Dk Isaac Maro achanachana fedha bandia studioni

Fedha bandia (picha, maelezo na GSengo blog)

Kama ulisikiliza kipindi cha Njia Panda kupitia redio ya Clouds FM hii leo kikiongozwa na Dk. Isaac Maro, utakuwa

Auwa wazazi wake na kuchoma nyumba moto

UPDATE/TAARIFA MPYA, Mei 12, 2014 Update hii inalandana na iliyopi katika gazeti la HabariLeo

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro, linamshikilia Yusufu Njau (32), mkazi wa kijiji cha Roo Wilayani Hai mkoani humo, kwa kosa la kuwauwa wazazi wake ‘kikatili’ kwa kuwakata na mapanga kichwani na kisha kuchoma moto nyumba waliyokuwa wanaishi wazazi hao.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Robert Boaz, ameiambia FikraPevu Jumatatu Mei 12, 2014 kuwa mtuhumiwa huyo aliyefanya kitendo cha kinyama Mei 09, 2014 saa kumi na mbili za jioni nyumbani kwao, ambapo kupitia msako ulioendeshwa na Jeshi hilo kuanzia siku ya tukio ambapo leo (Jumatatu) saa mbili asubuhi lilimkamata akiwa nyumbani kwa kaka yake Alifa Shaibu.

Mazishi
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika kijiji cha Roo, Tarafa ya Masama, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wakiwa katika sala ya mazishi ya marehemu iliyofanyika Mei 10, 2014, ambapo Shahidu Njau na mkewe Minei Swai, walipokutwa na mauti baada ya kucharangwa/katwa mapanga na mtoto wao
Boaz, amesema mtuhumiwa alimuua Baba yake mzazi, Shahibu Hassan (60), pamoja na Mama yake mzazi, Minae Mohamed (57), ambao waliozikwa Jumamosi, Mei 10 2014 katika makaburi ya familia kijijini hapo.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Roo, Alfani Swai, alisema mtuhumiwa huyo alitoka kutoka alipokuwa amejificha baada ya kukumbwa na njaa kali ndipo alipoenda nyumbani kwa kaka yake ‘Alifa Shaibu’ kwa nia ya kuomba chai.
Amesema mara baada ya mtuhumiwa huyo kufika kwa Kaka yake alipata simu kuwa mtuhumiwa huyo yuko katika nyumba hiyo, ndipo alipowasili na kumpeleka mtuhumiwa katika katika kituo cha Polisi Bomang’ombe.

Mara baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo wananchi wa kijiji hicho walisema kwa sasa wataishi kwa amani kijiji hapo, kutokana na kuwa na mashaka na mtuhumiwa huyo aliyekuwa akisumbua kijiji hicho kwa muda mrefu.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa hali ya usalama nchini, inaonekana kutia shaka wananchi kufuatia mfululizo wa matukio ya watu kutekwa, kuteswa hata kuuawa kwa ndugu wa familia moja wa watoto na baada ya mda watuhumiwa huripotiwa kukamatwa katika maeneo mbalimbali nchini na sheria kuelezwa inaanza kuchukua mkondo wake kwa kuanzisha upelelezi wa matukio hayo.

------------

(picha: DIxon Busagaga/"Globu ya Jamii" blog)

TAARIFA KWA MUJIBU WA GAZETI LA HABARI LEO


Simanzi kubwa imetanda katika Kijiji cha Roo, Kata ya Masama Mashariki wilayani Hai, Kilimanjaro, baada ya kijana mwenye umri wa miaka 32 kuwaua wazazi wake wawili kwa kutumia panga na shoka, kisha kuchoma moto nyumba yao.

Kijana huyo aliyetambulika kwa jina la Yusuph Njau aliwaua wazazi wake, Shahidu Njau (60) na Minae Swai (57) baada ya kuwafungia ndani na kuwakata kata kwa kutumia shoka na panga.

Akizungumza na mwandishi, Diwani wa Kata ya Masama Mashariki, Ally Mwanga alisema mauaji hayo yalitokea

Wanafunzi waandamana baada ya mwenzao kufa; Mwalimu Mkuu azimia

FikraPevu inataarifu kuwa Wanafunzi wapatao 344 wa shule ya sekondari ya wasichana Masasi mkoani Mtwara wameandamana hadi nyumbani kwa Mkuu wa wilaya ya Masasi, Farida Mgomi wakishinikiza kuondolewa kwa mkuu wa shule hiyo, Reinader Tesha kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha tano Omega Kabuje aliyefariki jana (Jumamosi).

Maandamano hayo yameganywa leo, Jumapili saa 11 alfajiri lakini wanafunzi hao hawakufanikiwa kukutana na Mgomi kwa kuwa alikuwa safarini Mtwara.

Mkuu wa shule hiyo, Reinader Tesha alijikuta akipoteza fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya