Jaji adai fidia ya milioni 300/= kwa ajali ya uzembe wa dereva

Jaji wa Mahakama Kuu, Grace Mwakipesile amefungua kesi ya madai ya kulipwa fidia ya Sh milioni 300 kutokana na majeraha na maumivu aliyoyapata katika ajali aliyoipata mkoani Shinyanga.

Amefungua kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya dereva Kamota Hassan, Michael Mosha na kampuni ya bima ya Zanzibar. Kesi hiyo itatajwa Agosti 4 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa.

Katika hati ya madai, Jaji Grace anaiomba mahakama iamuru walalamikiwa hao wamlipe fedha hizo kutokana na ajali anayodai ilitokana na uzembe wa dereva Hassan aliyekuwa anaendesha gari aina ya

Obama to rename Washington Fellowship for Young African Leaders program for Nelson Mandela

WASHINGTON (AP) -- A program designed to foster a new generation of young African leaders will be renamed after former South African President Nelson Mandela, the White House said Sunday.

President Barack Obama, who has said he was one of the untold millions of people around the world who were inspired by Mandela's life, is set to announce the name change at a town hall-style event on Monday in Washington with several hundred young leaders from across sub-Saharan Africa.

The youngsters are participating in the inaugural Washington Fellowship for Young African Leaders, part of the broader Young African Leaders Initiative that Obama launched in 2010 to support a

Taarifa za hivi karibuni kuhusu ugonjwa wa dengue

Gazeti la Mwananchi limechapisha habari kuwa kasi ya kuenea kwa homa ya dengue hapa nchini imepungua baada ya taarifa kuonyesha kuwa hakuna mgonjwa mpya kuanzia Julai 15.

Dk Vida Mmbaga, mtaalamu wa Kitengo cha Epidemiolojia cha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, alisema kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo ambao umeathiri watu 1384, inaendelea kupungua.

Alisema hadi sasa hakuna mgonjwa aliyelazwa wala kubainika kuwa virusi vya ugonjwa huo.

Alisema hii ni mara ya tatu kwa homa ya dengue kuibuka nchini. Mara ya kwanza ilikuwa Julai 2010, Juni 2013 na mwaka huu ambao umesababisha madhara zaidi.

Dk Vida alisema tangu kutokea kwa ugonjwa huo ni watu wanne tu kutoka Dar es Salaam waliopoteza maisha.

Job opportunity at StatOil: Senior License Adminstrator

Senior License Adminstrator (38902)

Statoil is an international energy company with operations in 35 countries. Building on more than 40 years of experience from oil and gas activity on the Norwegian continental shelf, we are committed to accommodating the world's energy needs in a responsible manner, applying technology and creating innovative business solutions. We are headquartered in Norway with approx. 21,000 employees worldwide, and are listed on the New York and Oslo stock exchanges.

Development Production International (DPI) is responsible for Statoil’s existing international comprehensive portfolio of producing assets and planned field developments. DPI focuses on building business clusters and maximizing the value of our producing fields internationally.

In 2007 Statoil signed a production sharing agreement (PSA) for Block 2 with Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) and the Government of Tanzania. Statoil Tanzania AS is the

Ilani mpya ya kutupa taka...?


Agizo muhimu kwa wazazi, walezi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Zanzibar kuhusu sherehe za Eid ul Fitr

Taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkadam Khamis


Kwa mnasaba wa sherehe za eidul fitr, jeshi la polisi linatoa mwongozo kwa wenye familia na kwa wale wanaotarajia kutembea na watoto wao siku za sikukuu, wawaandikie watoto wao namba za simu za wazazi/walezi na kuzihifadhi katika mifuko ya mashati au suruali au sehemu nyengine yoyote ili iwarahisishie kazi jeshi la Polisi kuweza kujua mtoto na mzazi/mlezi wake na kuweza kuharakisha mawasiliano kwa haraka

Taarifa ya Dk Chami kuhusu habari ya kifo cha mfanyakazi wa ndani

Cyril Chami
Cyril Chami

Juzi, blogu kadhaa zilichapisha habari ifuatayo:


Mfanyakazi wa ndani wa mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini Ciril Chami(CCM) aitwaye Mariam Said (16) amefariki dunia mapema alfajiri ya jana ikiaminika kwamba kifo chake kimesababishwa na kipigo toka kwamke wa Mbunge Chami.

Sababu kubwa imeelezwa kuwa binti huyo ambaye ni muislamu alikataa kata kata kwenda kuhudhuria misa kanisani.

Msimamo wa binti huyo ulimpelekea kipigo kikali, na hata mashuhuda walioshuhudia kipigo hicho cha kikatili kwa huyo binti.

