[video] Lipumba, Wasira, Lissu: Nani anataka kuwazuia Watanzania kupata Katiba Mpya - Mdahalo ITV


Ufafanuzi kuhusu aina ya ajira zilizositishwa katika Idara Uhamiaji

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA YA KUSITISHWA KWA AJIRA ZA KONSTEBO NA KOPLO WA UHAMIAJI ILIYOTOLEWA JANA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI HAIHUSIANI NA AJIRA 70 ZILIZOTOLEWA KWA NAFASI YA MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI


Baadhi ya Vyombo vya Habari leo tarehe 29 Julai, 2014 vimeandika kwa makosa kuwa ajira za Uhamiaji zilizositishwa jana zinahusiana na 70 zilizopatikana baada ya usaili uliofanyika katika Uwanja wa Taifa.

Ukweli ni kuwa usaili wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji ambao awali ulianzia Uwanja wa Taifa ulienda vizuri hadi wakapatikana wasailiwa wa kujaza nafasi 70 za Mkaguzi Msaidizi wa

Yericko Nyerere: Ninaunga mkono Israel kuitetea na kuilinda nchi yao ya ahadi

Madai ya Waisraeli yanaanzia katika misingi ya kidini ambapo katika Biblia (kitabu kitakatifu kwa Wakristo na Wayahudi), kitabu cha kwanza cha nabii Musa kiitwacho Mwanzo sura ya 12 inaonesha jinsi Ibrahim anavyoitwa na mwenyezi Mungu ili kumtumikia.

Eneo hilo la Palestina (zamani lilijulikana kama Kaanani)ndiyo chimbuko la dini kuu tatu zenye msingi wa Ibrahim ambazo ni dini ya Wayahudi, Ukristo na baadaye Uislam.

Dini ya wayahudi yenye misingi ya Biblia Agano la Kale likianza na vitabu vitano vya Musa (Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Mambo ya Walawi na Kumbukumbu la torati), Ukristo ukianza misingi kwenye Agano la Kale hadi Agano Jipya na Uislam ukishika vitabu vinne Tourat ya nabii Musa (a.s), Zabur ya nabii Dawood (a.s), Injili ya Issa bin Mariam (a.s.) au Yesu na Quran ya Muhamad (s.a.w)

Ibrahim mwenyeji wa Uru wa Ulkadayo (Mesopotamia) leo Iraq wa kabila la Waebrania anahama kutoka Iraq na kwenda Haran Syria na baadaye kutelemkia Kaanani (Uyahudi) ambapo Mwenyezi Mungu anamtokea katika njozi na kumwapia Ibrahimu kuwa ardhi yote hiyo amepewa yeye na

North Korea reopens international summer camp for kids 300; Campers from Tanzania, Russia, China, Vietnam, Ireland attend


About 300 campers from multiple nations are in North Korea to attend the country's only, and newly revamped, summer camp. (Wong Maye-E/Associated Press)

Summer camp in North Korea? It's got one — and it's got everything from giant water slides and a private beach to video games and volleyball courts. Oh, and, of course, a big bronze statue of the late leaders Kim il-Sung and Kim Jong-il surrounded by adoring children.

After some on-the-spot guidance from North Korea's new leader, Kim Jong-un, and a major face-lift, the Songdowon International Children's Camp reopened Tuesday for this year's flock of foreign campers — more than 300 young children and teenagers from Russia, China, Vietnam, Ireland and Tanzania.

The campers spend the eight days cooking, swimming, boating and mingling with their North Korean

South Korea: African officials value Saemaeul Movement

George Sempeho, an official for the U.N. Millennium Village Project in Africa, delivers a speech on the Saemaeul Movement at KOICA headquarters in Seongnam, Gyeonggi Province, Tuesday. / Courtesy of KOICA

Officials from African nations involved in an U.N. project to fight poverty and develop economies across the continent found the Saemaeul Movement to be "extremely practical" during their stay here, according to the Korea International Cooperation Agency (KOICA), Tuesday.

A total of 19 manger-level officials from Malawi, Ethiopia, Uganda, Kenya, Tanzania and Senegal — participated in a program offered by KOICA, a foreign assistance organization, to promote adoption of Korea's rural development campaign from the 1970s.

