Mwanafunzi mbaroni kwa utapeli akijidai "Ofisa Mpelelezi"

POLISI mkoani Rukwa inamshikilia mwanafunzi wa udereva katika Chuo cha Furaha Center katika eneo la Kantalamba Manispaa ya Sumbawanga, Clever Simfukwe (19) kwa tuhuma za kujifanya Ofisa Mpelelezi wa Polisi katika mikoa ya Rukwa na Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Frednand Rwegasira alisema Simfukwe alikamatwa jana saa 3:00 asubuhi akiwa karibu na Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Sumbawanga akiwa amechanganya mavazi ya sare ya polisi na nguo za kiraia.

Akizungumzia undani wa kukamatwa kwake, Rwegasira alidai kuwa ni kutokana na kupata taarifa za

Njoo uunge neno...


Majambazi yaiba kilo 40 za Tanzanite ya TanzaniteOne ya bilioni 10/=

Madini ya tanzanite ya Kampuni ya TanzaniteOne ya Mirerani, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara yenye uzito wa kilo 40 na thamani ya zaidi ya Sh bilioni 10 yameporwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.

Taarifa kutoka katika kampuni hiyo zilisema, uporaji huo ulitokea jana ndani ya kampuni hiyo saa tisa usiku.

Kwa mujibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Dauglas Swartz, tayari wafanyakazi watano wa kampuni hiyo wanashikiliwa na polisi katika kituo kidogo cha Mirerani kuhusu wizi huo. 

Alisema jana kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Manyara (RCO), Benedict Msuya alifika eneo la tukio kwa uchunguzi wa wizi huo.
“Ni kweli tumeibiwa madini ya tanzanite na baadhi ya wafanyakazi wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo wameshakamatwa na upelelezi bado unaendelea, niache kwa sasa,’’ 
Taarifa zilizopatikana ndani ya kampuni hiyo zinadai kwamba madini hayo yaliyokuwa yamefungwa katika mifuko miwili tofauti yenye uzito wa kilo 15 na kilo 25 na yameporwa mita chache kutoka mgodini eneo la kuingia chumba cha ulinzi. -- via HabariLeo

Ufafanuzi wa TFDA kuhusu taarifa za uwepo sokoni wa dawa zilizoisha muda wa matumizi

MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA

tfda tanzania logo


Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa zilizoripotiwa na gazeti la Tanzania Daima la kila siku kuhusu uwepo wa dawa zilizoisha muda wa matumizi kwenye duka la dawa la Core Pharmacy jijini Dar es Salaam. Taarifa hizi zimekuwa zikitolewa na mmiliki wa duka la dawa la Shine Care Pharmacy kwenye gazeti hilo. Baadhi ya dawa zilizotajwa ni Listerine antiseptic mouthwash, Pimple Gel, Misoprostol tablets 200mcg, Rabeloc IV 20mg, Mefenamic acidic tablets, Herpex – 800 DT, Inhaler 100 pg dose, Metformin Denk 850, Comprimes de carvediola 12.5mg na Cloderm cream.

Aidha, taarifa zimedai pia kuwa TFDA pamoja na kufahamishwa suala hili haikuweza kuchukua hatua zozote kwa mlalamikiwa.

TFDA inapenda kukanusha upotoshaji huo unaofanywa na chombo hicho cha habari kutokana na

Medical Specialty Training Positions in UK for Tanzania

Royal College of Physicians (RCP), in partnership with Physicians in Tanzania, is now accepting applications of interest to join the Medical Training Initiative (MTI) Scheme.

The MTI scheme offers the opportunity of up to 2 years clinical training and experience in UK National Health Service (NHS) hospital trusts for a small number of suitably qualified international medical graduates. https://www.rcplondon.ac.uk/medical-careers-training/international-medical-graduates/medical-training-initiative-mti

If appointed to a position after joining the scheme, doctors will be directly contracted to an

African wealthy individuals invited to invest in the USA and obtain US Green CardPRESS RELEASE

ArKay Beverages Inc. is Inviting African Wealthy Individuals to Invest in the USA and Obtain their US Green Card

If you are a foreigner investor and eligible, ArKay will help to get your US residence for you and your family

NEW YORK, July 17, 2014/ -- ArKay Beverages Inc. (http://shop.arkaybeverages.com), the world’s first maker of alcohol free liquors, is inviting African wealthy individuals to invest in the USA in a new concept of ArKay Non Alcoholic Bar & Lounge that will serve food and non-alcoholic cocktails during the day and transform itself in a fun place at night.

