Pres. Kikwete meets former British PM Gordon Brown; Mark Suzman of The Gates Foundation; Sunil Mittal CEO of Bharti Airtel in Abuja

President Jakaya Mrisho Kikwete in a bilateral meeting with Rt. Hon. Gordon Brown (MP), UN Special Envoy for Global Education and Former British Prime Minister in the sidelines of the World Economic Forum on Africa in Abuja, Nigeria, May 7, 2014.
President Jakaya Mrisho Kikwete in a bilateral meeting with Rt. Hon. Gordon Brown (MP), UN Special Envoy for Global Education and Former British Prime Minister in the sidelines of the World Economic Forum on Africa in Abuja, Nigeria, May 7, 2014.

Mahojiano ya SBS na Maria Sarungi-Tsehai kuhusu Bunge la Katiba

Wakati Bunge Maalumu la Katiba likiwa limehairishwa, mjini Sydney nchini Australia wiki hii Idhaa ya Kiswahili ya SBS ilipata fursa ya kuongea moja kwa moja kutoka Tanzania na Mhe. Maria Sarungi-Tsehai ambaye ni mmoja wa Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.

Mhe. Maria alichambua kwa kina vipi mchakato wa katiba hiyo ulivyokuwa na nini matazamio yake kwa muhula ujao wa bunge hilo.

Bofya kitufe cha pleya iliyopachikwa hapo chini (au hapa) ili kumsikiliza.

Siri za TPA zaandikwa: Orodha ya Watumishi walioonewa

Na Deodatus Balile

Siri nzito zimeanza kuvuja jinsi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mzee Madeni Kipande (58), anavyofanya unyanyasaji kwa wafanyakazi wa Bandari hiyo, hasa wanawake, vyanzo vimeifahamisha JAMHURI.

Pia, wafanyakazi waliozungumza na JAMHURI (majina yanahifadhiwa kwa sababu za wazi), wamesema katika viambaza vya Bandari hiyo sasa wanamuona Kipande kama aliyekuwa kiongozi wa taifa la Uganda dikteta Idi Amin Dada.

“Chini kwa chini wafanyakazi wamembatiza jina IDI AMIN, na wengi wanarejea filamu ya ‘Last Kingo of Scotland’ inayoigiza udikteta aliokuwa akifanya Idi Amin, wanasema Kipande naye amejielekeza katika

Mtwara Music Tour this Saturday!Venue: Makonde Royal Night Club-Mtwara

Artists: Nicki Mbishi, Songa, One The Incredible, JANB, Chaba, Chanya, Daz Naledge, Wagosi wa Kaya.

Host: Nandy wa Big Brother Africa

Date: 10th May 2014 (Saturday)

Time: 09:00 pm till dawn

Price : Tsh 7,000/-

HESLB yaanza kupokea maombi ya mikopo

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imefungua maombi ya mikopo kwa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na Taasisi za Elimu ya Juu zinazotambulika, kwa masomo ya shahada mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2014/2015.

Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Cosmas Mwaisobwa, amesema maombi ya mikopo yanafanyika kwa njia ya mtandao (OLAS) na yamefunguliwa kuanzia Aprili 23 mwaka hu na yatafungwa rasmi Juni 30, 2014.

Alisema Bodi inatarajia kutoa mikopo kwa wanafunzi takriban 35,000 wa mwaka wa kwanza, watakaodahiliwa kujiunga na masomo katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu.

Ripoti ya Twaweza: Je, vituo vya afya vipo kwa ajili ya kuwahudumia watu?

Ni mtu 1 tu kati ya watu 20 (6%) mwenye umri zaidi ya miaka 60 na ni mtoto 1 kati ya 5 (18%) mwenye umri chini ya miaka mitano ambao hupata huduma na matibabu bure katika vituo vya afya.

Sera ya Nchi inasema kuwa huduma kwa wagonjwa wa nje kutoka makundi haya mawili ni bure, lakini wananchi wanasema kuwa wanatozwa pesa.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika muhtasari wa utafiti wenye jina la Je, vituo vya afya vipo kwa ajili ya kuwahudumia watu? Wananchi na watumishi wa afya wazungumzia huduma za afya.

Muhtasari huu ni kwa mujibu wa takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti kwa njia ya simu za mkononi, wenye uwakilishi wa kitaifa uliofanyika kwenye kaya zote Tanzania Bara.

Pakua nyaraka

Taarifa maalum kwa Watanzana wa UAE

TANGAZO MAALUM

Ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Dubai, UAE, unapenda kuwatangazia Watanzania wote waishio UAE kuwa wanatakiwa kujiandikisha upya katika Ofisi za Ubalozi mdogo zilizopo UMM AL SHEIF Road, AL SAFA 2, JUMEIRAH 3, Dubai.

