Ufafanuzi wa TANESCO kuhusu umeme kukatika nchi nzima

Wabunge wakimulikiana kwa kutumia mwanga wa kurunzi la simu ndani ya ukumbi wa Bunge, Dodoma baada ya umeme kukatika huku kikao kikiendelea.

Baada ya kukatika kwa umeme majira ya saa moja na kusababisha karibu mikoa yote ambayo imeunganishwa na gridi ya taifa kukosa nishati ya umeme na kusimamisha shughuli za Bunge ikiwemo zoezi la upigaji wa kura ya Bajeti ya Serikali, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini, TANESCO, Mhandisi Felchesim Mramba ametoa ufafanuzi juu ya hilo na kubainisha kuwa mafundi wa shirika hilo wanaendelea kufanya uchunguzi.

Video ya ITV iliyopachikwa hapo chini ina taarifa zaidi...
SHIRIKA LA UMEME ZANZIBAR (ZECO)


Namba yetu
Maulizo: 024 223 8321
Dharura: 024 223 0232  
                                                        
Afisi Kuu
S.L.P 235,
Zanzibar – Tanzania
Simu: +255 774 334 455
Barua Pepe: [email protected]


TAARIFA KWA WANANCHI WA ZANZIBARJUU YA KUKATIKA KWA UMEME

Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) limesikitishwa sana na kuzorota kwa shughuli za maendeleo kutokana na kukatika kwa umeme visiwani Unguja na Pemba kuanzia majira ya saa moja usiku hadi saa tatu usiku.

Sababu iliyopelekea kukatika huko ni kutokana na kuondoka kwa gridi ya taifa ambayo Zanzibar inapata umeme kupitia gridi hiyo.

Maeneo yote ya Unguja na Pemba yalikosa umeme na baadhi ya mikoa mingi ya Tanzania Bara iliyounganishwa na Gridi ya taifa nayo ilikosa umeme ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Mengineyo.

Wakati akizungumza na kituo kimoja cha habari nchini Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesim Mramba amesema ya kuwa kuzimika kwa mitambo ya kuzalisha umeme ghafla ndiko kulikopelekea kukosekana kwa umeme nchi nzima ambako husababishwa na kuzimika kwa moja ya mitambo ya kuzalisha umeme.

Katika taarifa yake amefafanua ya kuwa chanzo hasa kilichopelekea kuzimika kwa mitambo hiyo bado hakijajulikana na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kutambua kilichosababisha katizo hilo.

Kwa upande wa Shirika la umeme Zanzibarlinasikitishwa na kukatika kwa umeme huko kwani shughuli nyingi za kimaendeleo ziliweza kusimama ikiwemo wananchi kukosa kutazama na kusikiliza maelezo ya moja kwa moja kutoka Baraza la Wawakilishi, kukosa kuangalia michezo ya kombe la dunia na kusimama kwa shughuli nyengine za kimaendeleo.

Shirika litaendelea kutoa taarifa za kina kwa vyanzo vyovyote vile vya kukatika kwa umeme na kuwaomba wananchi kuwa wastahamilivu wakati wa matukio kamahayo yanapotokea kwani husababishwa na mambo ambayo yako nje ya uwezo wa Shirika.

Shirika linapenda kutoa kuwakumbusha wananchi kuacha vitendo vya kuhujumu miundo mbinu kwa kuchimba mchanga chini ya njia za umeme kwani kuanguka kwa nguzo ya umeme ni chanzo kikubwa kinachopelekea kulikosesha taifa huduma hii muhimu ya umeme.

Imetolewa na Shirika la Umeme

Zanzibar.

