Tangazo muhimu la JKT kwa wahitimu Kidato cha VI

TANGAZO MUHIMU KWA VIJANA KIDATO CHA SITA 2014 MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA KWANZA NA AWAMU YA PILI


Orodha ya Vijana wa Kidato cha Sita watakaokwenda JKT kwa mujibu wa sheria Awamu ya Kwanza imefanyiwa marekebisho kama ifuatavyo:-
  • Vijana 1,200 wameondolewa kutoka kikosi cha Ruvu na kupelekwa vikosi vya Mautupora, Mafinga na wachache vikosi vingine.
  • Merekebisho machache pia yamefanyika katika vikosi mbalimbali.
  • Kutokana na marekebisho hayo, vijana wanasisitizwa kuhakiki tena majina yao katika orodha mpya iliyopo kwenye tovuti hii.
Vijana wote ambao hawajapangwa Awamu ya Kwanza, wamepangwa Awamu ya Pili na orodha yao itawekwa kwenye tovuti hii (www.jkt.go.tz) muda wowote kuanzia sasa.

Taarifa hii imetolewa na Makao Makuu ya JKT.
---

Mawasiliano na Jeshi la Kujenga Taifa

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa
S.L.P 1694, Dar es Salaam.

Simu:+255-22-2780588/2780712
Fax:+255-2-270048
Website: www.jkt.go.tz

Mana Conference with Mwalimu Mwakasege in US, June 6 - 8


Rais Kikwete ahani msiba wa Mama Mkwe wa Jaji Warioba

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji wanafamilia bada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa mama mkwe wa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Marehemu Hedwig Laurent Ojjik, Oysterbay jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2014

Wakimbizi walioko Tanzania kuhamishiwa Marekani

Wakimbizi wenye asili ya nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi wapatao 32,000 walioko nchini Tanzania wanatarajiwa kuhamishiwa nchini Marekani.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe alitoa taarifa hiyo jana Bungeni kwa kusema kwamba huo ni mpango maalumu unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano.

Alisema unatekelezwa katika mwaka wa fedha 2014/2015 kwa kushirikiana na Serikali ya Marekani baada ya serikali kusaini mkataba na mashirika ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia

Maziko ya Private Brian Salva Rweyemamu

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Bw. Salva Rweyemamu na mkewe Isabella wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wao Private Brian Salva Rweyemamu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2014

Hotuba ya Waziri Kivuli, G. Lema ya Wizara ya Mambo ya Ndani 2014/15

HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015 NA MHE.GODBLESS JONATHAN LEMA (MB).


UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,


Kwa mujibu wa ‘Instrument’ ya Serikali inayoainisha majukumu kila Wizara, Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi imepewa majukumu ya kushughulikia masuala ya Usalama wa Raia, Uhamiaji na utekelezaji wa Sera za zima moto na uokoaji. Aidha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inashugulikia pia masuala ya huduma za Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji, Uraia, Vitambulisho vya Taifa, Huduma za Wakimbizi, Usajili wa Vikundi au Vyama vya Kijamii, Huduma za Zima Moto na Uokoaji na mambo mengine yanayohusu maendeleo ya rasilimali watu katika Wizara hiyo.

Mheshimiwa Spika,

Ukitazama majukumu ya Wizara hii, utaona kwamba ina majukumu mazito sana yanayohusu usalama wetu sote kama raia wa nchi hii. Ni majukumu yanayohusu maisha yetu. Hivyo wizara hii inatakiwa