“Kweli nategemea kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015”Nguvu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuzuia wimbi la wanachama wake kutangaza nia ya ‘kumrithi’ Rais Jakaya Kikwete, wakati akiwa bado madarakani, zinaonekana kufifia.

Baada ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, kufikia hatua hiyo, Balozi Ali Abeid Amani Karume ambaye ni mtoto wa pili wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, amezungumza na NIPASHE Jumamosi mjini hapa, na kusema ameshajiandaa kuiomba CCM impitishe kuwania kiti hicho kwa sababu ana uwezo na sifa zinazostahili.
“Kweli nategemea kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,”
 alisema Balozi Karume.

Kwa mara ya pili kwa Balozi Karume ambaye ni kaka wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid

Serikali yatekeleza hoja ya Mch. Msigwa

Hatimaye serikali imetekeleza hoja ya Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa, kuhusu kuwafutia leseni za umiliki wawindaji wanaokiuka sheria za nchi.

Tayari, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ametangaza kufuta umiliki wa vitalu vyote vilivyopo chini ya kampuni ya uwindaji ya Green Miles Safaris Ltd, kwa kukiuka Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori nchini.

Uamuzi huo wa serikali ulitangazwa jana na Nyalandu, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Nyalandu alisema kuwa uamuzi huo wa serikali, ni onyo kwa kampuni za uwindaji wa kitalii zinazokiuka sheria, kanuni na utaratibu za nchi.

Alivitaja vitalu ambavyo umiliki wake ulifutwa kuanzia jana kuwa ni

Tanzania's lake Natron in CNN's list of World's strangest lakes

Lake Natron in Tanzania

Lake Natron, Tanzania -- Lake Natron adds new meaning to the idea of preserving wildlife; it literally turns animals into stone. Perfectly petrified bats and birds (even doves) have been found washed ashore, as if they've suffered the cursed fate of looking into the eyes of the Greek Gorgon Medusa.

The forbidding lake, whose temperatures can reach 140 degrees, developed its rare calcifying powers from toxic ash emitted by surrounding volcanoes. No one is sure exactly how the animals die, but it is thought that the lake's tremendously reflective surface tricks birds into taking a dive...from which they never recover.

photo: scienceyoucanlove.tumblr.com

photo: actionchallenge.com

WB to help children learn more in School through “BRN” Tanzania

WASHINGTON, July 10, 2014—The World Bank Group’s Board of Executive Directors has approved support for Tanzania’s “Big Results Now in Education” program, which aims to raise the quality of education in the country’s primary and secondary schools. The Board also approved further support to the ongoing Science and Technology Higher Education project which is helping produce more highly-skilled workers who can meet the needs of a fast-growing economy and help to sustain economic growth.
With millions more children enrolled in schools in Tanzania over the

Waziri Nyalandu atoa fedha na mabati kwa ajili ya maabara ya shule

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Iddy Mnyampanda akizungumza shule ya sekondari Kinyeto.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Iddy Mnyampanda akizungumza shule ya sekondari Kinyeto.

Na Hillary Shoo, SINGIDA -- Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mkoani Singida, Lazaro Nyalandu ametoa mchango wa mabati 420 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa shule mbili za sekondari za Kata za Mtinko na Kinyeto.

Mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Jimbo hilo kuchangia katika ujenzi wa maabara mbalimbali kwenye shule za sekondari za Jimbo hilo.

Akikabidhi msaada huo kwa Niaba ya Nyalandu ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii,

Daktari bandia akamatwa Hospitli ya Rufaa Morogoro

...akificha uso kukwea kamera.

Mtu mmoja kwa jina la Karume Habibu (22) amekamatwa katika Hospitili ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo kwa tuhuma ya kosa la kutoa huduma ya kitabibu kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo. -- via GPL.


...akiongozwa kuelekea kwenye gari.

Baadhi ya wafanyakazi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro wakishuhudia tukio hilo.

LeBron James goes back home to Cleveland, re-joins The Cavaliers

LeBron James
LeBron James 

LeBron James "LBJ" aka "King James" has announced that he is going back to his home state of Ohio and re-joining the Cleveland Cavaliers. The NBA superstar wrote in a piece for Sports Illustrated: "going home". The King opted out of his contract with the Heat after spending four seasons in Miami, where he won two championships. James, 29, played for Cleveland for seven seasons before leaving the town, and his home state of Ohio, for Miami.

Click here to read 5 rreasons why LeBron James is going back to Cleveland

Meneja fastjet atuhumiwa kupendelea Wakenya, kufukuza Watanzania

Meneja Bishara wa Kampuni ya Ndege ya Fastjet, Jean Uku, raia wa Kenya, ameingia katika kashfa ya kufukuza wafanyakazi (20) wa Kampuni hiyo ‘Watanzania’ bila kufuata utaratibu.

Kwa mujibu wa FikraPevu, taarifa zilizoifikia leo Ijumaa Julai 11, 2014 zinasema kuwa Meneja huyo pia anatuhumiwa kufanya kazi na kuishi nchini Tanzania bila kibali.