Binti wa Kitanzania anatafutwa na Chuo cha Marekani

Yule binti aliyecheza na mpira wa miguu katika mitaa mbalmbali ya Morogoro hasa kwenye stendi ya mabasi na kuwavutia watu mbalimbali kwa uwezo wake wa kuumudu mpira huku akionesha burudani safi --tizama video hapo chini-- , kiasi cha kuwekwa kwenye ukurasa wa tovuti kubwa ya habari 'mpwito mpwito' ya The Sun ya Uingereza, anatafutwa na Chuo kimoja cha nchini Marekani, kwa mujibu wa tweet ya Robert Alai.

Yeyote mwenye taarifa ama maswali kuhusiana na hili, tafadhali wasilana na Alai kwenye twitter.com/RobertAlai

Malawi to close some Embassies

Malawi's the Nyasa Times writes that the newly appointed Minister of Foreign Affairs and International Relations, Dr George Chaponda, has announced some cost-cutting measures, including the closure some of the country’s embassies.

That, Chaponda said after being sworn-in to take his portfolio that among his primary priorities was reducing the number of embassies that Malawi has partly as cost-cutting measure.

“We are a poor country and we only need to maintain those embassies that are

Rais KIkwete awasili Malabo kwa mkutano wa 23 wa AU


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Malabo, Equatorial Guinea, leo Juni 24, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Malabo, Equatorial Guinea, leo Juni 24, 2014

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mji mkuu wa Equatorial Guinea wa Malabo leo Juni 24, 2014 kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Africa – African Union (AU).

Mkutano wa sera za mgombea wa Jumuiya ya Watanzania DMV

Kutakuwa na Mkutano wa Sera za Mgombea wa Jumuiya ya Watanzania DMV

Bwana Liberatus Mwang'ombe

Atakachoongea katika mkutano wake ni kuhusu Elimu na Diversity Visa Lottery na YOUNG African Leaders Initiatives, Jumuiaya na Afya, Baraza la ushauri, Darasa la Kiswahili. Ushirikiano na umoja, Jumuiya na wajasiriamali, Jumuia na vyanzo vya mapato, Jumuiya na mrejesho wa ubalozi, "Power of attorney".

Mkutano huo utafanyika siku ya Jumamosi, Juni 28, 2014 kuanzia saa 10 alasiri (4pm) Meadowbrook Park 7901, Meadowbrook Lane, Chevy Chase, MD 20815 

Kutakuwa na vinywaji pamoja na uchomaji nyama 

Nyote Mnakaribishwa!

**********wavuti.com imeshirikishwa taarifa hii na Chief wa SwahiliVilla blog

Luis Suarez 'bites' Giorgio Chiellini in 2014 FIFA World Cup

He did it a third time!

In the 81st minute of the match between Italy and Uruguay in the FIFA World Cup Brazil 2014, Luis Suarez leaned in and appeared to bite Italian defender Giorgio Chiellini: "Suarez clearly bit the Italy defender as the two tussled in the penalty area, but Mexican ref Marco Rodriguez missed the incident."


Suarez then feigned injury in the aftermath and was not carded, but "[he] may not be so lucky with FIFA's disciplinary panel, who could hand a significant ban to the 27-year-old following his latest act of thuggery."
It's not even the first time he's been accused of biting someone. Sports psychologist Dr Fawcett told the BBC in April 2013, after the Ivanovic bite incident, that Suarez couldn't help it, and would do it again within five years. "It's in the man," he says. "I would think that in five years' time if there was a certain nerve hit or chord rung with Suarez in a different situation he would react in the same way."

Nafasi ya kutafsiri Video za mkutano wa TED kwenda Kiswahili‏‎

Habari zenu wadau,

Kwa wale ambao hawalifahamu hili ni kwamba kuna mkutano ambao umekuwa maarufu sana duniani unaitwa TED (TED: Ideas worth spreading), mkutano huu unakusanya wataalamu wa kada mbalimbali kujadiliana kuhusu jinsi ya kutatua na kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.

