Maandalizi Ya Ukumbi Itakapofanyika Kili Music Awards

Siku ya Jumamosi Mei 3 itakuwa kilele cha tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014 kwa kuwatuza wasanii, vikundi, watunzi na wandaaji muziki waliofanya vizuri mwaka 2013. Haya ni maandalizi ya mwisho katika ukumbi wa Mlimani City.

Sound check ya Live Band


Mfanyakazi afariki kiwanjani kwenye maadhimisho Mei Mosi, Dar

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kashikana mikono na viongozi wa serikali na wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) huku wakiimba wimbo wa wafanyakazi katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) leo Mei 1, 2014 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (picha: IKULU)


  • Rais Kikwete aongoza maadhimisho ya Mei Mosi 
  • Aahidi mishahara kupanda, P.A.Y.E kushuka
  • Mfanyakazi wa Ikulu apoteza uhai kiwanjani

Habari kwa mujibu wa Lukwangule blog zinasema kuwa Rais Jakaya Kikwete, amewaahidi wafanyakazi nchini kuwa mambo mazuri yakiwemo ya kupanda kwa mishahara na kupunguzwa kwa kodi ya mishahara maarufu kama P.A.Y.E.

Akihutubia kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Dar es Salaam leo, Rais Kikwete amesema:

[video] Mkutano wa UKAWA katika viwanja vya Kibanda Maiti, Unguja, Zanzibar

Iliyopachikwa hapo ni playlist yenye video tano za mkutano wa UKAWA uliofanyika siku ya Jumatano, Aprili 30, 2014 katika viwanja vya Kibanda Maiti mjini Unguja, Zanzibar.

 

Shukurani ya video iende kwa "KAMATI YA MARIDHIANO"

Wajawazito walalamikia ‘rushwa’ katika kituo cha afya Simambwe

Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Simambwe, Salome Mwaipopo (kulia) akizungumza na mwandishi wa habari hii. Kushoto ni mmoja wa manesi wa kituo

BAADHI ya akinamama na wanakijiji wa baadhi ya vijiji vya Kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya Vijijini wamewalalamikia wauguzi na wahudumu wa afya katika Kituo cha Afya Simambwe kwa kile baadhi yao kuwaomba kitu kidogo (rushwa) hasa kwa wajawazito wanapofika katika kituo hicho kupata huduma.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wanawake kutoka vijiji vinavyohudumiwa na kituo hicho vya Usoha Njiapanda, Shibolya, Simambwe, Garijembe, Ilembo Usafwa, Ngoha na Zunya walisema mjamzito

Wasichana 6,000 Mtwara wapatiwa elimu na vifaa vya afya

      t-marc logo 1         Description: vodafoundation logo.jpg                        


MRADI WA HAKUNA WASICHOWEZA WATOA ELIMU NA MISAADA YA VIFAA VYA KUJISITIRI WAKATI WA HEDHI KWA WASICHANA 6000 MKOANI MTWARA.
________________________________________________

Wasichana wa mkoani Mtwara wamefaidika na elimu ya afya pamoja na vifaa vitakavyowasaidia kujisitiri wakati wa hedhi. Elimu hii na msaada vimetolewa kupitia mradi wa Hakuna Wasichoweza unaotekelezwa na asasi ya T-MARC Tanzania.

Mradi wa Hakuna Wasichoweza unaendeshwa na asasi ya T-MARC Tanzania kwa ufadhili wa watu wa