Aprili, 1964 kule Zanzibar walitia saini Hati hiyo, mbele ya

Picha za maafa huko Kamachumu


Picha zaidi zimepachikwa hapo chini...

Fundraising Solution & General Enterprises: Tunatoa huduma ya "fundraising"

  • Wewe ni mjasiriamali? Unahitaji fedha kwa ajili ya kupanua huduma yako?
  • Wewe ni mfanyabiashara au mmiliki wa kampuni? Unahitaji fedha kwa ajili ya kukuza mtaji wako na kupanua biashara yako?
  • Wewe ni Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali? Unahitaji fedha kwa ajili ya kuendesha miradi na program mbalimbali?
  • Wewe ni mtayarishaji wa filamu au kiongozi wa kundi la maigizo ? Unataka kutayarisha filamu au tamthiliya lakini unashindwa kwa sababu ya ukosefu wa fedha za gharama za utayarishaji?

Kama jibu ni ndio basi hii ni habari njema sana kwako. 

FUNDRAISING SOLUTION & General Enterprises ni kampuni inayo jihusisha na

[video] Bunge la Katiba: Ripoti iliyowasilishwa na Mbowe ya Wajumbe walio wachache wa Kamati Namba Saba

[video] Bomu lililolipuka Arusha Night Park Bar

Ulinzi kaitka eneo la baa palikotokea mlipuko (picha: Arusha255 blog)

Jana Jumapili, Aprili 13, 2014 ulitokea mlipuko wa kinachodhaniwa kuwa bomu la kurushwa kwa mkono katika baa maarufu kwa maonesho ya mechi za mpira wa miguu wa Ulaya, ijulikananyo kama Arusha Night Park au Matako baa iliyopo maeneo ya Mianzini, mkoani Arusha na kujeruhi zaidi ya watu 20 wengi wao wakiwa wateja waliojazana kushuhudia mechi za soka.

Majeruhi walikimbizwa hospitali za Mt Meru na Dr Mohamed kwa matibabu ya

Hati ya Muungano wa Tanzania kuwasilishwa Bungeni

Mwenyekiti wa Kamati namba sita wa Bunge Maalum la Katiba Stephen Wassira akiwasilisha maoni ya Kamati yake leo mjini Dodoma kwenye kikao cha ishirini na mbili cha Bunge hilo.
Mwenyekiti wa Kamati namba sita wa Bunge Maalum la Katiba Stephen Wassira akiwasilisha maoni ya Kamati yake leo mjini Dodoma kwenye kikao cha ishirini na mbili cha Bunge hilo.

Na Magreth Kinabo, Dodoma via Tanzania Government Blog -- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Utaribu, Stephen Wassira amesema Serikali itawasilisha Hati ya Makubaliano ya Muungano katika Bunge Maalumu la Katiba baada ya siku mbili zijazo.

Wassira ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Namba Sita ya Bunge hilo ambazo zilikuwa zikijadili Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Katiba, alitoa kauli hiyo leo baada ya kuzuka mjadala juu ya uwepo wa hati hiyo na kama ipo kwa nini haijawasilishwa kwa wajumbe wa Bunge hilo.

Babu na Mjukuu waingia hatua ya tatu ya shindano la Tanzania Movie TalentsWashiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni babu na mjukuu wake kiuhalisia wakipongezana mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu ya kutafuta washiriki 15 bora na hatimaye kupatikana washindi watatu bora wa kanda ya kati ambapo kila mmoja ataondoka na kitita cha shilingi laki tano za Kitanzania.

Na Josephat Lukaza/Proin Promotions Limited - Dodoma

Leo Shindano la Tanzania Movie Talents limeingia ya hatua ya pili ya mchujo ambapo washiriki 30 wameweza kupatikana kwaajili ya kuendelea na shindano hilo hapo kesho ambapo washiriki 15 ndio watachukuliwa kwaajili ya kuendelea na mashindano hayo na hatimaye kupatika washindi watatu bora ambao

Burudani katika sikukuu ya Pasaka @ DarLive

Doris Mollel-Miss Ilala 2013 aikabidhi Shule ya Msingi Pugu vitabu 50

Miss Ilala 2013, Doris Mollel, akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembea shule hiyo ya msingi Pugu jijini Dar es Salaam.
Miss Ilala 2013, Doris Mollel, akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembea shule hiyo ya msingi Pugu jijini Dar es Salaam.