"The reason behind ArKay expansion into “the non-alcoholic bar and lounge market” is obvious,

TPDC: Kuhusu mkataba na StatOil

Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. James Andilile (kushoto) akijibu maswali toka kwa waandishi wa habari waliohudhuria Mkutano uliohusu Kampuni ya Statoil yenye mkataba wa kuchimba mafuta nchini Tanzania baada ya kutokea kwa mkanganyiko kwa baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari zilizokinzana kuhusu Kampuni hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Yona Killagane. (picha: Benedict Liwenga/Maelezo)
Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. James Andilile (kushoto) akijibu maswali toka kwa waandishi wa habari waliohudhuria Mkutano uliohusu Kampuni ya Statoil yenye mkataba wa kuchimba mafuta nchini Tanzania baada ya kutokea kwa mkanganyiko kwa baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari zilizokinzana kuhusu Kampuni hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Yona Killagane. (picha: Benedict Liwenga/Maelezo)


Na Winner Abraham -- SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limetoa ufafanuzi kuhusiana na Kampuni ya Statoil, yenye mkataba wa kuchimba mafuta nchini Tanzania baada ya kutokea kwa mkanganyiko kwa baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari zilizokinzana kuhusu kampuni hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzani (TPDC) Bw. Yona Killagane ameeleza taarifa zilizo sahihi kuhusu kampuni ya Statoil na mikataba yake mbalimbali na Serikali katika upataji wa faida kutokana na utafutaji wa mafuta na gesi.

Killagane ameeleza kuwa utaratibu unaotumika katika kutafuta mafuta ni aghali na ni hatari kwa

Zitto: Kuhusu mkataba wa gesi kati ya StatOil na Tanzania

Swali kwa TPDC: Kwanini Makubaliano ni tofauti na Mkataba Elekezi (Model PSA)?

Baada ya kuvuja kwa Mkataba wa kutafuta na kuzalisha Gesi Asilia (PSA) kati ya Serikali kupitia TPDC na Kampuni ya Norway ya StatOil na baada ya baadhi ya wachambuzi kuhoji kuhusu mkataba huo, Shirika la TPDC limetoa maelezo yake. Sio mara moja, sasa ni mara ya tatu. Kimsingi TPDC wanasema wachambuzi waliochambua nyongeza hiyo ya Mkataba hawana uelewa wa mambo haya na wanaleta siasa. Nadhani ni muhimu TPDC wakajikita katika kueleza kwa lugha ambayo wananchi wa kawaida wataelewa badala ya kusingizia uelewa wa watu katika masuala haya. Wizara ya Nishati na Madini haina uelewa wa pekee wa masuala ya Mafuta na Gesi kama wanavyotaka umma uamini. Kuna watanzania wengi tu wenye kufuatilia mambo haya na wenye uwezo mpana hasa katika masuala ya kodi katika tasnia hii. Ni wajibu wa TPDC kutoa maelezo yasiyo changanya wananchi na bora zaidi waweke mikataba hii ya Gesi na Mafuta wazi. Maelezo yaliyotolewa na TPDC mpaka sasa hayaeleweki na yana lengo la kuwachanganya wananchi kama sio kuwaongopea.

Swali la Msingi

Serikali kupitia “Model PSA” imeweka viwango vya mgawanyo wa mapato kati ya Mwekezaji na nchi. Viwango hivi ni vya mgawo wa mafuta au gesi asilia yanayozalishwa kwa siku. Mkataba huu

African Diaspora Policy Forum on "President Obama’s U.S. - African Leaders Summit", August 2014

Prince George's County Africa Trade Office presents the African Diaspora Policy Forum for President Obama’s U.S.-African Leaders Summit in August 2014.

Scholars, experts on African Affairs and business leaders will lead discussions at the African Diaspora Policy Forum in support of President Obama’s U.S.-African Leaders Summit being held in Washington, DC, from August 5-6, 2014, and the mobilization for the Prince George’s County 2nd Annual Gateway to Africa Gala “Promoting International Trade” scheduled for Friday, August 8, 2014.

