Nyimbo za Injili: Reuben Kigame na Wanakwanya wa Sifa Voice

Playlist yenye video nne za nyimbo za kumsifu na kumwabudu Mungu kwa utunzi wake Reuben Kigame (asiyeona/mlemavu wa macho) akishirikiana kuimba na wanakwaya wa Sifa Voice katika:-


  1. Sina Mungu mwingine
  2. Enda nasi
  3. Vita vizuri
  4. Baba Yetu wa Mbinguni


Na iwe Jumapili njema ya neema tele, baraka na fanaka!

Call: ITEC list of courses, Application form; Scholarship

Call for application for Indian Technical and Economic Cooperation (ITEC) 2014/2015

Applications are invited from qualified Tanzanians from the Public Sector to apply for Short Courses tenable in India for the year 2014/2015.

More information on courses and application forms are listed below:

Tanzanite benefits India despite ban on raw exports

(image via gemorie.com/)

By Adam Ihucha via Arusha Times -- Tanzania’s four-years-old partial ban on export of raw Tanzanite seems to have been ineffective to control a large chunk of gemstone from being shipped to Asia.

In July, 2010, Tanzania, the world’s sole source of Tanzanite, outlawed exports of rough stone weighing above one gram, in a bid to compel the world’s gemstone dealers to spur development of local processing industry.

The embargo was part of the Mining Act of 2010, which intends to create

Spika Makinda: UKAWA huko huko kwa Sitta si kwangu!

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amesema ni marufuku kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kufanya shughuli zake ndani ya Bunge la Bajeti, linaripoti gazeti la HabariLeo.

Spika amenukliwa akisema hayo juzi bungeni baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kutangaza Baraza Kivuli la Mawaziri na kusema hicho ndiko kikosi cha UKAWA ndani ya Bunge.

Spika Makinda alimtaka Mbowe kuhakikisha UKAWA inafanya kazi zake nje ya Bunge na si

Prof Costa Mahalu, Ms Grace Martin are completely free

The High Court in Dar es Salaam yesterday withdrew an appeal against the acquittal of former Tanzanian Ambassador to Italy Professor Costa Ricky Mahalu who ad been charged with defrauding the government money.

According to the High Court, the withdrawal of the appeal follows the appellant, Director of Public Prosecution (DPP) Eliezer Feleshi, showing no interest to continue with the case.

An appeal by the Director of Public Prosecution (DPP) had challenged the acquittal of Professor Costa Ricky

Wahariri wa Vyombo vya Habari na TGNP waichambua Bajeti

Picha na maelezo kutoka kwa Joachim Mushi/TheHabari.com

  Aliyekuwa Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Usu Mallya (kushoto) akiwasilisha mada yake kwa wahariri wa vyombo vya habari katika mkutano wa TGNP na wahariri hao.

Watanzania washiriki mbio na matembezi ya Susan G. Komen

Picha na maelezo kutoka kwa Luke Joe/Vijimambo Blog
Timu Tanzania katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mbio za maili tano.

Ziara ya Rais Kikwete katika kiwanda kikubwa cha saruji duniani "Dangote Cement Obajan Plant"

0L7C1291.jpg (1600×1066)

Rais Kikwete akioneshwa aina ya mali ghafi inayotumika alipotembelea Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014
  • Ni kile kinachomilikiwa na mwekezaji anayejenga kiwanda cha saruji Mtwara
Picha na taarifa kutoka Ikulu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametumia siku nzima Ijumaa, Mei 9, 2014, kutembelea kiwanda kikubwa zaidi cha saruji kuliko kingine chochote duniani cha Dangote Cement Obajana Plant na kinachomilikiwa na tajiri mkubwa zaidi wa Afrika, Bwana Aliko Dangote, ambaye pia anajenga kiwanda kikubwa cha saruji mjini Mtwara.