Baadhi ya wafanyakazi (majina yamehifadhiwa na FikraPevu) wakiwemo waliofukuzwa wamesema wenzao wawili wamefukuzwa kazi mbele ya wateja, kwa maneno makali na kisha kupewa barua:
“Tunazo taarifa kuwa hana kibali cha kufanya kazi na kuishi nchini pia ananyanyasa Watanzania sana leo asubuhi amefukuza wafanyakazi wawili 'Watanzania' mbele ya abiria katika Ofisi za mauzo zilizopo mtaa wa Samora asubuhi pamoja na Wafanyakazi wengine wa kitengo cha Rasilimiali Watu. Hadi sasa hivi kuna mtu anayejaza hiyo nafasi na vitengo vingine.”

Aidha, wamesema wanaiomba serikali na vyombo vinavyohusika kuingilia kati suala hilo ili kuwepo usawa na haki, kwani amekuwa akifanya vitendo hivyo wakati ambao Wakurugenzi wa Kampuni hiyo hawapo nchini na kutumia madaraka yake vibaya na kupendelea wafanyakazi ambao wanaotokea nchini Kenya.

For $128 million, Liverpool FC lets Suarez join Neymar, Messi in BarçaLuis Suarez, the Uruguayan striker who became headline news after biting fellow players in the pitch in the Netherlands (2010), England (2013) and during the World Cup in Brazil (2014), is moving to play for Barcelona, after the team reached terms with Liverpool in a transfer widely reported at 75 million pounds, or more than $128 million.

The transfer fee is simply for the sale of Suarez's contract.

Suarez, 27, will reportedly sign a 5-year deal with Barcelona, where he'll join elite players Neymar of

UN kusaidia Uchumi wa Kijani katika Hifadhi Hai ya Usambara Mashariki

Jamii zinazoishi katika Hifadhi Hai ya Milima ya Usambara Mashariki zinatarajiwa kukuza uwezo wao wa kutumia rasilimali zao za asili kwa njia endelevu.

Kupitia mradi wa UNESCO wa Shilingi za Tanzania milioni 700, "Uchumi wa Kijani katika Hifadhi Hai" unaofadhiliwa na KOICA (Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea), wananchi watapunguza utegemezi wao wa kiuchumi kwa kukata miti.

Mradi pia utasaidia kuchangia ulinzi wa Hifadhi Hai ya Milima ya Usambara Mashariki na kupanua shughuli za kiuchumi kwa ajili ya kupunguza umaskini na matumizi mazuri ya maliasili.

Baadhi ya shughuli za mradi huo kwa ajili ya kujenga uwezo zinahusisha mafunzo ya aina tatu kwa

Shabiki aliyesinzia kiwanjani adai fidia $10 milioni

Shabiki mmoja wa timu ya New York Yankees huko Marekani amekishitaki kituo cha habari cha ESPN akidai fidia ya dola za Kimarekani milioni 10 kwa madai ya kukashifiwa.

Jamaa huyo, ANdrew Robert Rector aliyenaswa na kamera za televisheni akiwa ameuchapa usingizi wakati wa mechi Aprili 13 kati ya Boston REd Sox na Yankees anadai kuwa watangazaji Dan Shulman na John Kruk walitamka maneno ya kumdhalilisha na kumshushia heshima, kama vile 'mnene' na 'mjinga', ndiyo maana amewashitaki. Lakini, ajabu ni kuwa maneno hayo hayasikiki kwenye video ambayo nakala yake ipo katika tovuti ya YouTube.

Rector pia anadai kuwa watangazaji hao walitumia maneno hayo kumaanisha kuwa yeye ni mfano wa watu waliofeli na wasioijua historia ya timu hizo mbili mahasimu, kiasi cha kuthubutu kulala kiwanjani huku mechi ikiendelea.

Hii ndiyo sababu Rector anadai kuwa amedhalilishwa na kuumizwa kiakili kiasi cha kushindwa kwenda kazini na kujiingizia kipato kwa maisha ya baadaye.

Mama wa Rector ameiambia New York Post kuwa kesi hii onyo kwa wapuuzi ambao wanapaswa kutojihusisha na maisha binafsi ya watu na kuwakejeli watu wasio na madhara yoyote kwao.

Kongamano la IV la Makatibu Muhtasi lafunguliwa Mwanza

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA), Mhe. Dk. Mary Nagu akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Nagu katika hotuba yake,amesema atawasimamia Makatibu hao na kuhakikisha wanaanzisha Benki yao ambayo itawawezesha kuweka abiba zao na kukopeshana pia. (picha zote: Othman Michuzi).

Mgeni Rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Angela Kairuki akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania, leo Julai 11, 2013 jijini Mwanza. Mhe. Kairuki amewahimiza Makatibu Muhtasi hao kuhakikisha wanaudumisha na kuulinda umoja walionao,kwani umoja ndio msingi wa maendeo.