Mijadala hii inarekodiwa katika video ambazo mtu yeyote anaweza kuziangalia, lakini mara nyingi lugha inayotumika katika mijadala hii ni kiingereza. Ili kuweza pia

Manispaa ya Ilala yasaini Mkataba wa bilioni 2.1/= kwa ajili ya mradi wa maji KIvule na Kipunguni

Mkandarasi wa Kampuni ya JP Traders (wa pili kutoka kushoto) akitia sahihi mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji baina yake na Manispaa ya Ilala. Kulia ni mwanasheria wa Manispaa ya Ilala, Mashauri akihakiki na kutia sahihi mikataba hiyo.

Sensei Rumadha Fundi azidi kupanda thamani Kimataifa

Azidi kunoelewa na Wataalam wa Kijapani katika

Houston, Texas, USA.

Si Mwingine bali yule yule mtaalam wa michezi ya karate wa kimataifa Sensei Rumadha Fundi aka Sensei Romi,kutoka Uswahilini mwenye makao yake mjini Texas,Marekani,juzi tarehe 21 Juni 2014 alikuwa miongoni mwa wataalam wa kimataifa walio teuliwa kushiriki seminar maalumu ya "Japan Karate-Do Federation KATA SEMINAR " iliyoendeshwa na wataalamu walimu mabingwa kutoka Okinawa,Japan. Semina hiyo ilifanyika katika University of St. Thomas, Houston,Texas,nchini Marekani.

Sensei Rumadha Fundi ni mwafrika pekee aliyeteuliwa kushiriki katika seminar hiyo. mtaalam huyu Sensei Rumadha Fundi mwenye mkanda mweusi na 3 Dan,ambaye pia ni mtaalam wa ngazi ya juu wa mazoezi ya Yoga, anatarajia kuongezewa dan nyingine kutoka kwa baraza la utawala la mchezo huo lenye makao makuu yake kule OKINAWA, JAPAN.

Sensei Rumadha Fundi, katika "Japan Karate-Do Federation KATA SEMINAR" iliyofanyika Jumamosi 6/21/2014 katika University of St. Thomas, Houston, Texas chini ya Master Sensei Masataka Muramatsu Dan 8 ( Hanshi), master Tatsuo Takegawa Dan 7 ( Kyoshi), kutoka Japan na washiriki kutoka Marekani, Mexico na bara la Ulaya chini ya uandalizi wa Sensei Ramon Veras Dan 6 wa Houston, Texas, USA.

pamoja na master Muramats
pamoja na master Muramatsu

sensei Muramatsu na Sensei Tatsuo Takegawa toka Japan
sensei Muramatsu na Sensei Tatsuo Takegawa toka Japan


Sensei Rumadha na Sensei Ernie Salinas
Sensei Rumadha na Sensei Ernie Salinas

Washindi TMT kutoka Nyanda za Juu Kusini wawasili Dar es Salaam

Washindi wa Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini wakibadilishana mawazo wakati walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Nyerere, Jijini Dar es Salaam jana.

Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited Dar es Salaam.

Washindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kutoka kanda zote za Tanzania wamewasili jijini Dar es Salaam jana kwaajili ya kuingia kambini tayari kwa Kuanza safari ya kushindania kitita cha shilingi milioni 50 za Kitanzania katika fainali ya Shindano la TMT itakayofanyika mwishoni mwa mwezi wa Nane.

Fainali hiyo ya aina yake inayotarajiwa kutoa mshindi mmoja mkubwa ambaye

For good apartments at Msasani, Mikocheni see Blue Mark Real Estate Co.


Sponsorship for Tanzanians in Health specialties

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA 

MINISTRY OF HEALTH AND SOCIAL WELFARE 

APPLICATION FOR SPONSORSHIP 

 The Ministry of Health and Social Welfare intends to sponsor candidate to pursue
 Postgraduate courses in various Health specialties for academic year 2014/2015

 ELIGIBILITY: 

 - Should be a Tanzanian Citizen.

 - Should have an admission letter for academic year 2014/2015 from a
 recognized university (attachment)