KOICA invited the participants, who work under the U.N. Millennium Village Project (MVP), from

Mpigie kura mshiriki umpendaye TMT


Taifa Stars safariki Afrika Kusini kwa mechi ya marudiano

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Msafara wa watu 27 wa kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kinaondoka kesho (Julai 30 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya Air Tanzania kwenda Afrika Kusini ambapo kitapiga kambi ya siku mbili kabla ya kuingia Maputo kuikabili Msumbiji (Mambas).

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itawasili saa 9 asubuhi kesho (Julai 30 mwaka huu) kwa ndege ya Fastjet kutoka Tukuyu mkoani Mbeya, na baadaye jioni kuunganisha safari ya Afrika Kusini.

Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itachezwa Agosti

Sherehe za Eid-ul-Fitr DMVBalozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania wa DMV na marafiki zao waliohudhuria sherehe ya Eid iliyofanyika siku ya Jumamosi Julai 28, 2014 Wheaton, Maryland nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiwa katika picha na Watanzania wa DMV na marafiki zao katika sherehe ya sikukuu ya Eid iliyofanyika siku ya Jumatatu July 28, 2014 Wheaton, Maryland nchini Marekani. Picha zote kwa hisani ya Missy Temeke.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TAMCO na Watanzania waliohudhuria sherehe ya Eid.Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiongea na mmoja wa Watanzania wa DMV (kulia) wakati sherehe ya Eid iliyofanyika Wheaton, Maryland nchini Marekani siku ya Jumatatu Julai 28, 2014 na kuhudhuriwa na Watanzania wa DMV na marafiki zao. Aliyepo katikati ni afisa wa masuala ya uhamiaji Bwn. Abbas Missana.

Ili kuona picha zaidi bofya bofya hapa.

---
Imeshirikishwa na Luke Joe/Vijimambo blog

Wachina waondoka na dhahabu wananchi wabaki na uharibifu

WACHINA walifika katika Kijiji cha Lupa Market wilayani Chunya, wakajizolea dhahabu, wakaondolewa, manufaa pekee kwa kijiji ilikuwa uharibifu mkubwa wa mazingira ya Mto Lupa na Zira huku wananchi wake wakiendelea kujichimbia kwenye umasikini.

Zaidi ya Wachina 13 walivamia Mto Lupa na Zira katika Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya. Wakiwa na mitambo ya kisasa, wakajichimbia dhahabu kwa gharama ya maisha ya Watanzania masikini waishio kwenye vijiji vilivyomo kwenye mabonde ya mito hiyo.

Wachina hao kutoka kampuni ya uchimbaji madini ya Epoch Mining Tanzania Ltd waliweka mitambo minne; miwili katika kila mto. Mitambo hiyo ilikuwa ikielea majini mithili ya pantoni ambapo wenyeji waliita meli.

Hadi wanaondolewa, si serikali ya kijiji, wilaya wala mkoa waliokuwa na taarifa ya kiwango cha

Key points on How to write a perfect resume for any jobLearn and avoid these 40 street scams!

40 Tourist Scams to Avoid This Summer

Mhamiaji haramu akamatwa na mitambo ya kutengeneza fedha bandia

Raia wa Kongo, Ambanipo Siva (33) jana alikiri mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Frank Moshi mashitaka aliyosomewa na Wakili kutoka Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania, Patrick Ngayomela kuwa anaishi nchini bila kuwa na kibali.

Hata hivyo Wakili Ngayomela alishindwa kumsomea maelezo ya awali, kwa kuwa alidai mshitakiwa huyo alipokamatwa, alikutwa akiwa na mitambo ya kutengenezea dola bandia za Marekani.

Wakili Ngayomela aliiomba Mahakama iruhusu mshitakiwa arudishwe Polisi ili ahojiwe waone kama watamuongezea mashitaka au la. Hakimu Moshi aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 12 mwaka huu, kesi itakapotajwa tena. 

Awali, Ngayomela alidai Julai 24 mwaka huu katika eneo la Mbezi Beach Wilaya ya Kinondoni, Siva alikutwa akiishi nchini bila kuwa na kibali. Alirudishwa rumande.

via HabariLeo

Albert Sanga: Tumefika pazuri, akili zitakujaHivi karibuni kulikuwa na habari iliyotikisa vyombo vya habari hasa kwenye mitandao ya kijamii iliyohusu usaili wa idara ya uhamiaji. Idara hiyo ilitangaza nafasi zisizozidi sabini lakini walioitwa kwenye usaili walikuwa waombaji zaidi ya elfu kumi (10,000). Usaili ule ulifanyika kwenye uwanja wa taifa kiasi kwamba ukitazama zile picha ungedhani lilikuwa ni rundo la watazamaji wa mpira wa miguu.

