Majina ya vigogo 12 waliotimuliwa JNIA baada ya Dk Mwakyembe kupokea ripoti ya wala rushwa na wabughudhi abiria

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amewatimua vigogo 13 kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Afya na Ustawi wa Jamik atika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kuwarejesha kwenye wizara husika kwa hatua zaidi za kinidhamu na kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Dk. Mwakyembe alisema vigogo hao wamekuwa na tabia za kuomba rushwa na kubughudhi abiria.

Aliwataja vigogo waliong’olewa kuwa ni:-

Basi la Magereza lashambuliwa na wezi waliopora fedha gari jingine


Sehemu ya kioo cha pembeni cha karandinga la Jeshi la Magereza baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi leo katika barabara ya Mwai Kibaki jirani na Mayfair Plaza jijini Dar es Salaam.

Inasimuliwa kutoka bogu ya Michuzi kuwa:

...kuna gari ndogo ilikuwa inatokea njia ya Kawe kwenda Shopperz au ilikuwa inaelekea mjini kwa kutumia hii njia ya Mwai Kibaki road.

Hiyo gari ndogo ilipofika Maeneo ya Million Hairs Salon jirani kabisa na Regency park hotel ikakwama kwenye foleni ndefu sana. Nyuma ya hiyo gari ndogo

Taarifa ya Wizara kuhusu kujiua kwa Kaimu Balozi wa Libya nchini Tanzania

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo imepokea taarifa kutoka Ubalozi wa Libya hapa nchini kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya, Bwana Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi.

Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya saa Saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa Lbya.

Inataarifiwa kuwa Bwana Nwairat alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto. Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlipuko wa

[audio] Timbwili la wafanyakazi CloudsFM studioni mic zikiwa on & live on air

[audio] Mahojiano na Nuru The Light @ Kwanza Production

(picha: Bongo Celebrity) 

Karibu katika mahojiano kamini kati ya Kwanza Production na NURU THE LIGHT. Msanii, Mjasiriamali, Mtangazaji, Blogger na Mwanaharakati ambaye amekuwa mkarimu sana kujiunga nasi moja kwa moja kutoka Stockholm Sweden.

Kazungumza mengi ikiwa ni pamoja na alivyoanza muziki Kisha akagusia kuhusu onyesho lake la kwanza kabisa jukwaani. Na kama nilivyokuja kumtambua, ni mtu mwenye misimamo na anayejitambua, utamsikia msimamo wake awapo studio

Nikataka kujua pia, nini anaona kama tatizo kubwa kwenye muziki wetu? Haya ni machache kati ya mengi aliyozungumza nami JIUNGE NASI katika audio kwenye pleya iliyopachikwa hapo chini...

Lowassa katika Jubilei ya Uaskofu wa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa


Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wake,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.