Mahojiano na washiriki wa maonesho ya Utamaduni wa Kenya hapa Washington DCKati ya Juni 25 na Julai 6, jiji la Washington DC lilikuwa mwenyeji wa maonesho ya kila mwaka ya yanayohusu maisha a watu na jamii mbalimbali.

Mwaka huu, nchi ya Kenya ilishirikishwa, wakionyesha utamaduni wao na changamoto za kuzidumisha katika zama hizi za sayansi na teknolojia.

Kwanza Production ilipata fursa ya kutembelea maonesho hayo na kuzungumza na baadhi ya washiriki wa maonesho hayo ambapo walieleza mengi ya kufurahisha.

Karibu uungane nasi...

[audio] Kafulila, Zitto, Mwakatobe katika mjadala kuhusu Escrow ya IPTL; Waziri Muhongo 'ahepa'

Kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow inazidi kuchukuwa nafasi nchini Tanzania baada ya bunge la nchi hiyo kumtaka Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Tanzania na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza uchotwaji wa shilingi bilioni 200.

Maoni mbele ya Meza ya Duara ya Idhaa y Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle - DW) inauliza ikiwa upo uwezekano wa bunge la Tanzania kuwa taasisi imara kusimamia fedha za umma na rasilimali za nchi. Je, upo uthubutu na utayarifu huo?

Kwenye Meza ya Duara ni David Kafulila, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini aliyeibua kadhifa hii Bungeni kwa mara ya kwamza, Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kusimamia Mahesabu ya Serikali, Gwapo Mwakatobe mchambuzi wa masuala ya siasa na uchumi akiwa Mwakaleli, Mbeya na mwananchi Rutaraka A., anayefuatilia kwa karibu masuala ya nchi yake, Tanzania.

Anayekosekana ni Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo ambaye alialikwa na DW katika Meza ya Duara lakini amenukuliwa kuwa alijibu mwaliko kwa kusema kuwa haoni kama "...huu ni mjadala ambao una maslahi kwa ujenzi wa nchi" yake.

Susikiliza audio ya majadiliano haya...


Your browser does not support html audio tag?

Pakua audio: hapa (DW Swahili)

Kashfa dhidi ya Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili

Kashfa za ufujaji na matumizi mabaya ya fedha zinazomhusu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili zimeendelea kuibuliwa, wakati tanuru la kuchomea taka likiwa halijapatiwa ufumbuzi.

Licha ya hospitali hiyo kuwa taabani kifedha, kukosa vitendea kazi na wataalamu, Mkurugenzi Mtendaji Dk.Marina Njelekela, anatuhumiwa kufuja fedha kwa kujilipa posho nyingi kinyume cha sheria.

Vyanzo vya kuaminika ndani ya hospitali hiyo, vimeiambia NIPASHE Jumapili kuwa, licha ya Njelekela, kununua gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 kwa Sh. milioni 207, fedha zilizolipwa kwa kampuni ya Toyota Tanzania kupitia hundi namba 117781 ya PV P3-13-001697 ya Mei mwaka huu.
“Tangu Mkurugenzi huyu ameingia Muhimbili, amekuwa akikiuka kanuni za fedha, baada ya kuona watu wanamshtukia anamtumia katibu muhtasi wake kuchukua fedha za posho za safari anazozipanga mwenyewe akijua kuwa hazina tija,” 
kilidokeza chanzo kimoja.

Baadhi ya fedha zilizodaiwa kuchukuliwa na mkurugenzi huyo ni kupitia hundi yenye namba

Rais Kikwete aingia mtaani na kununua samaki gengeni

RAIS Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakinunua samaki katika kibanda, katika Kijiji cha Bweni, Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, juzi, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara Shuke ya Sekondari Kipumbwi. (picha: Freddy Maro/Ikulu)

Kafulila kupandishwa kortini na IPTL itakayomdai bilioni 310/=

Gazeti la Uhuru limechapisha habari kuwa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL), inayotuhumiwa kuchota fedha katika akaunti ya Escrow, imeamua kumfikisha mahakamani Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na kumfungulia kesi ya madai ya sh. bilioni 310.

Gazeti hilo linasema kuwa IPTL kwa kushirikiana na Kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited na Mtendaji Mkuu wa kampuni hizo, Harbinder Sign Seth, wamemburuta Kafulila katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kutokana na kashfa anazodaiwa kuzitoa juu ya kuchotwa fedha katika akaunti ya Escow isivyo halali.