Akiandamana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Abdallah Kigoda, kwa siku nzima, Rais

Ufafanuzi wa Serikali kuhusu taarifa za "kufukuzwa" Wakurugenzi wa Wizara ya Maliasili na Utalii


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

IDARA YA HABARI - MAELEZO

PRESS RELEASE

P.O. Box 8031, Dar es Salaam, Tel: 2110585, 2122771/3, Fax: 2113814, e-mail: [email protected]

            Serikali inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa potofu zinazoendelea kuchapishwa na kutangazwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu Watumishi Waandamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Alexander Songorwa ambaye ni Mkurugenzi, Idara ya Wanyamapori na Prof. Jafari Kideghesho, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori.

            Kumekuwa na taarifa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba Wakurugenzi hao walikuwa wamefukuzwa kazi na Waziri wa Maliasili na Utalii, na kisha kurejeshwa kwa maelekezo ya Ikulu. Taarifa hizo si sahihi.

            Ukweli ni kwamba Prof. Alexander Songorwa na Prof. Jafari Kideghesho hawajawahi kufukuzwa kazi ama kuadhibiwa. Hatua za kinidhamu katika Utumishi wa Umma zina  taratibu na miongozo yake, inayotawaliwa na nyaraka kuu nne, miongoni mwa nyingine, kama ifuatavyo:-

Maelezo ya Waziri Mkuu yenye majibu ya hoja za Wabunge

MAELEZO YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU, WAKATI AKIJIBU HOJA ZA WABUNGE KUHUSU HOTUBA YA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA TAASISI ZAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015


UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,
·                     Niruhusu nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwenye Rehema kwa kunipa Afya njema hadi leo ninapohitimisha Majadiliano ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu; Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2014/2015.

Mheshimiwa Spika,
·                     Katika mjadala huu, jumla ya Waheshimiwa Wabunge 155 Walichangia. Waheshimiwa Wabunge 92 waliochangia kwa kuzungumza moja kwa moja hapa Bungeni na Waheshimiwa Wabunge 63 wamechangia kwa njia ya maandishi.

·                     Kama ilivyo miaka yote idadi ya Wachangiaji ni kubwa na muda wetu umekuwa mfupi sana. Hii inaonesha dhahiri jinsi ambavyo Waheshimiwa Wabunge mnatambua umuhimu wa majukumu yanayotekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini yake.

·                     Tumejitahidi kujibu hoja hizo kupitia Mawaziri na Naibu Mawaziri, lakini bado zimebaki nyingi. Kama ilivyo ada tutajitahidi kujibu hoja zilizosalia kwa njia ya maandishi.

MAJIBU YA HOJA

Mheshimiwa Spika,

Mbunge augua homa ya kidinga popo "dengue fever" / homa ya denge

Mbu anayeeneza virusi vya homa ya denge
Mbu aina ya Aedes anayeeneza virusi vya homa ya denge

Mbunge wa viti maalumu kutoka Unguja Kaskazini (CCM) Bahati Ali Abeid amelazwa katika hospitali ya Dk Mvungi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kuugua homa ya kidinga popo ama homa ya denge (dengue fever).

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Dokta Gunini Kamba alitaarifu kuwa Mbunge huyo alilazwa hospitalini hapo siku ya Jumatano akiwa katika uangalizi wa karibu wa madaktari.

Dk Kamba alisema ugonjwa huo unasambaa kwa kasi katika wilaya ya Kinondoni na takwimu za Serikali zinaonesha kuwa tayari watu 305 wameripotiwa kuugua homa hiyo. Alisema pia kuwa wapo watu wengine wanaougulia majumbani bila kwenda hospitalini.

Mwezi Juni mwaka jana na Februari mwaka huu, Wizara ya Afya ilitoa taarifa kuhusu homa ya denge. Mwezi Aprili mwaka huu, Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia idhaa ya Kiswahili nalo lilitoa taarifa kuhusu kusambaa kwa ugonjwa huu nchini Tanzania na nchi jirani ya Msumbiji na Dk Janet Mgamba ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti na Ufuatailiaji wa Magonjwa ya Milipuko alieleza (audio) hali ya homa hiyo ilivyo na hatua zilizochukuliwa.