PUBLIC EVENT: African Diaspora Policy Forum on President Obama’s U.S.-African Leaders Summit in August 2014

WHEN: Monday, July 28, 2014

VENUE: Prince George’s County Economic Development Corporation 1801 McCormick Drive, Suite 350, Largo, MD 20774
(First Floor Conference Room)

TIME: 9am-2pm

For more information: Contact the Africa Trade Office at (301) 583-4650

Waziri Nyalandu akutana na Balozi wa Heshima Issa, California

Balozi wa heshima Mhe. Ahmed Issa akifanya mazungumuzo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu Beverly Hills California mapama leo mazungumuzo yaliyohusu kutangaza Utalii wa Tanzana nchini Marekani pia Waziri Nyalandu alimpongeza Balozi wa Heshima kwa kuendelea kutangaza utalii wa Tanzania kwenye magari yake ya mizigo.
Balozi wa heshima Mhe. Ahmed Issa akifanya mazungumuzo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu Beverly Hills California mapama leo mazungumuzo yaliyohusu kutangaza Utalii wa Tanzana nchini Marekani pia Waziri Nyalandu alimpongeza Balozi wa Heshima kwa kuendelea kutangaza utalii wa Tanzania kwenye magari yake ya mizigo.

Taarifa hii imeshirikishwa wavuti.com na Luke Joe/Vijimambo blogWaziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu (kulia) akizungumza na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani Ahmed Issa juu ya mikakati mbalimbali ya kuvutia watalii wa kimarekani kutembelea Tanzania jana Beverly, Los Angeles.


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani Bw. Ahmed Issa (kushoto) na Abdul Majid baada ya kupokea taarifa ya mikakati wanayoitumia kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania kwa wamarekani jana Beverly, Los Angeles.


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) akiagana na Balozi wa Tanzania wa Heshima wa Utalii nchini Marekani Ahmed Issa mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya masuala kadhaa ya kuvutia Watalii wa Marekani nchini Tanzania jana Beverly, Los Angeles.


Mikakati inayofanywa na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania Ahmed Issa kutangaza utalii ni pamoja na matumizi ya magari yenye picha za vivutio vya utalii wa Tanzania katika miji mbalimbali nchini Marekani ikiwemo California kama inavyoonekana katika picha.

Sera za Liberatus Mwangombe kuhusu Darasa la Kiswahili


Taarifa hii imeshirikishwa wavuti.com na Abou Shatry/SwahiliVilla blog

Tanzania na Korea Kusini zasaini makubaliano ya msaada

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile(kushoto) na Balozi wa Korea hapa nchini Chung IL wakibadilishana hati za makubaliano msaada wa Kimaendeleo ya katika Nyanja za Afya, Kilomo, Elimu na Nishati baada ya kutiliana saini leo jijini Dar es Salaam Katika hafla iliyofanyika katika Ukuimbi wa Wizara ya Fedha. (picha: Frank Shija)

Na Winner Abraham -- Serikali yatiliana saini ya makubaliano ya msaada wa kimaendeleo na Jamhuri ya watu waKorea ambapo katika makubaliano hayo jumla ya Dola za Kimarekani zaidi ya 100 kwa ajili ya mikopo nafuu na dola milioni 10 kama msaada kutoka shirika la Mendeleo la Kimataifa la Korea (KOICA)

Makubaliano hayo yametiliwa saini baina ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile na Balozi wa Serikali ya Korea hapa nchini Chung IL.

Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile amesema kuw a makubaliano hayo yatasaidi katika

Bakhresa Group yaipa Serikali $93,000 kusaidia Timu za Taifa

Kutoka kulia Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Suleiman Nkami, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel, Meneja Chapa wa Kampuni ya Bakhresa Group, Katibu wa Naibu Waziri Bw. Francis Songoro na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Bakhresa Bw. Said Muhammad Said Abeid wakifurahia mara baada ya makabidhiano ya hudi yenye thamani ya Dola za Kimarekani 93,000/= ikiwa ni msaada wa kampuni hiyo kwa wanamichezo wanaoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Scotland.

Na Rose Masaka -- NAIBU WAZIRI wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mhe. Juma Nkamia amemuombammiliki wa kiwanja cha michezo cha Azam Complex Bw. Said Salim Bakhresakutoa ruhusa kwa wachezaji wa Tanzania kufanya mazoezi katikauwanja huo hasa wakati wa usiku ili ziweze kuwa katika nafasi nzuri na zipate uzoefu wa kucheza muda huo.