TAARIFA KWA KINA KUTOKA KATIKA GAZETI LA HABARILEO

Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), imemfungulia kesi Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ikimtaka aombe radhi na kulipa fidia ya Sh bilioni 310.

Katika kesi hiyo ya madai, Kafulila anadaiwa kuidhalilisha kampuni hiyo, kutokana na

Taarifa ya Bodi HESLB ya nyongeza ya muda wa maombi ya mkopo

MUDA WA NYONGEZA KWA WAOMBAJI MIKOPO AMBAO HAWAKUJAZA FOMU ZA MAOMBI YA MIKOPO KABLA YA JUNI 30, 2014


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza na Umma kwa ujumla kwamba muda wa maombi ya mikopo umeongezwa kwa mwezi mmoja kutoka Julai 1, 2014 hadi Julai 31, 2014.
Bodi ilianza rasmi kupokea maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao kuanzia Aprili 23, 2014 ambapo tarehe ya mwisho wa kupokea maombi hayo ilikuwa Juni 30, 2014.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa muda wa nyongeza kwa waombaji wa

Rais Kikwete katika sherehe za miaka 75 ya Kanisa la TAG

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi kwenye  kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa la Tanzania Assemblies of God  katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi kwenye kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014. (picha zote, melezo: Ikulu)

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 75 YA KANISA LA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD, UWANJA WA SOKOINE, MBEYA, TAREHE 13 JULAI, 2014


Dkt. Barnabas Weston Mtokambali, Askofu Mkuu wa
Tanzania Assemblies of God;
Ndugu Mkuu wa Mkoa;
Maaskofu na Wachungaji Wote Mliopo Hapa;
Viongozi Wenzangu;
Ndugu Waumuni;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;

Pongezi na Shukrani

Nakushukuru Baba Askofu Mkuu kwa kunialika kwenye sherehe zenu za kuadhimisha ya miaka 75 ya uhai wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG). Tukio hili ni muhimu sana kwa maisha ya kanisa lenu na Taifa letu pia. Hii ni miaka 75 ya upendo, uponyaji na uenezaji wa injili nchini. Pia ni miaka 75 ya kueneza dini bila kufarakana na dini nyingine na madhehebu mengine ambayo mliyakuta na yale yaliyowakuta. Sote bila kujali tofauti zetu za kidini na madhehebu tuliyopo tumefaidika na uwepo wenu. Kazi yenu na huduma zenu za kiroho na kijamii mnazozitoa kwa watu wote bila ubaguzi, zimewanufaisha Watanzania wengi.

Naungana na Watanzania wote kukupongeza Baba Askofu, viongozi wa kanisa unaloliongoza na waumini wote wa kanisa hili kwa kutimiza miaka 75. Katika miaka hii 75 mmetimiza matarajio yetu na sote tumefurahia kazi yenu. Umri huu ni mkubwa wa kutosha hivyo ni sahihi kabisa kusema kuwa kanisa hili limeota mizizi na kukomaa. Inafurahisha pia kwamba, mmeendelea kuonyesha ukomavu huo, hekima na busara katika kuchangia kudumisha amani, upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania. Daima mmekuwa wamoja wetu, miongoni mwetu na ndio sababu nasi tunajiona kuwa sehemu kamili ya miaka 75 ya mafanikio ya kanisa lenu. Ndiyo maana pamoja na mambo mengine nimetafuta wasaa kuja kuungana nanyi kusheherekea miaka 75 ya uwepo wenu, na kuwatakia mafanikio makubwa zaidi katika kazi yenu adhimu ya kueneza neno la Mungu.

Uimara wa Kanisa la TAG

Nakupongeza Baba Askofu Mkuu kwa maelezo yako mazuri kuhusu historia ya kanisa hili hapa nchini. Umesema kwamba misingi na nguzo sita za kanisa lenu zimeliwezesha kufikia umri huu kwa mafanikio ya kujivunia. Umezitaja nguzo hizo kuwa ni Ibada; Elimu rasmi ya Kiroho; Utumishi; Uinjilisti; Mfumo wa Kanisa la kienyeji lenye kujitegemea na kuongozwa na maono. Uimara wa nguzo hizi unadhihirishwa na kuthibitishwa na mafanikio makubwa ambayo kanisa lenu limepata.
Inatupa moyo na matumaini makubwa tunaposikia ukiendelea kusisitiza umuhimu wa nguzo hizi sita. Tunafurahia kwa kuwa unazidi kutuhakikishia nia na dhamira njema ya kanisa unaloliongoza katika kudumisha upendo, umoja, amani na kupanua huduma za kiroho na kijamii nchini. Pia, unatupa sababu ya kuziangalia nyakati zilizo mbele yetu kwa matumaini makubwa.