Mwezi mwaka huu, gazeti la Mwananchi limechapisha habari ya "Daktari akieleza alivyougua homa ya denge"

Discussion on trying in Tanzanian courts pirates captured by European Naval Forces

The following post was shared with us by Zainul Mzige/MoDewji Blog

Public Relation Officer of European Union Dormann addressing some issues during Press Conference.
Public Relation Officer of European Union Dormann addressing some issues during Press Conference.

Inakera! Inasikitisha! Wazee 2 wawalawiti watoto 6 wa shule

Wazee wawili akiwemo mlinzi mmoja wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya wilaya ya Bunda, mkoani Mara, wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kulawiti wanafunzi sita wa shule za msingi zilizoko wilayani hapa.

Waliofikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda, ni pamoja na Thomas Machugu (72) ambaye ni mlinzi na mkazi wa mtaa wa Saranga.

Mwingine ni Salum Mfumbasi (66) ambaye ni mfanyakazi wa ndani kwa mfanyabiashara mmoja wa

Mnara wa kuwakumbuka albino waliouawa Tanzania wazinduliwa

Rais wa Shirika linalohudumia watu wenye ulemavu wa ngozi duniani liitwalo Under the Same Sun, Peter Ash (wa pili kushoto) pamoja na mratibu wa shirika hilo nchini Vick Ntetema, wakiwa na Mkuu wa wilaya ya Sengerema (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa wilaya ya Sengerema Alfred Kapole (kulia) wakishikana mkono mara baada ya rais huyo kuzindua Mnara wa kwanza wa kipekee wa kumbukumbu ya watu waliouawa nchini Tanzania katika matukio mbalimbali yaliyo husisha imani potofu za kishirikina na suala la albinism.
Rais wa Shirika linalohudumia watu wenye ulemavu wa ngozi duniani liitwalo Under the Same Sun, Peter Ash (wa pili kushoto) pamoja na mratibu wa shirika hilo nchini Vick Ntetema, wakiwa na Mkuu wa wilaya ya Sengerema (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa wilaya ya Sengerema Alfred Kapole (kulia) wakishikana mkono mara baada ya rais huyo kuzindua Mnara wa kwanza wa kipekee wa kumbukumbu ya watu waliouawa nchini Tanzania katika matukio mbalimbali yaliyo husisha imani potofu za kishirikina na suala la ualbino (picha: GSengo blog).
Mnara uliozinduliwa unamwonyesha baba asiye na ualbino akiwa amembeba mabegani mtoto wake albino huku mama ambaye pia si albino akisaidia kumvika kofia mwanaye. Baba na mama wasio na ualbino katika mwonekano wa ngozi ya kawaida wanaweza kuzaa mtoto albino.
Mnara huu wa kwanza wa kihistoria dunia umesimikwa katika kipita shoto kikuu kinachounganisha barabara zinazoelekea mkoa wa Geita, Kahama, Bukoba mkoani Kagera na Kamanga mkoani Mwanza, ukiwa umeorodheshwa majina takribani 72 ya albino waliouawa.

Operesheni safisha Jiji yasitishwa

Umoja wa wabunge jijini Dar es Salaam umesema utasitisha operesheni ya safisha Jiji ambayo inaendelea na kuendeshwa kibabe ambapo ni kinyume na makubaliano yao na Mkuu wa Mkoa, liliandika gazeti la HabariLeo wiki hii.

Akitoa kauli hiyo juzi, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mwenyekiti wa umoja huo, alisema operesheni hiyo imekuwa na matukio ya uvunjifu wa haki za kibinadamu ikiwemo unyanyasaji wa walemavu. Alisema watu wenye ulemavu wamekuwa wakishurutishwa kuondoa bidhaa zao kwa