Mke wa Mbunge inasemekana aliwajibu mashuhuda kwa lugha ya kejeli na kuwaambia hakuna mtu anaweza kumfanya chochote hata akimwua, kwani serikali ni yao, na CCM ndiyo inayoongoza dola, kwamba mahakama yetu, polisi wa kwetu, hakuna kima atakayenigusa.

Alifoka mke wa Chami.

Kufuatia habari hiyo, Mhe. Chami ametoa taarifa fuatayo:


Mimi Dr Cyril August Chami, Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM) napenda kueleza masikitiko yangu kwa taarifa za uzushi na za kutunga kuwa eti mke wangu asiye na jina amemuua mfanyakazi wetu Mwislamu kwa sababu "marehemu" alikataa kwenda kanisani.

Mimi sina mfanyakazi wa jina hilo la Mariamu. Wala sina mfanyakazi mwenye umri wa miaka 16. Hatuna tatizo lolote la mfanyakazi yeyote kupigwa, achilia mbali kuuawa.

Lakini taarifa hizo ambazo ni za uongo mtupu zimewashtua wengi kwa sababu zimejengwa katika

Statement by Tanzanian Government regarding ongoing killings in Gaza

PRESS STATEMENT


In a Press Conference held on 14th July, 2014, the Minister for Foreign Affairs and International Co-operation, Hon. Bernard Membe, on behalf of the Government of the United Republic of Tanzania called on Israel and Hamas to ceasefire immediately, adding that The United Nations Security Council should step in to restore harmony in the Middle East.

The Government of the United Republic of Tanzania wishes to reiterate this position and

Tanzanian Mirror Journal wishes its readers a blessed EIDDear Tanzanian Mirror Journal Readers, 

We would like to wish you and your loved ones a blessed EID.

May Allah bless your home with happiness, your heart with devotion, your soul with purity today and always. 

EID Mubarak.

Baada ya Hospitali ya IMTU, Serikali tena yakifungia chuo cha afya

Siku moja baada ya Serikali kuifungia kwa muda usiojulikana Hospitali ya Chuo cha Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU), kinachohusishwa na utupaji wa viungo vya binadamu mithili ya takataka, Serikali mkoani Rukwa nayo imekifungia chuo cha Rukwa College of Health and Allied Sciences.

Moja ya sababu ya kukifungia chuo hicho ni kutokuwa na kibali cha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii huku mitaala ya kozi zake ikiwa haipo, kwa maana ya kupitwa na wakati.

Kutokana na kasoro hizo, Serikali ya mkoa kupitia Idara yake ya Afya imezuia wanafunzi wa chuo hicho kufanya mazoezi ya vitendo katika Hospitali ya Mkoa na nyingine mkoani hapa.

Chuo hicho kinachomilikiwa na Umoja wa Kuendeleza Wanawake Mkoani Rukwa (RWAA) ambacho kipo Kanondo, nje kidogo ya Mji wa Sumbawanga, kwa sasa wanafunzi wake wa

Mushi, Mongi wapandishwa kizimbani kwa lile tukio la kushabulia basi la Magereza kwa risasi huko Mikocheni, Dar


Watu wawili wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la kushambulia gari la magereza kwa risasi, wamepandishwa kizimbani juzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni wakikabiliwa na mashitaka matatu.

Watuhumiwa hao, Peter Mushi (36) dereva na Godlisten Mongi (40) ambaye hati ya mashitaka imemtambulisha kwamba ni mhandisi, walipandishwa kizimbani jana kwa mashitaka ya kula njama, unyang’anyi wa kutumia silaha na shambulio la kudhuru mwili.

Wakili wa Serikali, Matarasa Alungo alidai mbele ya Hakimu Anipha Mwingira kwamba Julai 2 mwaka huu, maeneo ya Mikocheni karibu na Hospitali ya Regency, Kinondoni, washitakiwa walikula

Serikali itafuta usajili wa madhehebu yenye migogoro ili kuepusha shari

Mathias Chikawe, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mathias Chikawe, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Pichani ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na maelfu ya Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa yaliyofanyika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam leo.

Waziri Chikawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo aliyataka Makanisa nchini kudumisha amani na utulivu na kuendelea kuliombea Taifa na kuepuka kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo itasababisha taifa kuingia katika uvunjifu amani makanisani. 