Mabadiliko ya Kijamii na Changamoto za Leo za Dini na Kanisa
Baba Askofu,
Wageni Waalikwa,
Tunasherehekea miaka 75 ya kanisa hili katika mazingira tofauti sana na yale yaliyokuwepo nchini lilipoanzishwa rasmi mwaka 1939. Idadi ya watu ilikuwa ndogo, hali kadhalika idadi ya madhehebu na changamoto za kueneza neno la Mungu nazo zilikuwa ndogo. Kazi kubwa na nzito ilikuwa ni katika kuwafikia wananchi walio wengi ambao wengine hawakuwa wamefikiwa na huduma za Kimisionari na Kiinjili. Ukubwa wa kazi hii haukutokana na ugumu wa watu kupokea huduma ya neno la Mungu bali miundombinu ya kuwafikia huko waliko. Ingawa wananchi wengi walikuwa wakiamini katika dini zao za asili, imani yao kwa Mungu na uadilifu katika maisha yao vilikuwa ni vitu ambavyo vikijidhihirisha katika maneno, mienendo na matendo yao. Vitu hivi viwili, yaani imani na uadilifu vilifanya kazi ya Kanisa kueneza neno la Mungu kuwa nyepesi.

Leo, miaka 75 baadae, nchi yetu imepiga hatua kubwa ya maendeleo. Idadi ya watu imeongezeka, idadi ya waumini imeongezeka, idadi ya madhehebu imeongezeka sana, hali kadhalika idadi ya Maaskofu na siku hizi nasikia kuna hata Manabii. Katika hali ya kawaida, tungetegemea kuwa maovu katika jamii yetu yangepungua sana. Maana, leo tunazo nyenzo za kisasa zaidi za kufanya kazi ya kueneza neno la Mungu. Tunazo televisheni, redio, barabara nzuri, waumini wenye uwezo zaidi kifedha na kielimu. Kinyume chake maovu katika jamii yameongezeka sana kiasi cha kushuhudia hata yale maovu ambayo hatukuwahi kuyafikiria. Baadhi ya hayo hufanywa hata na wale waliopewa dhamana ya kulea watu kimwili na kiroho.

Mmong’onyoko wa maadili umezidi kuwa mkubwa, upendo na kuaminiana kunapungua miongoni mwa wanadamu siku hadi siku. Watu wanazungumzia visasi, kumwaga damu, kutiana vilema, kudhulumiana na kufarakana. Wakati mwingine sisi Serikalini tumekuwa tunalazimika kubadili Sheria na kutunga Sheria kali zaidi. Kwa mfano, tumeongeza idadi ya makosa katika Sheria ya Rushwa kutoka makosa 4 hadi 24, kutunga Sheria ya Makosa ya Kujamiiana (SOSPA) yenye adhabu ya kifungo cha maisha na nyinginezo nyingi. Hivi sasa, tunajiandaa pia kutunga Sheria kali ya kupambana na biashara ya dawa za kulevya. Hata hivyo, idadi ya makosa haijapungua na Magereza yanaendelea kujaa, tena basi, wafungwa na mahabusu walio wengi magerezani ni waumini wa dini zetu kubwa mbili za Ukristo na Uislamu.

Msingi wa Dini ni Imani
Askofu Mkuu,
Wageni Waalikwa;
Nyakati tulizonazo leo zinatutaka sote tufikiri na tuenende tofauti na mazoea yetu. Tunapaswa kutazama upya namna Serikali, Dini na Jamii zinavyowaandaa na kuwalea watu wake kiroho, kielimu na kimaadili. Maana kwa jinsi mambo yalivyo leo, ni dhahiri kuwa kuna mahala ama tumepotoka au tumekosea. Ili kutoka hapa tulipo, hatuna budi Serikali, Dini zetu na Jamii kushirikiana kwa karibu kwani hakuna mmoja wetu anayeweza kuwa na majawabu peke yake. Maana, ukamilifu wa mwanadamu ni kukamilika kwa afya ya mwili, akili na roho.

Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipotambua mchango wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) katika sekta za elimu na maji. Tunawashukuru kwa kujitoa kwenu kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutimiza wajibu wake wa kutoa huduma hizi muhimu za jamii. Kuwepo kwa shule za seminari za Faraja kule Kilimanjaro, Ebenezer kule Iringa na sasa kule Eyasi kunasaiadia kutoa fursa kwa watoto wa Kitanzania kupata elimu na maarifa bora. Nimefurahishwa pia na taarifa za mchakato wa kujenga vyuo viwili vya ualimu na miradi ya visima virefu vya maji huko Dodoma, Singida, Same na Manyara. Hatuna maneno ya kutosheleza kuelezea shukrani na furaha zetu kwa mchango wenu huu mkubwa. Nasema asanteni sana. Mola awaongezee maradufu pale mlipopunguza.

Ahadi ya Serikali kwa Kanisa
Sisi kwa upande wa Serikali tunayo dhamira ya dhati ya kutimiza ule wajibu wa kutoa elimu ya hapa duniani, kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kijamii na kutunga Sheria na kuunda taasisi za kusimamia sheria hizo. Tunaahidi kuendelea kuhakikisha mazingira mazuri ya kuwawezesha viongozi wa dini na taasisi za dini kutekeleza wajibu wenu wa kujenga watu wetu kiroho. Tutaendelea kuheshimu na kulinda uhuru wa kuabudu na ule wa kuendesha shughuli za kidini. Tunaahidi pia kuendelea kushirikiana na dini zote katika shughuli za kuwaletea maendeleo Watanzania na katika kudumisha amani, umoja na mshikamano. Sisi sote tunayo kazi moja tu ya kuwahudumia wana kondoo wa Bwana. Tofauti yetu ni aina ya huduma. Ninyi za kiroho na sisi za mahitaji yao ya maisha yao duniani. Tunajenga nyumba moja, hatuna sababu ya kunyang’anyana fito.

Ombi kwa Viongozi wa Dini
Ombi langu kwenu, nawaomba mtusaidie sana kujenga imani miongoni mwa watu wetu. Historia ina mifano na mafunzo mengi kuwa dini pekee bila imani haitoshi. Kwa kivuli cha dini, maovu mengi yamefanyika na damu imemwagika. Watu wabaya wametumia mwamvuli wa dini kueneza chuki na kuchochea mifarakano katika jamii. Tusiruhusu hali hii ikaendelea katika jamii zetu. Turejeshe imani miongoni mwa jamii yetu, kwa kutoa msisitizo katika kulea mioyo ya watu wetu. Jamii yenye watu wenye imani, watu hupendana, husikilizana, husameheana na huishi kwa amani. Tukifika hapo, hata sheria na taasisi zetu za kusimamia sheria na kutoa haki zitapungukiwa na mzigo mkubwa zinazoubeba leo.

Katiba Mpya
Baba Askofu Mkuu;
Ndugu Waumini;
Baba Askofu Mkuu ameelezea masikitiko ya Kanisa lenu kuhusu kukwama kwa mchakato wa Katiba, na ametoa rai kwa wadau wote kurejea Bungeni mapema mwezi ujao. Masikitiko yenu ndiyo masikitiko yangu na ndiyo masikitiko ya Watanzania wote. Rai yenu ndiyo yangu na ndiyo ya Watanzania wote ambao matumaini yao wameyaweka kwenye mchakato huo kuwapatia Katiba mpya inayolingana na wakati tulionao na mbele tuendako. Nafarijika kusikia kuwa nanyi viongozi wetu wa dini mkizisihi pande zote kurejea Bungeni na kumaliza tofauti zao kwa mazungumzo ndani ya Bunge. Hamko peke yenu. Watu wengi wameelezea umuhimu wa Wajumbe kurejea Bungeni. Wametumia hoja mbalimbali na kuelezea mantiki zenye kushawishi wale waliotoka Bungeni kurejea bila mafanikio. Pengine mkisema ninyi watu wa Mungu na kuzungumza na mioyo yao wataitikia na kuwasikia.
Napenda kuwahakikishia kuwa matumaini yenu ndiyo matumaini yangu, na ndiyo matumaini na matarajio ya Watanzania wenzetu wengi, kwamba tupate Katiba Mpya. Wakati mwingine nia hii njema imekuwa ikipotoshwa kwa makusudi. Napenda kurudia na kusisitiza kuwa nilibuni wazo na kuanzisha mchakato huu kwa lengo la kuwapatia Watanzania Katiba Mpya iliyo bora zaidi ya tuliyonayo sasa. Tulitengeneza misingi mizuri ya kutufikisha hapo. Kama mtakavyokumbuka, tulianza kwa kutunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Pamoja na changamoto zilizokuwepo wakati wa mchakato wa kutunga Sheria hiyo, tarehe 18 Novemba, 2011, Bunge la Jamhuri ya Muungano likapitisha Sheria hiyo. 

