Taarifa ya kukwapuliwa akaunti ya Facebook ya Meya Jerry Silaa

Jerry Silaa
Jerry Silaa

Napenda kuwajulisha marafiki zangu wote kwamba akaunti yangu ya Facebook ime-hack-iwa na kuanza kutuma ujumbe kwa marafiki zangu kuwataka waingie kwenye link kwani nina maongezi ya siri.

Tafadhali puuzia ujumbe huo kwani utasababisha akaunti yako nayo ku-hack-iwa.

Tafadhali sambaza ujumbe huu, wakati tunaendelea kujaribu kuiokoa. Nawaomba radhi wote walopatwa na usumbufu huu.

Jerry Silaa

Usiku wa Wanawake wa Tanzania-Marekani wafana


Meza alioyokaa Mhe. Liberata Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja kwenye ukumbi wa Martin's Crosswinds uliopo Greenbelt, Maryland kwenye usiku wa Wanawake wa Tanzania ulioratibiwa na kikundi cha wakinamama watano chenye maskani yao DMV kinachobeba jina la Tano Ladies na kuufanya

Tangazo la Chuo cha Ualimu Kidugala

KKKT Dayosisi ya Kusini tumeanzisha Chuo Cha Ualimu cha Kilutheri Kidugala kitakachotoa masomo ya Sayansi na Sanaa ngazi za Diploma na Cheti kuanzia Julai 11, 2014.

Ili kupata maelezo na taarifa zaidi, tafadhali piga simu kwa:
  1. Mkuu wa Chuo, Mwal. Yohannes Mwangamila 0756390354 
  2. Mwalimu wa Taaluma, Mwal. Albert Masinga 0754805674 

Au tuandikie kwa barua pepe: [email protected]

Anwani ya barua:

Chuo cha Ualimu Kidugala,
S.L.P. 999,
Njombe.

Kashfa: Mgonjwa aliyeoza makalio afukuzwa hospitalini

KASHIFA nzito imeikumba Hospitali ya rufaa ya Bugando ya Jijini Mwanza baada ya kudaiwa "kumfukuza" mgonjwa wake ambaye ameozea makalio wodini hapo, Joseph Luhogola (38), na sasa anaendelea kuoza akiwa nyumbani kwa mganga wa tiba za asili.

Luhogola, mkazi wa Kitongoji cha Nyabugera, Kijiji cha Mganza Wilaya ya Chato katika Mkoa wa Geita alipokelewa Hospitalini hapo tarehe 22 Aprili 2014 akitokea katika Hospitali ya Wilaya ya Chato ikiwa ni saa chache baada ya kupata ajali.

Tafadhali:

Makamu wa Rais abariki tamasha la 17 la ZIFF 2014, Zanzibar


Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na mabalozi kwenye ufunguzi wa tamasha la 17 la ZIFF.


Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto, akizungumzia changamoto mbalimbali na mafanikio aliyoyapata baada ya kushiriki kwenye filamu hiyo.


Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na mabalozi kwenye ufunguzi wa tamasha la 17 la ZIFF.

Mwanafunzi alazimishwa kula kinyesi chake kwa kosa la kujisaidia kisimani

Valence Robert @ Malunde1 blog anaripoti kuwa, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 8 wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Nyakabale huko Geita amelishwa kinyesi chake baada ya kukutwa anajisaidia kwenye kisima akiwa na wenzake wakitoka shuleni.

Kamanda wa polisi mkoani wa Geita Joseph Konyo amesema kuwa tukio hilo limetokea tarehe 11 mwezi huu majira ya saa 4 asubuhi ambapo mwanafunzi huyo akiwa na wenzake watatu wakitoka shule kufanya usafi, walipofika eneo hilo mwanafunzi mwenzao alienda kujisaidia karibu na kisima cha

Picha za tamasha la "NAIAMINIA TANZANIA" lilizofanyika Dodoma

Mama Maria Nyerere akiwa tayari kwa Tamasha la "NAIAMINIA TANZANIA" hapa Dodoma.


Kampeni hii itakwenda nchi nzima kwa ajili ya kusambaza upendo na kutambua umuhimu wa kulinda na kulitetea Taifa la Tanzania.
Mwana FA

MSD yaanza kusambaza dawa zenye nembo ya Serikali, "GoT"


via Doto Mwaibale blog -- Ili kudhibiti upotevu  wa dawa za serikali, katika mwaka huu wa fedha Bohari ya Dawa imeanza kuziwekea nembo ya GOT (Government Of Tanzania) yaani “Serikali Ya Tanzania” dawa zake, kama serikali ilivyoagiza.

Akielezea hatua hiyo kwaViongozi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na Ushawishi na utetezi juu ya Utawala Bora katika sekta ya Afya, SIKIKA ambao walifikaofisiza MSD kufuatialia utekelezaji huo, Kaimu MkurugenziMkuuwa MSD, Bwana CosmasMwaifwani amesema tayari sampuli 32 za dawa zimesha wekewanemboya GOT nawazabuniwotewameelekezwakuwekanembohiyokatikadawanavifungashio.

Bwana Mwaifwani ameeleza kuwa tayari vituo vya afya, zahanati na hospitali zimeanza kupokea dawa ambazo zina nembo ya GOT hiyo na ile ya MSD, huku akiongeza kuwa dawa nyingine zilizosalia zitawekewa nembo hiyo, isipokuwa zile ambazo zina umbo dogo zitawekewa katika vifungashio tu.

Kwaaupande wake Mkurugenziwa SIKIKA Irenei Kiria ameishauri Bohariya Dawa kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha juu ya nembo hiyo ya GOT kwenye vidonge, ilikuchangia ulinzi shirikishi wa dawa kupatikana katika maeneo yasiyostahili.

MSD tayari imekuwa na machapisho na vipindi mbalimbali na semina kuelimisha wadau juu ya uwekaji wa nembo ya GOT kwenye vidonge, na inatarajia kuwa na mpango endelevu wa elimu kwa umma kuhusiana na nemboya GOT.