Tukio lile lilizua hisia tofauti miongoni mwa wengi, wengi wakimwaga lawama kwa serikali na kuonesha hofu yao kuhusu tunakoelekea na hili tatizo la ukosefu wa ajira. Binafsi nilipoliona tukio lile nililitazama kwa jicho jingine na nilifurahi, kuona tumefika mahala pazuri kama utakavyoona kwa kadiri ninavyoendelea kuchambua hapa.

Kwanza ifahamike kwamba tatizo la ukosefu wa ajira lipo dunia nzima. Hata zile nchi zinazotufadhili tatizo hili linawatafuna kule kwao. Mathalani ukosefu wa ajira nchini Marekani ni asilimia 6.1% na

Uingereza ni asilimia 6.8%, ilhali Tanzania ni asilimia 11.7%. Kwa hiyo tunapolitazama tatizo hili tuhakikishe tunalipatia sura ya kidunia kitu kitakachotusaidia kufikiria na kupata majibu halisi kwa mujibu wa hali inayoendelea ulimwenguni pote.

Katika nchi nyingi zilizoendelea na hata katika mataifa mbalimbali yanayoendelea Afrika ikiwemo Misri, Nigeria, Tunisia na nyingine; ukosefu wa ajira ndio ulioboresha ujasiriamali. Baada ya kuona ajira hakuna, baada ya kuona serikali imeelemewa, wananchi wengi katika mataifa hayo walianza kuumiza vichwa namna ya kujikwamua kama mtu mmoja mmoja. Ndipo ubunifu wa biashara, kuona fursa ndogo na kubwa kulipoendelea kuwa sehemu ya utamaduni na maisha ya kila siku kiuchumi.

Kinachowafanya vijana wengi katika nchi yetu Tanzania, kutoona namna ya kujiajiri ni kwamba bado shida hazijawapiga ipasavyo na kama zimewapiga ipasavyo basi bado hawajazinduka. Wengi wa vijana wetu wanapomaliza masomo yao bado hawajafikia hatua ya kukosa chakula, kukosa pa kulala na pengine kukosa mavazi.

Hata wakiwa hawana ajira wanakula, wanapo pa kulala na wanavaa vizuri. Wanamudu haya kwa sababu jamii na familia zetu nyingi bado tuna utamaduni wa kijamaa. Kijana anahitimu masomo yake leo lakini anaweza kuishi kwa mjomba, kaka, dada, mzazi, binamu, mtu wa kutoka eneo moja; hata kwa mwaka mzima akila, akilala na akivaa eidha kwa kisingizio cha kutafuta ajira ama kwa kigezo cha “kwa sababu hana ajira”.

Huu mtindo unachangia sana kudumaza akili za ubunifu kwa vijana wetu wasomi, hawaoni fursa kwa sababu hakuna kitu kinachowalazimisha kuziona. Shida, matatizo na changamoto ni kani (nguvu) zenye mchango mkubwa kumsukuma mtu kuziona fursa.Kwa kadiri shida, matatizo na changamoto zinavyozidi kuwa kubwa ndivyo ambavyo uwezekano wa mtu kuona fursa ndogo ndogo unavyozidi kuongezeka. Kama hujabanwa vizuri na matatizo ni rahisi kudharau fursa fulani fulani.

Hebu tujiulize hadi sasa ni vijana wangapi wanahitimu vyuo vikuu na kuthubutu kwenda kutafuta vibarua vya kukata majani ya mifugo kwa wafugaji? Ni wasomi wangapi baada ya kukosa ajira wamediriki kuanza biashara ya kutembeza maji mitaani, kwenye stendi na sehemu zenye watu?

Tunao vijana wangapi wahitimu wa shahada, stashahada na vyeti wenye nguvu na afya zao ambao baada ya kukosa ajira wameamua kukaa kwenye masoko mbalimbali kufanya tenda za kushusha mizigo? Niambie tuna vijana asilimia ngapi ambao wanauthubutu wa kuweka tai zao chini na kuamua kuwafuata wenye maduka ili wawe vibarua wa kusogeza mizigo stoo? Kilimo kinalipa, lakini ni vijana wangapi wenye shahada zao ambao wanaweza kuweka vyeti vyao kwenye makabati kisha wakapiga kambi vijijini huko mashambani kwa ajili ya kulima?