Kwa mujibu wa Sheria hiyo, mchakato wa kuunda Katiba Mpya ulipangwa kuanza kwa kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Tume hiyo ilipewa jukumu la kusikiliza maoni ya wananchi na taasisi mbalimbali katika jamii, kisha kutengeneza Rasimu ya Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi pamoja na utafiti na maoni ya Tume. Baada ya Tume kukamilisha kazi yake, Sheria imeagiza kuwa Rasimu hiyo ifikishwe kwenye Bunge Maalumu la Katiba kujadiliwa na Katiba Mpya kutungwa. Ukamilifu wa mchakato wa kupata Katiba mpya ni pale itakapopitishwa na wananchi, ambao ndiyo wenye mamlaka ya mwisho kuhusu Katiba hiyo kwa kupiga kura. Mchakato utahitimishwa kwa wananchi kupiga kura ya maoni.

Baba Askofu Mkuu;
Kama sote tujuavyo, tarehe 18 Februari, 2014 Bunge Maalumu la Katiba lilianza kwa kuchagua Mwenyekiti wa Muda, kuapisha Katibu na Naibu Katibu kisha kuwaapisha Wajumbe. Baada ya hapo ilifuatia kazi ya kutunga Kanuni za kuendesha Bunge lenyewe. Walipomaliza kutengeneza Kanuni wakachagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo. Lakini kabla ya kuanza kazi ya kujadili Rasimu ya Katiba walimalizia mjadala wa jambo waliloliacha kiporo kwenye Kanuni ambalo lilihusu upigaji wa kura uweje: wa Siri au Wazi. 

Askofu Mkuu na Ndugu Waumini;
Baada ya kukamilisha Kanuni, ndipo tarehe 18 Machi, 2014 Mwenyekiti wa Tume alipowasilisha Rasimu ya Katiba Mpya katika Bunge na tarehe 21 Machi, 2014 nililizindua rasmi Bunge Maalumu la Katiba. Baada ya hapo ndipo Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walianza kazi ya kujadili Rasimu. Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Maalumu, Wajumbe waligawanywa katika Kamati 12 ili kutoa muda wa kutosha kwa Wajumbe kutoa maoni yao kuhusu vifungu mbalimbali vya Rasimu.
Kwa uamuzi wa Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walikubaliana kuanza Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu. Busara iliwatuma wafanye hivyo kwa sababu hizo ndizo sura mama za Rasimu, kwani ndizo zinazotambulisha na muundo wa Muungano. Sura nyingine zilizosalia zinahusu namna ya kuendesha shughuli mbalimbali za taifa na za Serikali ambazo zinatawaliwa na aina ya nchi na Muundo wa Muungano tuutakao. Walikubaliana kuwa watumie siku 14 katika Kamati kisha warudi kwenye Bunge zima kupokea taarifa ya maoni na mapendekezo ya kila Kamati. Katika kuwasilisha taarifa walikubaliana katika Kanuni kuwa maoni ya wengi yatawasilishwa kwa dakika 40 na maoni ya wachache kwa dakika 20. Aidha, kwa upande wa wachache walipewa dakika nyingine 30 kutoa ufafanuzi wa maoni yao. Kwa maneno mengine walio wengi wamepewa dakika 40 kutoa maoni yao na wachache dakika 50 za kutoa maoni. Hivyo basi, Kanuni zimetoa fursa ya kutosha kwa kila upande kutoa maoni yake na upande wa Kamati ya upinzani wamepewa dakika 10 zaidi ya upande wa Chama tawala.