Aidha, Chikawe aliongeza kuwa migogoro katika Makanisa na Madhehebu mbalimbali nchini imekuwa mingi katika kipindi hiki ambapo migogoro hiyo inasababishwa na ubinafsi wa viongozi, kutofuata Katiba na Ubadhirifu wa mali za Kanisa. Kutokana na migogoro hiyo Chikawe alisema:
“Serikali haitavumilia vitendo vya uvunjifu wa amani makanisani na ikibidi itafuta usajili wa madhehebu na makanisa yenye migogoro ili kuepusha shari”. 

via blogu ya Wizara 

Serikali yazungumzia madai ya THTU na CWT kuhusu nia ya kupunguza mafao ya pensheni kwa Wanachama wa LAPF na PSPF

Mkurugenzi wa Sheria wa SSRA, Ngabo Ibrahim (katikati), akiandika taarifa hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka na Meneja Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde.

Na Dotto Mwaibale - SERIKALI imekanusha tamko liliotolewa na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisiza Elimu (THTU) na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) la kudai kwamba kuna mpango wa kupunguza Mafao ya Pensheni ya wanachama mifuko ya LAPF na PSPF.

Akizungumza Dar es Salaam leo Kamishna wa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Saul Kinemela

[picha] Shindano la Vodacom Dance 100 lapamba moto

Kikundi cha Wakali Sisi kutoka Kinondoni wakionyesha umahiri wao katika Viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam, katika shindano la Dance miamia ,liloandaliwa na East Africa TV na kudhamini wa Vodacom Tanzania.

Kikundi cha Worries cha Kimara jijini Dar es salaam, wakitoa burudani kali wakati wa shindano la Dance miamia lililofanyika katika Viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.Shindano hilo lilishirikisha makundi 18 kutoka katika wilaya ya Kinondoni,kikundi kitakachoshinda katika shindano hilo kitajinyakulia kitita cha shilingi milioni 5.

Mshiriki mwingne aaga nyumba ya Tanzania Movie Talents

Washiriki walioingia kwenye Jua la Utosi wakiwa mbele ya Meza ya Pilato huku mshiriki mmoja kutoka kwa washiriki hao aliyaaga mashindano ya TMT.

Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar es Salaam.

Hatua ya mchujo katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limeingia wiki ya tatu ya mchujo sasa mara baada ya mshiriki mmoja kuaga shindano hilo wiki hii. Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limekuwa shindano bora ambalo kadri siku zinavyozidi kwenda linazidi kuteka nyoyo za watanzania wengi waliopo ndani na nje ya Nchi kutokana na utofauti wake na uzuri wake pia.

Mshiriki mmoja ambaye ni Pendo Edward aliweza kuchomwa na jua la utosi lililompelekea kutoka

Wanamuziki wapamba uzinduzi wa kampeni ya Shuga Redio

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Sekondari wakiwemo Shule ya wasichana Iringa wakiendelea kumiminika kwenye viwanja vya Samora mkoani Iringa.
Stella Shubi kutoka Clouds Media (kulia) akibadilishana mawazo na Afisa Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumba kabla ya kuanza kwa sherehe za uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio uliofanyika kwenye viwanja Samora mjini Iringa.

Ukatili! Shangazi amuunguza mtoto wa miaka 4 sababu ya kiaziMtoto Fabiani Masumbuko (4) mkazi wa tarafa ya Butundwe wilayani Geita anadaiwa kunyanyaswa kwa kuunguzwa mikono yake na shangazi yake kwa kile kinachodaiwa kuwa mtoto huyo alichukua kiazi kitamu bila ridhaa yake na kukichoma kwenye moto ili baadaye akile kutokana na njaa aliyokuwa nayo.

Tukio hilo limetokea tarehe 4 mwezi huu ambapo hadi sasa hivi shangazi wa mtoto huyo hajafahamika alipo mara moja baada ya kutenda unyama huo na kutoroka huku wasamaria wema waliomkuta mtoto huyo walimchukua na kumpeleka hospitali.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Geita George Rweyemela amesema kuwa

Raia Mwema: Vigogo wa Upinzani mbioni kutimkia...

KATIKA hatua itakayowatikisa vigogo wa Upinzani, wabunge kadhaa wa kambi hiyo wamo mbioni kuikimbia, Raia Mwema limeambiwa.

Wabunge hao wanatarajiwa kuhama vyama vyao vya sasa na kujiunga na chama kipya cha upinzani wakati wowote kuanzia kumalizika kwa Bunge Maalumu la Katiba (BMK), taarifa zinasema.

Wengi wa wabunge hao wanatoka katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Mashariki na Ziwa Magharibi na gazeti hili limeambiwa kwamba maamuzi tayari yamekwishakufanyika, kinachobaki sasa ni tukio lenyewe.

Chama wanachotajwa kuhamia wabunge hao ni kile cha Alliance for Change and Transparency (ACT) kinachohusishwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe.

Zitto mwenyewe hajahamia katika chama hicho lakini mmoja wa maswahiba wake kisiasa, Samson