Kimsingi vijana hawawezi kuona kuwa kukata majani ni fursa hata kama wana digrii kwa sababu bado shida hazijawapiga vizuri. Hawawezi kuona kana kwamba kutembeza maji mtaani ni fursa kwa sababu wanapo pa kulala, wanapo pa kula, wanazo simu za gharama zinazowafariji kwa mitandao ya kijamii na bado wanavaa vizuri.

Nakuthibitishia kuwa kijana iwe ana shahada ya uzamili, shahada, stashahada ama cheti, ikitokea mambo yamemuwea magumu kabisa; hana pa kulala, hana pa kula hana mavazi ya kuvaa; hawezi kukataa kazi ya kufyeka majani, hawezi kudharau kazi ya kulima, hawezi kujivunga kwenda kushusha mizigo stendi wala hawezi kudharau fursa yeyote hata kama itamletea shilingi hamsini. Atathubutu, atatenda na atafanikiwa!

Ukienda kule Nigeria ni kawaida kukuta vijana wenye shahada za uzamili na shahada wakipiga rangi za viatu mitaani, wakiuza maji na wakizunguka na bidhaa kiumachinga. Hata kule Misri kilichoibua hasira za maandamano yaliyoung’oa utawala wa Rais Husein Mbarak ilikuwa ni baada ya askari wa jiji kumnyanyasa kijana msomi wa chuo kikuu ambae aliamua kujiajiri kwa kuanzisha banda la ‘umachinga’ baada ya kukosa ajira.

Vijana wasomi kuwa machinga, wapiga debe, wabeba mizigo, wakata majani na wakulima wadogo wadogo; mtu anaweza kusema ni ‘bomu’. Lakini ukweli ni kwamba hiyo ni nukta nzuri. Wasio na ajira (wawe wasomi ama wasiosoma) wanapopatwa changamoto kiuchumi kisha wakawa tayari kuzichangamkia fursa ndogo ndogo na zinazodharauliwa, hiyo ni hatua nzuri sana.

Mara nyingi nimekuwa nikisema na kurudia kuwa tatizo la Tanzania sio ukosefu wa ajira bali kuna umasikini mkubwa wa kifikra unaosababisha watu kutouona uwezo wao wa ndani na kushindwa kuona fursa zinazowazunguka. Hapa ndipo tunapotakiwa kuwekeza sio kumwaga misaada na mikopo ya fedha pekee.

Ongea na vijana(wasomi na wasiosoma), kina mama, na wengine kuhusu kujikwamua kiuchumi; kilio chao watakueleza ni ukosefu wa ajira na kuhusu kujiajiri watakutolea machozi kwamba wanakosa mitaji (fedha). Sasa jaribu kuwachukua vijana wasomi waulize huu ukosefu wa fedha ni kiasi gani kinahitajika katika biashara zipi?Wengi utaona wanakutajia biashara kubwa kubwa za mamilioni ya fedha.

Kitu ninachosema na kusisitiza ni kuwa tatizo la ukosefu wa ajira litaendelea kuwa kubwa mpaka pale wahusika watakapoweza kuwa na ufahamu wa “kiupambanaji” ambao unaiona shilingi elfu moja kama mtaji mkubwa. Bahati mbaya ni kuwa tuna kizazi cha wasomi (na watanzania wengi) ambao utafutaji wa maarifa sio kipaumbele kwao.

Lakini katika kitabu changu, kwenye chambuzi zangu na kwenye semina zangu nimekuwa nikieleza kwa mifano namna unavyoweza kuzalisha fedha pasipo fedha. Hivyo utabaini kuwa sababu nyingine ya vijana wetu wasomi na Watanzania kwa ujumla kulalamika kuwa wanashindwa kujiajiri kwa kukosa fedha (mtaji) ni kwa sababu hawana maarifa ya namna ya kuzalisha fedha pasipo fedha. Maandiko matakatifu yanaonya kuwa “Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa”

Wasomi wetu wana maneno mengi ya kujitetea na kulalamika kwa sababu bado wanaishi kwa falsafa za kale katika zama mpya. Enzi hizo ilikuwa “soma upate kazi” lakini siku hizi ni “soma utengeneze kazi”. Kwa zamani nchi yetu ilikuwa chini kielimu, waliokuwa wakisoma walikuwa wachachena wote ilibidi kupata kazi kutokana na mahitaji.

