Taarifa ya kusitishwa mkutano wa hadhara Zanzibar

Nakala ya barua ya kutisishwa kwa mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika Zanzibar kesho ukiongozwa na viongozi wa UKAWA ambayo unaweza kuiona kwa kubofya hapa, inasomeka ifuatavyo:-

YAH: TAARIFA YA KUSITISHWA MKUTANO WA HADHARA


Naomba urejee barua yangu Kumbu. Nam. W/MGH/SO/7/2/A/4 ya tarehe 17 Aprili, 2014 inahusika.

Ninakujulisha rasmi kuwa mkutano huo uliokuwa ufanyika kesho tarehe 19 Aprili, 2014 hapo Viwanja ya Demokrasia Kibanda Maiti umesitishwa kwa sababu za

Wanaume TMK, Tip Top Connections kupamba mechi za Simba vs Yanga na Azam vs JKT Ruvu

Makundi mawili maarufu ya muziki wa kizazi kipya nchini TMK family na Tip Top Connections wanatarajiwa kupamba mechi za ligi kuu Vodacom ya Simba na Yanga na ile ya Azam FC dhidi ya JKT Ruvu inayochezwa kesho Jumamosi jijini dar es salaam.

Uwepo wa burudani hizo ni sehemu ya mkakati wa mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom ya kuhitimisha msimu wa ligi wa 2013/2014 kwa kishindo na burudani ya aina yake.

Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim amesema kundi la Tip Top Connections likinogeshwa na msanii mahiri Ma D litaipamba mechi ya watani wa

[audio] Wizara yasitisha malipo ya Wajumbe wa Bunge la Katiba

Wizara ya Fedha kupitia Naibu Waziri wa Fedha (Sera), Mhe. Mwigulu Nchemba (aneyekaimu nafasi ya Waziri wa Fedha aliyeko safarini tangu Aprili 10, 2014) imetangaza uamuzi wa kufuta malipo ya Wabunge waliosusia vikao vya Bunge la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma.

Uamuzi huu umetangazwa ikiwa ni siku ya pili tangu Wajumbe wanaounda Umoja wa Bunge la Katiba (UKAWA) ili wasusie shughuli za Bunge hilo kwa madai ya kuchoshwa na matusi, kejeli na vitisho vinavyoendelea katika vikao hivyo.

Nchemba ameziagiza Benki zote kurudisha cheki malipo ya posho na "sitting allowance" ambazo zilipelekwa Bungeni mnamo Aprili 16, 2014 ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wajumbe hao ikiwa ni malipo ya mpaka Aprili 30, 2014.

Kwa ufafanuzi zaidi, bofya kitufe cha pleya iliyopachikwa hapo chini...

UPDATED w/ video [audio] Lukuvi arejea, akariri na kufafanua kauli yake iliyowakera UKAWA

Waziri William Lukuvi akifafanua kauli yake na kuchangia hoja katika Bunge la Katiba, Aprili 17, 2014. 
(picha: PT blog)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, amerejea na kukariri kauli yake aliyoitoa katika Kanisa la Methodist huko Dodoma akifafanua kuwa ana haki ya kuwa na hofu na si makosa raia yeote wa Tanzania kuhofia majeshi ya ulinzi kuchukua nchi ikiwa muundo wa Muungano wa serikali mbili ukibadilishwa na kuwa serikali tatu.

Aidha, amesema pia anahofu kuhusu mwenendo wa CUF unaoshirikiana kisiasa na Taasisi ya kidini ya al maaruf, Uamsho, inayotekeleza majukumu yake Zanzibar kwamba umelenga kuua Muungano na kuhatarisha amani kwa mgongo wa dini ya Kiislamu. Kauli hiyo ndiyo iliyodaiwa na UKAWA (Umoja wa

Taarifa ya Jeshi la Polisi kuelekea Sikukuu ya Pasaka

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tunapoelekea kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Polisi nchini, linatoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini katika suala la usalama wa maisha na mali zao. Uzoefu unaonyesha kwamba, katika kipindi kama hiki cha sikukuu kuna baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi katika mikoa yote limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza na endapo vitajitokeza viweze kudhibitiwa kwa haraka.Aidha, ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote, yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na

Kesho UKAWA watafanya mkutano wa hadhara Zanzibar

Kesho, Jumamosi Aprili 19, 2014 Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wamepanga kufanya mkutano wa hadhara Zanzibar kwa malengo ya kuongea na wananchi juu ya msimano wao wa kususia vikao vya Bunge.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini Dodoma, mwakilishi wa kundi hilo Profesa Ibrahim Lipumba alisema kuwa katika kikao chao wamekubaliana kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara kwa

Taarifa ya mabadiliko ya uelekeo wa barabara Dar es Salaam

MABADILIKO YA UELEKEO WA BARABARA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZIA SIKU YA TAREHE 28/04/2014. (TRAFFIC CIRCULATION AT CBD)Ufunguo wa ramani iliyopachikwa hapo juu:-
  1. RANGI YA NJANO - Njia ya uelekeo mmoja (One Way)
  2. RANGI YA BLUE MPAUKO - Njia ya mielekeo miwili (Two Way)
  3. RANGI YA KIJANI - Mitaa ya kutembea kwa miguu, magari marufuku (Walking streets)
  4. RANGI NYEKUNDU - Barabara za kupita daladala
  5. RANGI YA BLUU ILIYOIVA - Barabara za DART
  6. DUARA ZA NJANO - Mzunguuko (Round-about)
  7. MSALABA WA KIJANI - Makutano yenye taa za kuongozea Magari (Signalized intersection)

1. Kipande cha Mtaa wa Samora kuanzia Mnara wa Askari (Askari Monument) hadi Clock Tower. Magari kutakuwa na mabadiliko ambayo magari yatakuwa yanaelekea Clock Tower badala ya Askari Monument.

2. Barabara ya Sokoine kuanzia Station hadi makutano ya Mtaa wa Maktaba, Posta ya Zamani, magari

Rais Kikwete: "Ni kukosa adabu, Tuwaache walivyo, Dunia itawafundisha"TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ni ukosefu wa adabu kuwatukana waasisi wa Tanzania - JK

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu kuwa baadhi ya Watanzania kuwatukana, kuwadhihaki na kuwakejeli Waanzilishi ma Taifa la Tanzania, Hayati Julius Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amaan Karume.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa viongozi hao wawili wameifanyia Tanzania mambo mengi, mambo makubwa na mambo ya kihistoria kiasi cha kwamba Watanzania wanao wajibu wa kudumisha na

Serikali yataka gazeti la Mawio kujieleza kuhusu Hati ya Muungano

Mkurugenzi wa Idara ya Habari ambaye pia ni Msemaji wa Serikali akionesha gazeti lenye taarifa inayopaswa kutolewa maelezo, iliyochapishwa na gazeti la Mawio (picha: MAELEZO).

Serikali imeagiza gazeti la Mawio kueleza sababu za kupotosha na kukejeli nia njema ya serikali kwa wananchi wake kuhusu Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Akizungumza jana, Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema gazeti hilo la wiki linatakiwa kujieleza ndani ya siku tatu. Alisema mbali na kujieleza, gazeti hilo limepewa siku saba hadi