Miss Ilala 2013, Doris Mollel ijumaa ya wiki iliyopita alitembelea shule ya msingi Pugu jijini Dar es Salaam na kukabidhi vitabu 50 za hadithi kwa wanafunzi wa shule hiyo katika harakati zake binafsi za kuwajengea wanafunzi na watoto utamaduni na

Vodacom yaipongeza Azam FC kwa kuwa mabingwa VPL

Mbeya 14, Aprili 2014 --  Mdhamini Mkuu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, wameipongeza timu ya Azam FC kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2013/2014 ikiwa ni Mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake miaka 7 iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Mbeya City na Azam FC kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya sokoine mjini Mbeya Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampumi hiyo, Salum Mwalim amesema wakiwa

[video, text] Bunge la Katiba: Ripoti iliyowasilishwa na Jussa ya Wajumbe walio wachache wa Kamati Namba Sita


MAONI YA WAJUMBE WALIO WACHACHE WA KAMATI NAMBA SITA YA BUNGE MAALUM LA KATIBA KUHUSIANA NA SURA YA KWANZA NA SURA YA SITA ZA RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


(Kwa mujibu wa Kanuni 32 (4) ya Kanuni za Bunge Maalum za Mwaka 2014)

UTANGULIZI

Sura ya Kwanza na Sura ya Sita za Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndizo msingi ambao Rasimu yote imejengwa juu yao. Hii ni kwa sababu Sura hizi mbili zinazungumzia mfumo na muundo wa Muungano. Katika Sura ya Kwanza, mfumo na muundo wa Muungano unatajwa kwenye Ibara ya 1 na Ibara ya 2 na kwa upande wa Sura ya Sita, sura nzima inahusu Muundo wa Jamhuri ya Muungano.

Katika kufikia maamuzi ya Kamati Namba Sita, wajumbe waligawanyika, na katika Ibara ya 1 na ya 3 ya Sura ya Kwanza na Ibara zote za Sura ya Sita, sharti la kupata theluthi mbili za wajumbe wote wa kamati kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili za wajumbe wote wa Kamati kutoka Zanzibar lilishindwa kufikiwa.

Gari dogo laangukiwa na lori lenye mchanga Makongo


Picha za ajali iliyotokea asubuhi ya leo huko Makongo jijini Dar es Salaam ambapo lori lililokuwa limebeba mchanga lililiangukia gari dogo.

Juhudi za Askari wa Jeshi la Wananchi wakishirikiana na kikosi cha zimamoto na uokoaji zilifanikisha kumnasua kutoka kwenye mchanga dereva wa gari dogo mendo wa

CNN interviews Tanzania's Finance Minister on Investment, Entrepreneurship

Hon. Saada Mkuya Salum, Minister for Finance during the interview with CNN International's Producer Brian MacBride
Hon. Saada Mkuya Salum, Minister for Finance during the interview with CNN International's Producer Brian MacBride

Hon. Saada Mkuya Salum, Tanzania's Minister for Finance. engages with CNN International on the role that the Government is playing in creating an environment that is conducive for investment in support of Small and Medium Enterprises (SME's) and Start Ups. 

Central to the interview held at the Tanzania embassy in Washington DC in the US, was CNN's quest to know how Tanzania differentiates itself from other African countries in terms of fostering entrepreneurship and facilitating investment in

Mkuu wa Kituo cha Polisi awagonga kwa gari raia watatu

Majeruhi wa awali Joseph Malugu akiwa hospitali ya wilaya ya Kahama baada ya kuumia vibaya mguu wake na sehemu nyingine za mwili.
via gazeti la MAJIRA -- Watu watatu wamejeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, Bw. Elia Haway. 

Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ambapo tukio hilo limetokea juzi, katika barabara iendayo Isaka, eneo la Nyasubi. 

Mkuu huyo wa kituo alikuwa akiendesha gari lenye namba T 798 BSK, aina ya

IPTL and PAP sue Standard Chartered Bank (HK) over ‘fraud’

The Independent Power Tanzania Limited (IPTL) and Pan African Power Solution Limited (PAP) have filed a suit at the High Court in Dar es Salaam, demanding 3,240,000,000 US dollars (about 5.3tri/-) from Standard Chartered Bank (Hong Kong) Limited (SCBH) over an alleged fraud.

It is alleged in the suit filed last week that SCBH had been falsely representing being a creditor of IPTL and procured a decision before a London Court in February this year for, among others orders, recalculation of tariffs payable by Tanzania Electric Supply Company (Tanesco).

The two plaintiffs, IPTL and PAP, through the legal services of Bulwark Associates Advocates and ASYLA Attorneys, have also sued and added a Tanzanian advocate, Martha Kaveni Renju, as the second defendant for allegedly presenting herself as IPTL administrator-receiver.

Furthermore, the plaintiffs have joined Tanesco in the suit for the purpose of preventing the state owned company from enforcing the decision issued by the London Court, the International Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID). Click here to read more.