Hayo yamesemwa leo na Mhe. Nkamia katika kikaocha kukabidhiwa cheki naBw Bakhresayenye thamani ya Dola 93,000 ili kuisaidia timu ya Taifa ya riadha kufika Glasgow, Scotland pamoja na mahitaji mengine kamajezi na vifaa:
“Fedha hii itasaidia timu yetu yenye wachezaji 39 ,makocha, pamoja na walimu waliotoka China kuweza kurudi salama.” 
Aidha, Mhe. Nkamia ametoa pongezikwaRais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuweza kuzungumza na wachezaji hao na kuwakabidhi bendera ya Taifa huko waendako.
Bw. Bakhresa amesema kuwa anaisapoti timu ya Taifa kwenda Scotland kwa sababu michezo siyo mpira wa miguu tu na amefafanua kuwa mashindano ya michezo ni kitu muhimu katika nchi na kinaleta maendeleo.
“Tunachokipata kinatokana na jasho la watanzania na tunakirudisha kwa watanzania,Tanzania inajengwa na watanzania wenyewe siyo watu wa nje”. Alisema Bakhresa.

Taarifa ya CHADEMA ya kikao cha siku mbili

Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itakutana jijini Dar es Salaam kwa siku mbili kuanzia Ijumaa ya tarehe 18-19 Julai, 2014, katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama.

Katika siku mbili hizo, wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA watajadili pamoja na masuala mengine;
  • Mchakato wa Katiba Mpya.
  • Taarifa ya hali ya siasa nchini.
  • Uchaguzi wa ndani ya chama. Taarifa ya fedha, Mpango Kazi na Bajeti.
  • Mapendekezo ya marekebisho ya Katiba, Kanuni na Miongozo ya Mabaraza ya Chama.
  • Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
  • Taarifa ya Katibu wa Wabunge.
  • Rufaa mbalimbali.
  • Nembo na Kadi za Mabaraza ya Chama.
Kikao hicho kitatanguliwa na hotuba ya ufunguzi ambapo vyombo vya habari vinaalikwa kuhudhuria.

Imetolewa leo Alhamis, tarehe 17 Julai, 2014 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari- CHADEMA

Rais Kikwete aanza ziara mkoani Ruvuma

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kamishna wa Polisi Msaidizi Mwandamizi (SACP) Mary Nzuki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Julai 17, 2014 wakati akipanda ndege kuelekea mkoani Ruvuma kuanza ziara ya Kikazi ya wiki moja ambapo atakagua na kuzindua miradi ya maendeleo na kuongea na wananchi. Kati kati ni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi Selemani, Kamanda wa Polisi katika Uwanja huo wa ndege. (picha: Ikulu)

CCM kuzipitia adhabu ilizowapa wawania UraisJana tarehe 16/07/2014 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ilifanya kikao cha kawaida cha siku moja mjini Dar es salaam. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kilipokea taarifa ya mazungumzo yanayoendelea kati ya CCM kwa upande mmoja na CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kwa upande wa pili.

Mazungumzo hayo yanayosimamiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi yana

Mvulana na Mzazi wa msichana walioongoza matokeo ya Kidato cha Sita 2014 watoa sirii ya kufaulu

Isaack Shayo, aliyefanya vizuri kitaifa katika masomo ya Sayansi

Mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa katika masomo ya Sayansi, Isaack Shayo ameweka wazi mbinu alizozitumia kufanikisha ufaulu wake.

Akizungumza na gazeti la HabariLeo na NIPASHE jana nyumbani kwao jijini Dar es Salaam, Isaack (20) ambaye alihitimu Shule ya Sekondari ya St Joseph’s Cathedral alisema, pamoja na mbinu nyingine, aliwasumbua walimu kutafuta maarifa na pia alihangaika kujitafutia vitabu.

Isaack yumo kwenye kundi la watahiniwa 10 bora kitaifa kwa masomo ya Sayansi na pia kwenye kundi la wavulana bora kitaifa katika masomo hayo. 

Kijana huyo ambaye alikuwa akichukua masomo ya Fizikia, Kemia na Hisabatu (PCM), alisema aliamini anaweza kufaulu lakini hakufahamu ni kwa alama zipi. Katika matokeo yaliyotangazwa jana, amepata alama 4. Fizikia amepata B+, Kemia A, Hisabati A pamoja na Sayansi ya Kompyuta (somo la ziada) amepata A. 

Alisema chanzo cha yeye kupata ufaulu huo ni