Baadhi ya Kamati ziliongezewa muda baada ya kushindwa kumaliza kazi ndani ya siku 14. Kwa sababu hiyo ilichukua siku 19 kwa Kamati zote kumaliza kazi ya kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu. Kila Kamati ilipiga kura kwa utaratibu wa kura za Wajumbe wa Tanzania Bara na Zanzibar wakipiga kwa upande wao. 

Baada ya hapo, tarehe 10 Aprili, 2014, Bunge Maalum la Katiba lilikutana tena katika kikao cha Wajumbe wote na kuanza kupokea taarifa za Kamati. Ilipofika tarehe 13 Aprili, 2014 taarifa za Kamati zote 12 zilikuwa zimewasilishwa kwa maana ya maoni ya wengi na ya wachache. Tarehe 14 – 25 Aprili, 2014 mjadala wa taarifa za Kamati uliendelea Bungeni. Katika hali isiyokuwa ya kutarajibiwa tarehe 16 Aprili, 2014 Wajumbe wa kutoka baadhi ya vyama vikiwemo vyama vya CHADEMA, NCCR Maguezi na CUF walitoka nje ya Bunge na kusema hawatarudi tena. Walitoa sababu ya kufanya hivyo ni lugha ya matusi na kejeli. Hawakutoa masharti ya kurudi. Hapo ndipo Bunge Maalumu la Katiba lilipoingia katika mgogoro uliopo sasa.

Baba Askofu Mkuu;
Baada ya taarifa ya Kamati zote 12 kupokelewa kinachofuatia, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Maalumu, ni Wajumbe kufanya uamuzi kwa kupiga kura kwa sharti la theluthi mbili ya Wajumbe wa kutoka pande zote mbili za Muungano kukubali. Hata hivyo, kwa mujibu wa Kanuni, kabla ya kufanya hivyo Bunge litapokea taarifa ya Kamati ya Uandishi kuhusu marekebisho ya kufanywa katika Sura hizo mbili. Kamati ina Wajumbe wa pande zote mbili za Muungano na kambi mbili za siasa na Wajumbe wa kutoka kundi la 201.

Kwa maneno mengine kazi ya msingi kuhusu Sura ya Kwanza na ya Pili imekwishafanywa. Kilichobaki ni kupiga kura. Kazi hiyo iko mashakani kwa sababu ya Wajumbe wa vyama hivyo kutoka Bungeni. Wakierejea na kura kupigwa mchakato utaingia hatua mpya. Na, iwapo watakubaliana kuhusu sura hizo mbili kazi iliyosalia haitakuwa na ugumu sana kama hii ya Muundo wa Muungano.

Baba Askofu Mkuu;
Bahati nzuri kuanzia wiki iliyopita wawakilishi wa vyama vya CCM, CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi wamekuwa wanakutana kwa juhudi za Msajili wa Vyama vya Siasa. Nimeambiwa bado wanaendelea na mazungumzo. Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa viongozi wa vyama hivyo kwa uamuzi wao wa kukutana na kuzungumzia namna ya kusonga mbele. Hivyo ndivyo uongozi unavyotakiwa kuwa. Tunatoa pongezi maalumu kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mheshimiwa Jaji Mutungi kwa kufanya uamuzi mzuri wa kuwakutanisha viongozi wetu hao.

Baba Askofu Mkuu;
Wageni Waalikwa;
Maombi yangu kwenu ni kuwaombea viongozi wetu wawe na mazungumzo mazuri na yenye mafanikio. Wakubaliane juu ya kuendelea na kuukamilisha mchakato katika siku 60 za nyongeza kuanzia tarehe 5 Agosti, 2014. Tuombe kwa nguvu zetu zote ili Bwana Mungu awaongoze viongozi hao wapate muafaka utakaoliwezesha taifa kupata Katiba mpya nzuri inayotekelezeka. Katiba itakayodumisha umoja, mshikamano na upendo miongoni mwa watu wa nchi yetu licha ya tofauti zetu za rangi, kabila, dini na maeneo tutokako. Katiba itakayodumisha amani na utulivu nchini na kuchochea maendeleo ya nchi yetu yatakayojumuisha na kunufaisha watu wote. Katiba itakayolinda haki za binadamu ikiwemo uhuru wa kuabudu.