Tafadhali hakikisha kuwa unawasilisha taarifa zifuatazo:-

  • JINA KAMILI
  • MWAKA WA KUZALIWA
  • JINSIA
  • MWAKA ULIONGIA UAE
  • MUAJIRI
  • ANUANI YA MUAJIRI
  • ANUANI YA UNAKOISHI
  • SIMU
  • EMAIL

Karibuni mjiandikishe kwa manufaa yenu, ili kutuwezesha pia kufahamu idadi kamili ya Watanzania waishio UAE.

increase of Internet users pushed Africa towards online development

Back in the days the African continent was not the place people can invest their money in the ICT sector in general, big companies feared that the region was not very productive for investment especially in the ICT.

Africa is the second most populated continent and the second world largest continent, but the emerging of internet came late in the 90’s.

Today Africa is developing very fast and the increase of the Internet users have managed to push Africa towards the online development. Now there are a large number of online opportunities and there is a large increase in investment towards the ICT sector.As reported by vc4africa, the statistical record shows that the growth forecast is staggering. In 2013 Internet

Walimu wamfungia DED ofisini

WALIMU zaidi ya 125 wanaofundisha shule mbalimbali wilayani Igunga, wameandama na kufunga Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ili kushinikiza walipwe mishahara na posho zao wanazodai kwa kipindi cha miezi minne.

Kufungwa kwa ofisi hiyo kulisababisha wafanyakazi wa halmashauri kukaa nje ya ofisi na huduma kusimama kwa saa tano.

Mmoja wa walimu hao, ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema wanasikitishwa na kitendo cha kucheleweshwa mishahara yao na posho zao kwa kuwa ni kitendo cha kinyama.

Alisema tangu wapelekwe wilayani humo, wamekuwa wakifuatilia mishahara na posho bila mafanikio na

Rushwa kali katika upangaji vituo kwa watumishi wapya

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia, amesema upangaji wa vituo kwa watumishi wapya ni eneo lenye harufu kali ya rushwa.

Amesema walimu ndio wamekuwa waathirika wakubwa kutokana na watumishi waliopewa jukumu hilo kudai rushwa na kwamba, hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa ili kudhibitiwa.

Amesema hakuna dalili njema kwenye eneo hilo na mianya ya rushwa iliyopo inatakiwa kuzibwa haraka na

Kumbe watu wakiamua mambo ya Serikali yanawezekana? - LLKHiyo ni zahanati ya serikali iliyoko Kunduchi Mtongani. Nilikwenda hapo mara ya kwanza kama miezi mitatu iliyopita; nilishangaa kuona wahudumu walio “serious”, maabara inayofanya kazi na vifaa vipo, pia na madawa yapo. Na kila dawa inayotoka inarekodiwa!

Nimerudi hapo juzi, nikashangaa kukuta ukarabati mkubwa uliofanywa, ndani ya muda mfupi sana. Tiles nyeupe kote, mpaka majengo ya nyuma, choo safi namaua yanayohudumiwa. Pia huduma za uhakika. Nilitaka

Askari Wanyama Pori waua ng'ombe 150 Biharamulo

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amekiri kuuawa kwa ng’ombe 150 kulikofanywa na askari wa Wanyama Pori katika Hifadhi ya Biharamulo, kutokana na mgogoro uliokuwepo wa kuwaondoa baadhi ya wafugaji, waliovamia eneo la hifadhi.

Akizungumza na gazeti la HabariLeo kwa njia ya simu jana, Prof. Tibaijuka alisema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amewaagiza baadhi ya Mawaziri kwenda wilayani humo, kusuluhisha mgogoro huo:
"Tuko huku baadhi ya mawaziri, tumeagizwa na Serikali Kuu kuja kushughulikia mgogoro huu, kulikuwa na mgogoro ambapo watu waliokuwa wakiondolewa hifadhini, sasa mchakato huo ukasababisha ng'ombe hao uliowataja kufa," "Tuko huku na sasa hivi ndiyo tumetoka kwenye kikao cha kushughulikia mgogoro huu, lakini mpaka sasa tumeshafikia pazuri.,"
alisema Waziri Tibaijuka.

Alisema wachungaji wa ng’ombe hao, walikamatwa ndani ya hifadhi pamoja na mifugo yao, na utaratibu ulipaswa kuwapiga faini au kufikishwa mahakamani kwa wale watakaogoma kulipa faini, lakini katika mazingira hayo kuliibuka mgogoro huo.

[video] Mdahalo ITV: "Bunge la Katiba na Tanzania tunayoitaka"

Iliyopachikwa hapo ni playlist yenye video za mdahalo ulioandaliwa na kituo cha runinga cha ITV kuhusu Bunge Maalum la Katiba na Tanzania tuitakayo, uliofanyika siku ya Jumapili, Mei 4, 2014.Shukurani za video upload/sharing zifikie "KAMATI YA MARIDHIANO"