Siku hizi mwamko wa elimu umekuwa mkubwa, shule na vyuo vinaongezeka kila siku, kwa hiyo ndoto za “soma upate kazi” inazidi kuyeyuka. Msomi yeyote ambaye anasoma kwa mtazamo wa “soma upate kazi” ni rahisi sana kuchanganyikiwa anapoingia mtaani na kukuta kazi hamna.

Kwa hiyo, tatizo hili la ajira linavyozidi kuongezeka, tunavyozidi kuwa na vijana wengi wasomi wasio na kazi mtaani, ndivyo maisha yatakavyozidi kuwa magumu zaidi na zaidi. Huu mtindo wa kijamaa wa kula, kulala na kuvaa kwa mjomba, kaka, binamu; unazidi kuisha kutokana na ugumu wa maisha.

Maisha yanapozidi kuwa magumu kwa waliokosa ajira, wajomba wanapoendelea kuchoka kulisha na kulaza wasio na ajira; itakuja nukta ambayo aliekosa ajira hatakuwa na namna isipokuwa kuziona fursa hata zile fursa ndogo ndogo zinazodharauliwa ziwezazo kumuokoa kiuchumi. Hapo ndipo ninaposema tumefika pazuri, kwa sababu akili zitakuja.

Hili wimbi la ukosefu wa ajira halina haja ya kulihofia kwa sababu hizi akili za watanzania wengi haziwezi kubadilika tusipopitia tunapopita sasa. Vijana wetu wamekuwa wavivu wa kubuni, hawana maono kuhusu kesho zao, wamekuwa mabingwa wa kuchagua kazi, wana ndoto za maisha makubwa ya kulala masikini na kuamka matajiri, hawana utamaduni imara wa kujifunza na kujisomea kuyajua maisha halisi kutwa kucha wanahangaika kuota maisha ya ‘mamtoni’, maisha ya kwenye filamu na maigizo. Akili kama hizi sio rahisi sana kubadilika mpaka shida ziwachakaze kisawasawa, hapo ndipo watazinduka.

Kwenye kitabu changu cha “Ni wakati wako wa Kung’aa” katika sura inayoeleza namna mtu unavyoweza kuzalisha fedha pasipo kutumia fedha, nimeeleza nguvu mbili ziitwazo “Push power” na “Pull Power” zinavyowasukuma watu kutafuta mafanikio. Nimeeleza kuwa unapokuwa katika matatizo makubwa halafu kukawa hakuna namna unayoweza kutulia ama kurudi nyuma, hapo unatakiwa kutumia “push power”.

Hii ni nguvu ambayo inaambatana na mtu pale anapobaini kuwa akitulia na kulia-lia matatizo yatammaliza; hivyo anaamua kupambana. Na anapokuwa akipambana huku akijua kuwa alikotoka ni kubaya na hakufai kurudi, basi hataacha kupambana zaidi na zaidi.Wakati utakuja ambapo mtu aliekosa ajira yeye mwenyewe atainuka kwenda kuchakarika pasipo kuililia serikali.

Kuna mazingira ambayo serikali imekwisha yaandaa yanayoweza kuwasaidia watu kujiajiri lakini hayajatumika kwa asilimia 100%. Kabla ya kuilalamikia na kuililia serikali hebu yatumike kwa asilimia 100%. Lakini hili tatizo la ukosefu wa ajira tupende ama tusipende litatuletea akili za kujitegemea na kupambana.

Inawezekana kila Mtanzania kuwa mshindi wa kiuchumi!

Makala hii imeandikwa na:
Albert Sanga, 
Iringa.
0719 127 901 

Shule yawafukuza Walimu 4 na Wanafunzi 2 sababu ya 'ngono'

Inaripotiwa kuwa Shule ya Sekondari ya Mwembetogwa ya Mjini Iringa imepongezwa kwa kuwafukuza kazi walimu 4 wa kiume waliobainika kuwa na mahusiano ya kimapenzi ("fataki") na wanafunzi wao wa kike.

Mkuu wa shule hiyo, Kevin Mlengule amenukuliwa akisema kuwa pamoja na walimu hao shule iliwafukuza wanafunzi wa kike 2 waliobainika kukubuhu kwa ngono.

Alisema kura ya siri iliyopigwa dhidi yao ndiyo iliyowabaini walimu na wanafunzi hao kuwa