Wakati nawaomba viongozi wa dini kuwaombea viongozi wa CCM, CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi wapate baraka na maongozi ya Mola wetu, nawaomba Watanzania wenzagu tuwape nafasi viongozi wetu hao wazungumze kwa utulivu. Hebu kwanza tuache maneno maneno yatakayowachanganya. Maana siku hizi wasemaji wamekuwa wengi na kauli nyingi na nyingine ni za upotoshaji na uchochezi. Kwa sasa tuwaache wazungumze. Tuwaombee wakubaliane kwani siyo tu tutapata Katiba bali pia tunaiepusha nchi yetu dhidi ya machafuko na kuvunjika kwa amani.

Hitimisho

Baba Askofu Mkuu;
Maaskofu, Wachungaji, Waumini naWageni Waalikwa;
Kwa kumaliza napenda kurudia kushukuru kualikwa katika siku hii adhimu. Mmenipa heshima kubwa ambayo nitaikumbuka daima. Ninawahakikishia ushirikiano wangu binafsi na ule wa Serikali ninayoiongoza katika kuwezesha Kanisa lenu kufanya kazi yake kwa ufanisi. Nimepokea maombi ya Kanisa kwangu kuhusu kiwanja, shule zilizotaifishwa na ukiritimba katika usajili wa shule za Kanisa. Nikiri kuwa, maombi haya yanatawaliwa na sheria, kanuni na taratibu hivyo, si rahisi kwangu kuyatolea amri ya papo kwa papo. Naahidi kuyachukua na kuangalia uwezekano wa kuyapatia majawabu. Nitawapeni majibu. Aidha, hongereni kwa kutimiza miaka 75 yenye mafanikio makubwa yanayoonekana. 

Asanteni sana kwa kunisikiliza.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha  Tanzania Assemblies of God (TAG) akiwa na  Askofu Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Weston Mtokambali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa hilo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014
Rais Kikwete akizindua kitabu cha TAG akiwa na Askofu Mkuu wa TAG, Dkt Barnabas Weston Mtokambali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 75 ya kanisa hilo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014

Rais Kikwete akikabidhiwa tuzo na Askofu Mkuu TAG, Dkt Mtokambali wakati wa kilele cha sherehe hizo.


IPTL yasaidia milioni 20/= kwenye maandalizi ya mashindano ya riadha

Makamu wa Rais-Utawala wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) William Kallaghe (wapili kushoto) akipokea sehemu ya fedha taslim Tsh milioni 20 zilizotolewa na kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kusaidia maandalizi ya mashindano ya mwaka huu ya Riadha ya Kitaifa yatakayoanza leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaaam. Kulia ni Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/ Pan African Power Solutions (PAP), Bw. Joseph Makandege, akifuatiwa na Msaidizi wa kampuni hiyo Rajiv Bhesania na kushoto ni Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui.

SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT) limepokea shilingi milioni 20 kutoka katika kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL) kwa lengo la kusaidia uandaaji wa mashindano ya Riadha ya Kitaifa yanayoanza leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui aliwaeleza waandishi wa habari kuwa fedha hizo zilipokelewa zitasaidia katika maandalizi ya mbio hizo kubwa za kitaifa ambazo zitatumika katika

UK Government marks 30 years of International scholarships


Tanzanian Deputy Permanent Secretary attends UK Government 30 years of International scholarships celebrations


On 9th July over 500 past and present Chevening Scholars representing 118 countries gathered at Chevening House to mark 30 years of the UK’s most prestigious scholarship programme and to invite the brightest graduates around the world to apply.

Deputy Permanent Secretary of the Ministry of Information, Youth, Culture and Sports, Prof. Elisante Ole Gabriel was chosen among the Chevening alumni to represent Tanzania in a historical event celebration.
“I have been lucky to be selected among the six (6) Chevening candidates in 1998 out of 9,000 applicants. The recruitment process of Chevening Scholarships is clean and professional. I benefited a lot from my experience, exposure and knowledge gained for the time I spent in the UK under Chevening scholarship. Therefore, I can boldly say, I am what I am today because of Chevening scholarship” 
said Prof. Elisante Ole Gabriel.

The event was hosted by Minister of State in the Foreign and Commonwealth Office, Hugo Swire.

The Chevening Scholarships Programme finances graduates from around the world with potential to be